NasDaz,JokaKuu,
Sina shaka kwamba tunapoteza mapato mengi sana, hilo halina ubishi. Kwamba hivi sasa serikali hawajui au wanafanya makusudi jibu ni kwamba wanafahamu na ndio maana wakati tunaingia kwenye mining economy, hapakuwa na taasisi inayohusika na ukaguzi ndipo baadae baada ya kugundua tunaibiwa ndipo wakaanzisha Mining Audit Agency. Aidha, kwavile serikali iligundua kwamba vidani ni moja ya njia zinazotumika kuiba ndipo ikapitishwa sheria ni gramu ngapi za vidani zinakuwa accepted kama ni for personal use na ikizidi, unahesabika kwamba ulitaka kutorosha madini! Na kwa kupitia njia hii, kuna vidani vya billions of TZS pale Airport vimekamatwa ambavyo zamani vingehesabika kwamba ni vidani for personal use.
Pamoja na yote hayo bado am very certain kwamba bado tunapoteza mapato mengi kwenye sekta ya madini. Nimekupa mifano ya hapo juu ili kujibu hoja yako kwamba je, serikali haifahamu au wanafanya makusudi! Lakini hata hivyo, bado mkuu wangu tatizo lako ni lile lile ..hujioni kabisa kwamba nawe(kama Mtanzania) ni sehemu ya tatizo la nchi hii! Wengi tunalalamika serikali serikali huku tukisahau wajibu wetu! Kama utakumbuka mimi na wewe tulishawahi kuwa kwenye mjadala mzito kuhusu ufaulu Tanzania .wengi wetu kama ilivyo ada, tukasahau wajibu wetu tukawa tunabaki kulalama kuhusu serikali. Kama unakumbuka, wakati tunahitimisha mjadala ule, uliniuliza nina maoni gani kuhusu nini kifanyike ili kuongeza ufaulu. Nikakujibu kwamba lazima kila mmoja atimize wajibu wake! Mwanafunzi lazima atimize wajibu wake wa kusoma kwa bidii. Mzazi lazima atimize wajibu wake wa kumsimamia mwanae na kuhakikisha ana-behave like a student. Mwalimu nae atimize wajibu wake badala ya kuendelea kusingizia maslahi madogo kama kigezo cha kutotimiza wajibu! Mwisho serikali nayo itimize wajibu wake! Aidha nika-conclude kwamba hata kama utakuwa na shule bora kuliko zote duniani zenye kila kitu lakini mwalimu, mzazi na mwanafunzi wakishindwa kutimiza wajibu wao; itakuwa ni kazi bure! Kwa bahati mzuri, ukiangalia matangazo ya HakiElimu hivi sasa yanasisitiza uwajibikaji wa wadau tofauti kabisa na zamani ambapo matangazo yao yalikuwa ni kama vile wanafunzi walikuwa perfect, walimu perfect, wazazi perfect lakini tatizo lilikuwa serikalini pake yake! HakiElimu kwa sasa nao wamegundua kwamba pamoja na matatizo yote ya serikali lakini bado kuna tatizo la wadau (wanafunzi, wazazi na walimu) kutowajibika! JokaKuu, sio kwamba nataka kujifagilia lakini nitasema na kama utaona najifagilia, kimpango wako. Kuna wakati mimi niliwahi kufanya kazi NMB na kwa bahati mbaya kabisa nilikuwa nalazimika kufanya kazi nyingi zaidi peke yangu. Ilipokuwa inafika mwisho wa mwezi, nilikuwa naingia ofisini saa kumi, nimechelewa sana saa kumi na moja alfajiri. Nilikuwa nalazimika kufanya hivyo kv nilikuwa nalazimika mishahara ya wafanyakazi inalipwa on time na vile vile nihakikishe naandaa na kuwakilisha monthly reports on time! Na wala si kwamba nilikuwa nafanya hayo kwa ajili ya posho; manake hadi natimuliwa NMB, hakuna kitu ambacho nilikuwa naona uvivu kufanya kama kuandikia Claim ya Sitting Allowance! Simple rule, hakuna atakayekuandikia Sitting Allowance wakati pesa ni zako mwenyewe!! Lakini pamoja na yote hay ohayo, huwezi amini, kuna wapumbavu pale ofisni walikuwa wanasema napenda sifa kwavile tu nilichokuwa nafanya ni wajibu wangu! Hili ndilo tatizo letu, hatupendi kuwajibika lakini ni wepesi sana wa kuilalamikia serikali! With due respect Sir, mkuu wangu JokaKuu nawe ni hodari sana wa kuilalamikia serikali! Je, huwa unatimiza wajibu wako? Na uki-maximize uwajibikaji, kuna wapumbavu watakuchukia na kukuona mpenda sifa!
