Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Hivi mpango wa ubinafishaji reli ya kati uliohasisiwa na mkuu kwa mbwembwe nyingi na waziri wa miundo mbinu wa wakati huo umeishia wapi? While Kenya are lunching their sustainable ambitious vision 2030 including Konza city project, Grand East Africa railway etc, sie bado tuna nia kila siku nia. Uhuru anataka defining legacy of his presidency by implementing that project, sie bado nia nia tu.
 
MkamaP, Salary Slip

..lakini JK alishatangaza hii "nia" in 2011.

..sasa tangu wakati huo serikali imefanya nini?

..kwanini in 2013 anarudia kutangaza "nia" aliyokwisha tangaza hapo awali??

..kwanini hatendi??

..wakati mwingine nalazimika kukubali kwamba kuna justification ktk hizi dharau na kejeli toka kwa majirani zetu wa Afrika Mashariki. Uongozi wetu umekuwa wa maneno-maneno tu kama hizo "nia" zinazotangazwa na viongozi wetu.

..someni hapa:Tanzania, Rwanda, Burundi team up on $5bn rail proposal

cc Geza Ulole, Nguruvi3

JK ahadi zote alishazimaliza sasa hao ndugu zetu wa SIMIYU kawapa ahadi zile zile lakini zenye remix, Anaziboresha na kupaka rangi ahadi za zamani zionekane ni mpya na sio zile za zamani.
 
..Reli hiyo inajengwa mradi unaanza wakati wowote kuanzia sasa.

Hata kama una nia ya kutetea kitu, haiwezi kuwa kwa staili hii, sentesi hii mtu aliye iandika lazima atakuwa amevurugwa sana mpaka hajui hata anachokiandika! Pole sana Ritz kwa juhudi zako!

...inajengwa-Inamaana ujenzi tayari umekwisha anza!
...unaanza wakati wowote kuanzia sasa - yaani ujenzi bado haujaanza ila maandalizi yamekamilika. Je ni kweli?

Hapo JK alikuwa anajitoa kimasomaso baada ya kuona wenzake wanapanga na kutekeleza ndani ya muda mfupi. Endelea kutumika wakati wenzetu wanasonga mbele.
 
[B FaizaFoxy,

..OK, nime-copy taarifa toka link uliyoileta.

..nadhani kichwa cha habari ni kwa ajili ya kuvutia wasomaji.

..JK bado yuko katika hatua ya kutangaza "nia" ya kujenga.

..Wajapani wanadai tubakie na gauge iliyopo mpaka 2030 na wataleta wataalamu wa feasibility study.

..in the middle of the article unayonitaka niisome, mwandishi anadai nchi washirika wa mradi watafute funds ili ujenzi uweze kuanza.

..majuzi napo Rwanda wamechomoka na kuachana na mradi wetu, sasa wanataka kujenga reli kuelekea Uganda na Kenya.

..sasa hebu tueleze tufuate kipi hapa?!!

[/B]

cc FaizaFoxy
Mkuu JokaKuu,
Kwanza nitamke wazi kwamba linapokuja suala la ujenzi wa reli na miundombinu mingine, Watanzania wengi tunageuka kuwa makengeza ama kwa makusudi yanayotokana na ushabiki wa kisiasa ama kwa kutokujua. Ni bahati mbaya sana katika analysis zetu huwa tunajilinganisha na watu wengine; this's completely wrong!

