Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Mteule akiwa mwiba mchungu kwa watawala Nchini basi haongezewi hata sekunde 5 ofisini.
Kila la kheri Assad.
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.

Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.

Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Desemba,2014

-----------------------

Hii ndo ikulu inaandika hivi?
 
Nilisikia CAG huwa hawastaafu, ina maana utaratibu huo umebadilishwa au?
 
Assad ni mwalimu wangu na nimjuavyo mm si mtu wakuyumbishwa na mtu wa msimamo sikuzote husimamia ukweli nakumbuka nilipokua nikisoma udsm 2004 alikua mkemeaji mkubwa wa matumizi mabaya yaliyokua yakifanya na uongozi wa Luhanga makamo mkuu wa chuo by then hakuogopa kufukuzww kazi alikua akiwapa makavu black and white, nimpambanaji nakumbuka alipopambana mpaka darasa lete la AC100 lilipogaiwa into two kutokana na kufurika kwa wanafunzi mpaka wengine wakawa wanasimama na kukaa ktk vidaka vya ngapi vya theatre s
Si dhani kama he can be compromised in any situation given his faith and professional ism and im certain he will rather be step down with respect and dignity than be hiding the truth or intermingled in dirty and culpritic manuevours

Sina tatizo kabisa na Mteuliwa,ni mtu mwenye uwezo na sifa kushika nafasi husika. Tatizo langu ni timing ya uteuzi,anaye teua akiwa amebakisha muda mfupi madarakani! Tunafahamu kwamba Utoh alikuwa ameongezewa muda ili aondoke na mkuu! Ubishi wake wa kugomea uchakachuaji wa ripoti ikabidi astaafu kwa mujibu wa sheria.Ripoti ilifanyiwa uchakachuaji lkn ulikua wa kumuondoa Rais na Wizara ya Fedha ktk scandal hii. Nadhani ndilo kosa la aliye kuwa anakaimu!
Serikali haiendeshwi kwa dhana.
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.

Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.

Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Desemba,2014

-----------------------

10313732_648287681948876_6001176764329198945_n.jpg

Huyu Rweyemamu boga kabisa..headed paper ya kiingereza content ya kiswahili..huyu kasoma wapi pimbi huyu?
 
mbali na cv yake kuwa nzuri laki profesa tez kazidi udini mpeni pole maana kiala anaeteua sasa kwa asilimia kubwa swala tano yangu macho sasa
 
ukweli unauma ndo maana unatukana, mimi sina mda wa kubishana na wewe fanya utafiti wa wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa na aliowaacha utakubaliana na mimi ukizingatia wakristo ni wengi kuliko waislam
 
mnaoponda maprofesa....semeni mlikuwa mnataka uteuzi wa

Hawa Ghasia au Assumpta Mshana au Silinde????

mkuu jaribu kuwa makini na majina ya watu kuna lusinde (ccm) na silinde (chadema) ni watu wawili tofauti
 
mbali na cv yake kuwa nzuri laki profesa tez kazidi udini mpeni pole maana kiala anaeteua sasa kwa asilimia kubwa swala tano yangu macho sasa
Kuna tatizo mtu akiwa ni swala tano? so unataka atuteulie walevi na wezi uridhike
 
ukweli unauma ndo maana unatukana, mimi sina mda wa kubishana na wewe fanya utafiti wa wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa na aliowaacha utakubaliana na mimi ukizingatia wakristo ni wengi kuliko waislam
Wakristo wanajichotea pesa za umma kama zao,mda umefika nao wakafanye biashara wajue ugumu wa kuzipata hela.
 
liwekeni hilo vichwani mwenu siku hazigandi na mtalopoka sana
 
ukweli unauma ndo maana unatukana, mimi sina mda wa kubishana na wewe fanya utafiti wa wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa na aliowaacha utakubaliana na mimi ukizingatia wakristo ni wengi kuliko waislam
 
Wewe unasumbuliwa na chuki na roho ya husda tu.

Tatizo la makafiri wengi ukichaguliwa sehem nzuri kama hizo lazima wakuundie Zengwe halafu kama ukishakuwa mtu wa msimamo kama prof Assad ndio kabisaaaa
ImageUploadedByJamiiForums1417534373.424054.jpg
 
Mwana Mpotevu

Tunaomba rekebisheni Cv yake vinginevyo yafuatayo yatavuma haraka:
1.Miaka ya 2000 Dkt Assad aliwahi kufanya mitihani ya NBAA ili kupata CPA(T) akafeli na aliamua kuandaa kitabu kupinga NBAA
2.Kwenye CV yake hakuna popote palipoandikwa kuwa Dtk Asaad ni CPA(T) holder na inaonyesha kuwa yeye hana practise yoyote ndani ya uhasibu na wala jina lake halipo
3.Hata hivyo zipo taarifa kuwa Asaada alipewa CPA(T) kwa kumuheshimu tu . Kwa vyovyote vile tunaomba NBAA waonyesha Asaad ana status gani kwenye ngazi ya Uhasibu??Maana kuna yafuatayo
(i) Graduate accountant [CPA(T)]
(ii)ACPA(T)
(iii)FCPA(T)
Je katika ngazi hizo Dkt Asaadi yupo wapi???
Kama hakuna maana yake yeye hawezi kufanya na kusimamia kazi kama CAG.
Afadhali angepewa acting CAG
Sio kweli ,ASSAD ni ACPA, huwezi kuwa ACPA bila ya kupractice,ndio maana una jaza logbooks kazi ulizofanya ili uweze kuwa associate, pia ASSAD ana audit firm, NBAA hakuna CPA ya heshima, huwezi kuwa na audit firm kama sio ACPA-PPS (External auditor) na kuendelea mfanO FCPA-PPS
 
Hivi huyu aliyeandika ili tangazo ana-capacity kweli ya kutosha?! angalia level ya degree za mteuliwa - Uzamivu (PHD) badala ya Uzamivu (PhD), halafu Uzamivu (Master's) badala ya Uzamili (Master's). nafikiri hii inaonesha namna gani humo Ikulu watu wasivyokuwa makini.
NI Makosa ya kibinaadamu
 
Back
Top Bottom