JokaKuu,NasDaz,
..bado tunaendelea kupoteza mapato hata baada ya kuunda mining audit agency.
..as a country we need to do more kuhakikisha tunapata mapato zaidi kutoka ktk sekta hiyo.
..kwa kifupi serikali inatakiwa iongeze vyanzo vya mapato, ipunguze upotevu wa mapato, na zaidi ipunguze matumizi.
..Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani, Dr.Ndalichako, alisema serikali ilifanya makosa kufungua shule za sekondari bila kuwa na waalimu na vitabu na maabara. Hilo ndilo tatizo la msingi kabisa la elimu nchini kwetu, hayo mengine unayozungumzia ni secondary tu.
NB:
..kuna tofauti kati ya kutekeleza wajibu wako ktk nafasi yako ya kazi, na kutekeleza wajibu wako kama raia wa kawaida.
..mimi natekeleza wajibu wangu kama raia kwa kuikosoa, kuishauiri, na kuihimiza serikali yetu na Chama tawala. tatizo ni kuwa wakati tunatekeleza wajibu wetu wanatokea wakina NasDaz wanatuchukia na kutuona walalamishi.
Kila sehemu mambo yanaenda spidi huku simiyu tenda zinatangazwa kibao ujenzi na uthamii kila kona unaendelea hakika jk anafanya kazi kweli kathubutu kaweza na sasa anazidi kusonga mbele.Kikwete unafanya kazi na kazi inaonekana Mungu akubariki. Ndugu Salary Slip ahadi zinatekeleka. Hapo kibaha maeneo ya viziwaziwa Rais alikuwa ameahidi maji na kweli tenda ilitangazwa mwezi julai mwaka huu na tayari mkandarasi keshaanza kupima. Naamini hata kwa maeneo mengine kazi zinafanyika. chama je huko gongo la mboto hali ikoje. Ritz atatujuza ya town senta.
Kukata tamaa? Come on men, sina huo msamiati akilini mwangu....nafanyaga kuusikia tu kutoka kwa watu!! Ninachosema na ambacho nitaendelea kusisitiza ni Watanzania kuwajibika; wengi wetu hatupo responsible na tunaamini uwepo wa serikali ndo basi tumekasimu kila kitu....mambo yakienda hovyo, tunalalamika kwamba serikali hii wakati wenyewe hatutekelezi wajibu wetu!! GOvernment performance is all about collective individual responsibility, accountability and commitment to what everyone does! Hii collective individual responsibility, accountability and commitment ndiyo inazalisha aggregate government/country performance. Dunia hii hakuna sehemu ambako hakuna rushwa lakini kwanini wengine wanaendelea ingawaje kuna rushwa na ufisadi? Asian countries ni very corrupt, tena kule ni hizi grand corruption as compared na zilizojaa huku za polisi, mahakamani na hospitalini lakini bado wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo compared to African countries; WHY? The answe is simple, jamaa wapo responsible and commited!! Wanachukua chao mapema na bado wanapiga mzigo!!!Thnx! ndg yangu NasDaz kwa ufafanuzi Nimetolea mfano wa wa2 weupe 7bu wao wameshauzoea mfumo huo naamini pia unawasaidia kila uchaguzi wananchi wanapima Utendaji hata hapo GHANA wanaotawala sasa wanajua wakivurunda kipindi cha 1 watang'olewa! maBADILIKO yanaanza na mtu 1 Ila ninavyokusoma km umekata tamaa! kwamba hata 2kibadili CHAMA hakuna kipya kitakachotokea hapana cc wanaNCH 2natakiwa 2lazimishe watawala wafanye 2navyotaka sio wanavyotaka! 7bu % Kubwa ya waAFRICA ni waLEVI wamadaraka so yapasa 2wamulike