Watu wengi tumekuwa hodari wa kuponda linapokuja suala la kutokuwa na reli lakini wakati tunaponda tunaponda tunasahau mambo mengine ya msingi. The best manager ni yule anayefanya rational decision pale anapokabiliwa na multiple objectives...hili wengi wetu tunalisahau! Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa budget constraint; hili ndo tatizo la msingi hasa pale manager anapokabiliwa na multiple objectives! Tusijitie upofu, nchi hii ina matatizo lukuki(multiple objectives) na mengi yake kama sio yote tumetoka nayo tangu enzi za uhuru. Mambo ambayo labda yalitakiwa kufanyika in 1960's or 1970 or probably 1980's if not 1990's ndo yanafanyika sasa! Sasa basi, a manager anajikuta kati kati ya nchi kutokuwa na barabara na nchi kutokuwa na reli....hakuna ubishi, yote yana umuhimu mkubwa kwa ustawi wa nchi lakini kwavile ana-operate under budget constraint, huyu manager anatakiwa ku-choose among multiple objectives. A rational manager hawezi ku-opt kujenga reli wakati nchi haina barabara kwa sababu maamuzi yake yanatakiwa kuwa na impact in both sides; economically and socially! Mjerumani wakati anajenga Reli ya Kati hakuangalia social impact kwavile suala la Mnyamwezi kutoka Tabora kuja Dar atumie gari/treni au aje kwa mguu haikuwa juu yake(Mjerumani). Mjerumani huyu alichojali ni kuhakikisha mazao ya aina mbalimbali yanatoka bara hadi Dar es salaam(bandarini); basi! Lakini leo hii kunapokuwa na serikali ya wananchi, decision maker lazima ajiulize; kwamba hata kama tutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka na kwenda bara; what about usafirishaji wa watu/abiria? And what about sehemu zile ambazo reli haitapita hasa tukizingatia hatuna uwezo wa kutengeneza rail networks? Njia ya reli ya kawaida kabisa(cheap) inachukua at least USD 2 million kwa kilometa moja....kwa viwango vya hapa Tanzania, hizo ni sawa na kilometa tatu za barabara ya lami! Hii maana yake ni nini; assume kutoka hapa hadi Mwanza ni kilometa 900; lakini hakuna barabara wala reli. Good enough, kuna 900 billion ambazo ukijenga reli zitaishia Dodoma wakati ukijenga barabara utafika hadi Mwanza!! Kwa mtu anayezingatia socio-economic impacts lazima ata-opt kujenga barabara kwavile anafahamu akija kupata 900 billion zingine; hatazitumia kumalizia reli ya kwenda Mwanza tena bali atazitumia kwa ajili ya kuboresha route nyingine!

Kwa bahati mbaya sana tunapenda kujilinganisha na Kenya huku tukisahau kwamba wakati Tanzania tunahangaika na barabara kuu, wenzetu Wakenya barabara hizo tayari wanazo miaka na miaka! Kwa maoni yangu, Wakenya wamechelewa sana kujenga railway ya kisasa kwavile uchumi wao tayari ungewaruhusu kufanya hivyo more than 20 years ago. Hivyo basi, mtazamo wangu ni kwamba serikali ilifanya uamuzi wa busara kuanza kuangalia roads network kabla ya kuanza na reli...nazungumza hili kwavile siwezi kujitia upofu na kudhani kwamba kuna billions of dollars outta there lakini zinawasubiria akina Kikwete wakazibebe kwenye mabegi na waje kujengea reli! Njia nyepesi ya kufahamu haya mambo ni kuangalia personal planning/budgeting/financing. Watu tujiangalie wenyewe kuna mambo mangapi tunakusudia kuyafanya na tunafanikiwa mambo mangapi na kwanini tumefanya hili na sio lile! Ukiangalia critically utagundua kwamba mara zote ulikutana na multiple objectives wakati upo constrained na bajeti.
 
Last edited by a moderator:
Nas nakubaliana kiasi na mtazamo wako, lakini unatakiwa upimie pia maintenance cost , ambazo wengi wana sema ni unsustainable kwenye matumizi ya barabara kama njia ya kubeba mizigo ukitilia maanani sisi tuna port.
pili impact ya hiyo miradi kiuchumi sema rate of return on investment na time, na other cost savings ambazo zitakuruhusu kuinvest zaidi au kulipa huo mkopo. kati ya mradi wa barabara na reli.
tatu reli ilikuwepo na nyingine tuliongezea tazara na route ya singida, ingawa nyingine haikuwa standard gauge, lakini ilikuwa ina leta alot of cost saving katika usafirishaji, na maintenance ya barabara.
 
NasDaz,

..tatizo la Tanzania ni UZEMBE wa watawala wetu.

..kwamba Kenya alikuwa na miundombinu mizuri in the 90s kuishinda Tanzania, is not a justification kwa sisi kuwa nyuma yao kimiundombinu in 2013.

..Tanzania ina rasilimali nyingi zaidi, na nguvu kazi kubwa zaidi, hatutakiwa kuwa washika mkia ktk eneo hili la Afrika Mashariki.
 