Mkuu August,
Nimetaja mambo mengi ikiwa ni pamoja na hayo uliyoyataja hata kama nitakuwa nimeyataja in other way round. Tatizo letu ni kwamba tunasahau kwamba na sisi Watanzania ni sehemu ya Tanzania!! Hao viongozi unaowataja hawatoki mbinguni bali wanatoka miongoni mwetu....huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! Anakuwa sawa na wale wale kwa sababu nae ni sehemu ya tatizo lakini hajajigundua kwamba nae ni tatizo kubwa nchi hii! Hili halipo Tanzania tu bali karibu nchi zote za Afrika, utafikiri tumepigwa laana! Waafrika wote ni sehemu ya matatizo ya Afrika! Hata kule ambako wameshafanya mabadiliko mara kadhaa bado kuna matatizo kibao coz' wale wapya wanaopata nafasi ya kuongoza nao walikuwa ni sehemu ya tatizo!!
Salary Slip,
..wakati Raisi Kikwete anatangaza "nia" ya kujenga reli, Raisi Uhuru Kenyatta atakuwa na ground breaking ceremony ya ujenzi wa reli toka Mombasa kuelekea Uganda na Rwanda kesho.
cc Koba, Ritz, Mchambuzi, Kubwajinga
...hapa nakubaliana nawe. na mdau mkubwa kwenye hili unamjua!Hivyo basi, hoja ya Ndalichako kwamba serikali ilifanya kosa kujenga shule nyingi kabla ya walimu ni sahihi kwa maana moja kubwa; ilichangia kuongeza mass failure lakini sio msingi wa tatizo....msingi wa tatizo ni wadau kutokuwa RESPONSIBLE!!
...si kweli kwamba tuna limited budget, as far as tunataka kuboresha elimu nchini. tukipunguza upotevu wa fedha za serikali, refer report za CAG, itakuwa ni moja ya njia. pili, hata kwenye sekta yenyewe, kuna upotevu wa fedha za maendeleo. hakielimu wametafiti na kutoa repoti juu ya hili.Now turudi kwenye hoja yenyewe ya Ndalichako! You have limited budget, you either start building schools or start training teachers! Acording to Ndalichako and many others, unaanza ku-train teachers! Then ushakuwa na (say) 10,000 teachers at disposal; then what next? Unawamwaga mtaani wakati mnasubiria shule kujengwa or what? Or hata shule ambayo requirement ni walimu 20, unapeleka walimu 40 ili mradi kila mmoja awe na ajira ili wasiwa-disappoint wengine wanaotaka kuingia Ualimu kwa kuona pamoja na kwamba vyuo vinadahili walimu wengi lakini wote wanaishia mtaani? Sio siri, Ualimu ni taaluma isiyopendwa na wengi lakini cku hizi wengi wanaenda Ualimu kwa sababu wanafahamu kuna uhakika wa ajira.....so, ni situation gani ingekuwa created kwa kusomesha walimu wengi halafu hawana kazi kwa sababu wanasubiri shule zijengwe? By the way, anakaa mtaani halafu miaka minne baadae ndo anaenda kwenye shule; huyo atakuwa mwalimu tena au mhitimu wa chuo kikuu mwenye cheti cha ualimu?!