Last edited by a moderator:
Jasusi

Naungana na wewe ni kweli reli ya kati itasaidia sana kukuza uchumi wetu itaunganisha mikoa ya kati mpaka kanda ya ziwa kusafirisha bidhaa.

Mkuu Ritz.
Kukamilika mapema kwa ujenzi wa Reli ya Mombasa-Nairobi-Kampala-Kigali maana yake ni kwamba bandari ya Dsm haitakosa shehena kubwa ya mizigo toka kwa majirani zetu Uganda na Rwanda tu,bali na hapa Tanzania ktk mikoa ya kanda za kaskazini na ziwa!

Wafanyabiashara wetu kutoka kanda hizo watatumia bandari ya Mombasa kwa mizigo yao kusafirishwa kwa kasi na train,na kuisafirisha kwa umbali mfupi na malori.Serikali iimarishe vituo vya forodha ktk mipaka ya Silari Tarime,Namanga,Mutukula na vile vya Tanga na Kilimanjaro. Vitakua busy sana miaka 2 ijayo.
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,

..tatizo la Tanzania ni UZEMBE wa watawala wetu.

..kwamba Kenya alikuwa na miundombinu mizuri in the 90s kuishinda Tanzania, is not a justification kwa sisi kuwa nyuma yao kimiundombinu in 2013.

..Tanzania ina rasilimali nyingi zaidi, na nguvu kazi kubwa zaidi, hatutakiwa kuwa washika mkia ktk eneo hili la Afrika Mashariki.
JokaKuu,
Hapa hakuna suala la ku-justify or anything like that; issue hapa ni kufanya Jambo X at time Y under the available resources!! Issue hapa is all about prioritizing alternatives under available resources; simple like that. Lakini kwa upande mwingine, huwezi ku-ignore ukweli kwamba Kenya tayari walishakuwa na miundombinu msingi kuliko Tanzania kwahiyo hata planning yao itakuwa tofauti tu! Wakati Tanzania sehemu kubwa ya bajeti yake inaenda kwenye barabara, Kenya lazima itaenda kwenye mambo mengine kwavile tayari barabara wanazo; huwezi ku-ignore ukweli huu unless kama unaamini there's somewhere outta there where people can go na kurudi na mifuko ya fedha na kisha kuwekeza kwenye mambo mbalimbali.

Tukija suala la kwamba Tanzania hatutakiwi kushika mkia ukanda huu, nashindwa kukuelewa kwavile Tanzania hatushiki mkia labda kama unamaanisha kitu kingine. Sio siri kwamba Kenya ana-lead lakini Wakenya wenyewe wanafahamu nafasi ya Tanzania...Watanzania tunajidharau wenyewe lakini technically Wakenya wanatuogopa na wanafahamu hawana muda mrefu wa kuwa the leading economy in EA. Angalia data for the past ten years kati ya Kenya na Tanzania ili uone position ya Kenya na TZ.....there's a very wide gap btn two countries lakini gap linapungua mwaka baada ya mwaka; yaani ni kama Kenya anatembea wakati Tanzania inakimbia. Jana nilifuatilia LIVE Coverage ule uzinduzi pale Kenya ambapo Kiongozi mmoja alisema wazi kwamba inabidi ujenzi wa Mombasa uanze mapema coz' wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka TZ ambao nao wapo mbioni kujenga reli of the same quality.

Tukija hilo la uzembe wa watawala wetu, sikatai lakini ni rahisi sana kusema hivyo ukiwa nje (usidhani mimi nipo ndani). Kwenye bajeti ya mwaka huu(2013/2014) nilikuwa na hamu sana ya kuichambua Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwavile wao kama wanasiasa ni rahisi sana kusema "tatizo ni CCM" Nilipoichambua bajeti ile nikakuta ina surplus ya kama shilingi trilioni moja hivi as compared to bajeti ya serikali! Kimsingi nilitarajia iwe ni bajeti iliyoainisha vyanzo vipya vya mapato lakini badala yake nilikuta hiyo additional TZS 1 Trillion wamefanya "ON" and "OFF", yaani walichokuwa wamefanya ni kupunguza kile walichoita posho zisizo za lazima (ingawaje wenyewe hadi leo wanachafuana mitandaoni kwa ajili ya posho) na misamaha ya kodi! Kwangu mimi, bado ongezeko la trillion (tena zisizo na uhakika) ni bado sana. UKiangalia mfano huo, utagundua kwamba tatizo la Tanzania ni zaidi ya watawala na ndio maana mimi nitakuwa mtu wa mwisho nchi hii kuamini eti kuna chama fulani hapa kitakachokuja kuweka mambo sawa wakati watanzania kwa ujumla wetu ni wale wale na viongozi/watawala ni wale wanaotoka kwenye jamii ile ile!!

Tukija upande wa rasilimali, nakubaliana na wewe tunazo za kutosha lakini ukiangalia vizuri, raslimali ya pekee ambayo imekuwa exploited kwa kiasi kikubwa ni dhahabu. Kwa bahati bahati mbaya sana, suala la dhahabu Watanzanai nalo tunaliangalia kwa makengeza; ni ukweli mchungu lakini ndiyo hivyo! Mathalani, hivi sasa ambapo usafirishaji wa dhahabu umepanda, dhahabu inayosafirishwa ni wastani wa tani 40 kwa mwaka....mimi na wewe tufanye ni tani 50. Bei ya dhahabu kwenye soko la dunia haijawahi kufika USD 2000 kwa troy ounce kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita lakini mimi na wewe ngoja tuseme USD 2000 ndiyo bei ya one troy ounce. Pamoja na kwamba tumejipendelea na kusema tunasafirisha tani 50 kwa mwaka, hizo ni sawa na takribani 1.6 troy ounce; kwahiyo ukizidisha kwa USD 2000, ni kama tunaingiza USD 3.2 billion kwa mwaka!! Hiyo ni gross income, less all other costs kisha assume una best mining contracts kisha niambie ungepata Sh. kwa mwaka bila kusahau kwamba figure nilizoweka nimezipandisha.

Hivyo basi, ukiangalia ukweli huo utagundua kwamba raslimali ya madini wala isingeweza kututoa kwenye umasikini. Uchumi wa raslimali za asili is all about what you gonna do with revenues from those resources lakini kwa nchi kama Tanzania ambayo bado haina miundo mbinu ya kutosha, tunalazimika revenues from resources ku-invest kwenye miundombinu badala ya ku-channel kwenye other sectors of economy. Nakubali kabisa kwamba tatizo lingine tulilonalo ni ufisadi na katika hili, hakuna CHADEMA wala CCM, Watanzani walio wengi ni watu wa hovyo hovyo na wezi bila kujali itikadi zao. Atakayekuja kuondoa matatizo makubwa ya nchi hii ni yule anayeamini kwamba Watanzania ni tatizo kuliko nyinyi ambao mnaamini kwamba watawala/CCM ndo tatizo kwavile utawala utakuja kubadilika na watu kudhani kwamba tumepata mwarobaini lakini kinyume chake tukaja kuona yale yale!
 
Last edited by a moderator:
Rais Kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa. Rais amesema reli nyembamba inapatikana eneo la Afrika Mashariki tu.

Mh. Rais kayasema hayo mkoani Simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani.

CHANZO: ITV

MY TAKE:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!

Hizi nia ni mpaka lini?
 
Umeekeza kwa kirefu kuhusu mtazamo wako kwa watanzania na wanasiasa wa kitanzania bila kuweka wazi itikadi yako ya kisiasa.Lakini kwa mtu makini atagundua wewe ni mwana-CCM tena mwenye chuki dhidi ya CHADEMA.

Nyinyi ndio wale ambao mkiulizwa uko chama gani unajibu "mimi sina chama"!
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,

..kwanza umeshajifunga mawazo yako kwamba HATUWEZI.

..sasa ongezea hapo na UZEMBE na UFISADI basi ndiyo maana Tanzania ipo hapa ilipo.

..nitakupa mfano mdogo: hivi kuna sababu yoyote ile ya msingi ya kuwa na mgao wa umeme for 20yrs? tatizo hili limekuwepo tangu JK yupo wizara ya madini na nishati na nimeng'ang'ania mpaka sasa hivi anaelekea kustaafu.

..Tanzania haipigi hatua za kimaendeleo zinazoendana na kiwango cha rasilimali tulizo nazo. hicho ndicho kinachonifanya niamini kwamba ktk eneo hili tumeshika mkia. kwa maneno mengine ni kwamba tungekuwa resource constrained kama wenzetu, halafu ukachanganya na uongozi tulio nao, basi tungekuwa tumeshambaratika kama taifa.