...nadhani jibu la unlimited budget liko kwenye hii bolded point ya pili. hiyo ya kwanza ni tafakari ya muhimu sana, ambayo, luckly ni subject ya vitabu kadhaa siku hizi.Government performance is all about collective individual responsibility, accountability and commitment to what everyone does! Hii collective individual responsibility, accountability and commitment ndiyo inazalisha aggregate government/country performance. Dunia hii hakuna sehemu ambako hakuna rushwa lakini kwanini wengine wanaendelea ingawaje kuna rushwa na ufisadi? Asian countries ni very corrupt, tena kule ni hizi grand corruption as compared na zilizojaa huku za polisi, mahakamani na hospitalini lakini bado wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo compared to African countries; WHY? The answe is simple, jamaa wapo responsible and commited!! Wanachukua chao mapema na bado wanapiga mzigo!
Good, now let's do it this way.......si kweli kwamba tuna limited budget, as far as tunataka kuboresha elimu nchini. tukipunguza upotevu wa fedha za serikali, refer report za CAG, itakuwa ni moja ya njia. pili, hata kwenye sekta yenyewe, kuna upotevu wa fedha za maendeleo. hakielimu wametafiti na kutoa repoti juu ya hili.
...taaluma hii haipendwi kwa kuwa tumeitelekeza. na majibu tunayaona kwenye kufeli wanafunzi, ubora hafifu wa mazao ya elimu, inayopelekea kuwa na upungufu wa skilled workers ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
...NazDaz, nadhani kimkakati, issue si kusomesha walimu, bali kuboresha mazingira ya sekta hii ili kuvutia watu wenye uwezo mzuri kuwa walimu au kusomea ualimu. in short, incentives.
...hakuna nchi duniani utaenda wakakwambia wana unlimited budget for education. its all about strategic management of these resources chache tulizonazo.
Khaaa! Wee JokaKuu....mbona unaongea kama mwanasiasa wa kwenye majukwaa ambao kazi yao ni propaganda? Nani kasema mwalimu hataki? Nimesema walimu sitaki au nimesema nini kinatakiwa kuanza whn u've limited resources while facing multiple objectives?! Unaleta vituko vingine; kwamba sitaki uongozi ubadilike; mie ya kubadilika au kutobadilika yananihusu nini?! Mkuu wangu JokaKuu, am telling you from deep inside my heart; and am saying this in front of God and am very certain tht He(God) knows my conscious is clear. Ninachotaka kusema ni kwamba; I don't care who's in power....whether CCM or CHADEMA, I don't care! Kwangu mimi CCM na CHADEMA wote ni wale wale tu!! CCM mwizi na fisadi wa leo wakati CHADEMA some1 else ni mwizi na fisadi wa kesho!! Kama ni kuangalia political issues am more interested na combination ya bunge na wala sio nani yupo Ikulu! Am always praying isije kutokea tukawa na bunge ambalo limehodhiwa na chama kimoja kama ilivyo sasa....I believe, kukiwa na combination mzuri basi huko kutatokea watu wenye uchungu wa kweli na nchi hii; watu wanaotaka kuwajibika....kwa sababu tofauti yangu mimi na nyinyi ni moja na ndio maana hatufikii muafaka! Nyinyi mnaamini kwamba tatizo ni CCM na serikali yake kwahiyo mnajidanganya kwamba CCM wakiondoka nchi itabadilika kuwa ni nchi ya maziwa na asali....!! BInafsi mimi siamini katika hilo unless unitajie nchi moja ya mfano barani Afrika ambayo baada ya kubadilisha uongozi, nchi ikabadilika na kuwa inayotiririsha maziwa na asali!! BInafsi, naamini matatizo ya Waafrika yanafanana kutoka nchi moja hadi nyingine! Waafrika wengi ni watu wa hovyo hovyo, hatupo committed na responsible! wengi ni wezi na wala rushwa! Kwahiyo kitu cha kwanza muhimu kuliko vyote ni kubadilika..tukibadilika; jamii ina maana jamii mzima itabadilika na kuwa na responsible societies, committed societies, non-corrupt societies! Ukishakuwa na jamii kama hiyo basi hata viongozi watakaotoka kwenye jamii husika ni responsible nd committed leaders, non corrupt leaders...kinyume chake ni kama unamtoa fisadi nyangumi madarakani na kisha unamwingiza fisadi papa coz' hata wale unaowaingiza watakuwa wanatoka kwenye jamii ile ile ya hovyo hovyo....yaani jamii ya hovyo hovyo unaitarajia kutoa viongozi wenye maadili...gimme a break!!NasDaz,
..waalimu mashuleni, hutaki.
..kubadilisha uongozi, hutaki.
..kila kitu wewe hutaki.
..maandiko yako yanaonyesha kwamba u dont want to try anything different frm what we r currently implementing.
..ndiyo maana wachangiaji wengine tunaona UMEKATA TAMAA.
Nafahamu kwamba it can take the time!! Ngoja nikuambie kitu kimoja! For those who believe in God, Mungu alimshushia Nabii Mussa Torati! God was very smart, aliishusha Torat kwa sababu za msingi....alifahamu wakati ule Wayahudi walikuwa mafedhuli kweli kweli; akafahamu kwamba hawa ukiwapekekea sheria laini laini hawa; hawatabadilika! Akawaletea TOrat,ambayo in fact, ni full dictatorship constitution! Akaja Yesu, Mungu akadhani wanadamu wameshabadilika, akashusha katiba laini laini ambayo tunaiita INJILI! Katiba ambayo inahubiri kwamba mwenzako akikupiga kofi shavu la mkono wa kushoto, mgeuzie na la kulia akupige! Baadae Mungu akashituka tena, akagundua wanadamu bado ni waovu; na ktk sisi tunaoamini in Islam, akaja Muhammad na Katiba kama ile ile ya Mussa...!! Now tell me; yale zile adhabu zilizo kwenye Torati au Quran ingekuwa ndo zinatekelezwa hapa hapa duniani, ni wangapi wangeiba wakati wanafahamu ukidakwa; watu wanakula mkono wako! Wangapi wangekuwa wazinzi wakati wanajua wakidakwa; you get stoned to death?Niliamua kuwa member wa JF kwaajili ya Mijadala km hii yakuongezeana UFAHAM. ndg NasDaz,nikweli ili 2we na Taifa linalojitambua nilazima kila m2 awe7bu ya mabadiliko anayoyatamani lkn kwa Njia unayoipendekeza huoni km itachukua KARNE nyingi kufikia huko? ukichukulia kwa ss hakuna tena UZALENDO PESA MBELE kwanini 2sianzie angalau hii njia ya mkato yakuwatoa watawala kila wanapovurunda! Badala yakusema wt ni wale wale mfano CCM wanaoena AIBU cdhani chama kingine kitakuwa na Dhambi hiyo kwann 2sianzie hapo!!
Unajuwa wakati naisoma post yako, nikajiuliza "mbona mkuu August ame-personalize sana hoja yake?" Ikabidi nirejee nione nimeandika nini, nikakuta nimeandika "..huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! " Anyway, it's just an example, don't take it personal!!Mkuu Nas, kauli uliyo weka hapa ni ya kukataa tamaa kwamba hakuna mtu anayeweze ku mzuri au mtendaji mzuri, ndio maana umeweka mfano kwamba hata mimi nikipata hayo madaraka nitafanya hivyo, lakini ningependa kukuhakikishia licha ya binadamu wote kuwa na mapungufu yetu, lakini kwangu mimi, siwezi kuchukua rushwa hata ya 1m usd, or even 1m tshs, nitengeneza hasara kwa nchi kwa kutengeneza barabara mbovu, au kuuwa uchumi , au kwa kuleta dawa mbovu, ambayo ndio hulka ya viongozi wengi wa Tz, sijui Kenya, na hata Mwl alivyo kuwa south South commission aliwahi kuliongelea hilo kuwa ni weeakness kwa nchi nyingi za afrika, lakini niaminie kwamba kweangu mimi the Big picure ndio desire yangu na kujenga mahekalu nk kwa kuuwa uchumi ni uzumbukuku mkubwa ambao sote tuna takiwa tuupige vita. Commission siwezi kukata kupokea lakini sio Rushwa ambayo siwezi ku i declare,
But sisi hatupo Responsible, from Top to Bottom....lakini yote kwa yote; niseme tu kwamba thx kwa kufanya quotation zisizoumiza kichwa kujibu manake kuna moja ya kwako ilibidi niipotezee....ilikuwa kila nikiingaliaaaaa; mnh! hamu inaisha hapo hapo ya kujibu....lol!...nadhani jibu la unlimited budget liko kwenye hii bolded point ya pili. hiyo ya kwanza ni tafakari ya muhimu sana, ambayo, luckly ni subject ya vitabu kadhaa siku hizi.
Ndugu yangu Nas huo mfano ulioweka hauniti hofu wa personalisation , hofu yangu ni pale mtu unapokosa kuangalia unapotoka na unaelekea wapi yaani kuwa na plan ya the way fwd.Unajuwa wakati naisoma post yako, nikajiuliza "mbona mkuu August ame-personalize sana hoja yake?" Ikabidi nirejee nione nimeandika nini, nikakuta nimeandika "..huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! " Anyway, it's just an example, don't take it personal!!
Tukija hoja ya Kukata Tamaa naona wengi wanairudia rudia hadi najiuliza kwanini watu wanaona kama suala la kubadilika ambalo mimi nasisitiza watu hawalitaki!!!!! Ina maana hatuwezi kubadilika no matter what? Ina maana hatuwezi kuwa responsible society no matter what? Sasa huko si ndo kukata tamaa kwenyewe mkuu wangu???!! Let me put it this way, SIJAKATA TAMAA, but I don't trust many of African Politicians!!!! Most of these guys wanatoka kwenye jamii ambayo tayari ni ya hovyo.....jamii ambayo ukifanya kazi mwaka mmoja halafu ukajenga ghorofa, watu wanakusifia na kukuona una miakili ile mbaya! Wanakusifia ingawaje wanajuwa kwamba pesa zenyewe ni za magumashi!!! Hawa wanasiasa wetu wanatoka kwenye hizi jamii!! So, how do you expect the polluted society to give the good leader? Ndiyo unaweza kukutana na honest guys/leaders lakini wengi wanakuwa majanga!! Lakini jamii ikibadilika, ama kwa kutaka au kwa kulazimishwa na mfumo; basi tutapata good leaders coz' hawa watakuwa wanatoka kwenye good society!
Halafu kuna hoja yako juu kabisa ambayo umesema "kauli uliyo weka hapa ni ya kukataa tamaa kwamba hakuna mtu anayeweze ku mzuri au mtendaji mzur..." Hapo naomba niongee kwa kifupi sana! Hapa sio suala la kuwa na mtu mzuri na mtendaji mzuri but it's all about having GOOD SOCIETY ambayo ipo very commited, responsible and non corrupt society....SIO MTU!! YES, tunaweza kupata mtu mzuri na mwenye maadili kama MALAIKA, then What? Assume anakuwa ndo President, after 10 years, anaachia ngazi...then? Tunarudi business as usual!!! Au anakuwa mchapakazi na mkali kama Hayati Mwalimu Nyerere...after 10 years, anaondoka ofisini; then what? Business as usual kama ilivyokuwa baada ya kuondoka Nyerere!!! It's far better to have a bad leader in a good society than to have a good leader in a bad society! This bad leader can be held accountable by his good society but one good leader can't hold accountable the whole bad society.