..hiyo budget surplus ya wapinzania if it is something that we can have over a number of years inaweza ku-finance miradi mikubwa ya kiuchumi. tatizo letu ni kwamba watawala ni wezi na wajifunga akili zao kwamba haiwezekani.
 
Mkuu JokaKuu, nashangaa serikali ya JK kusema tunajipanga kila siku.

JK ni waziri kwa miaka zaidi ya 20 mfululizo akiingia katika baraza la mawaziri. Hivi kuna kipi alichokuwa hajui?Sula la reli ya kati ina maana hakuwahi kulisikia likiongelewa.

Umeme ameshiriki sana katika nishati.Unakumbuka IPTL ina mkono wake, hadi leo hajui tatizo la umeme li wapi.Eti anatangaza kuanza kwa reli, nimeshangaa sana!!
 
NasDaz,

..kwanza umeshajifunga mawazo yako kwamba HATUWEZI.

..sasa ongezea hapo na UZEMBE na UFISADI basi ndiyo maana Tanzania ipo hapa ilipo.

..nitakupa mfano mdogo: hivi kuna sababu yoyote ile ya msingi ya kuwa na mgao wa umeme for 20yrs? tatizo hili limekuwepo tangu JK yupo wizara ya madini na nishati na nimeng'ang'ania mpaka sasa hivi anaelekea kustaafu.

..Tanzania haipigi hatua za kimaendeleo zinazoendana na kiwango cha rasilimali tulizo nazo. hicho ndicho kinachonifanya niamini kwamba ktk eneo hili tumeshika mkia. kwa maneno mengine ni kwamba tungekuwa resource constrained kama wenzetu, halafu ukachanganya na uongozi tulio nao, basi tungekuwa tumeshambaratika kama taifa.

..hiyo budget surplus ya wapinzania if it is something that we can have over a number of years inaweza ku-finance miradi mikubwa ya kiuchumi. tatizo letu ni kwamba watawala ni wezi na wajifunga akili zao kwamba haiwezekani.
JokaKuu,
Nimejifunga mawazo kwamba hatuwezi; KI VIPI? Kwanini tusiweze? Ni wapi ambapo nimesema hatuwezi? Ninachosema ni kwamba huwezi kujenga uchumi kwa njia za kufikirika...kwamba kwavile (say) Air Tanzania haina ndege wakati hata Rwanda wana ndege ndo basi tena nasi tununue ndege bila kufanya prioritization...huo utakuwa ni uchumi wa ajabu! Ninachosema ni kwamba we've already messed up for the past 50 years kwahiyo katika mazingira kama hayo ni lazima ufahamu uanze na nini kisha ufuate nini! Umechukulia mfano wa umeme....kuna watu wanadai zamani hapakuwa na matatizo ya umeme huku wakisahau kwamba enzi hizo hatukuwa na demand kubwa ya umeme!! INgawaje umeme uliokuwa unazalishwa haukuwa mwingi lakini bado ulitosheleza kwavile hapakuwa na shughuli nyingi za kiuchumi ambazo zili-demand matumizi makubwa ya umeme!! Zilikuwa ni enzi ambazo ungeweza kuzunguka mtaa mzima na usikute nyumba yenye friji au pasi ya umeme! Baada ya economic liberalization, demand ya umeme ikaongezeka maradufu ndani ya kipindi kifupi wakati uzalishaji ulikuwa ni uleule! Demand ikaendelea ku-shoot year after year na hivi sasa umeme ni moja ya zile multiple objectives ambazo nimezisema awali! Sasa unapokuwa katika mazingira kama hayo ni lazima u-choose among the best alternatives! Huku hakuna umeme, kule hakuna barabara, upande wa pili hakuna maji; mtaa wa tatu, shule na idadi ya wanafunzi vimeongezeka maradufu; ukigeuka upande mwingine unakuta unalazimika kuongeza vituo vya afya...and so on!! Katika mazingira kama hayo, lazima uchague, uanze na kipi na kwa ukubwa gani unless kama kuna sehemu ambako unaweza kwenda kuchota fedha na kumaliza yote hayo kwa pamoja!

JokaKuu, trust me bado nchi hii ina matatizo ambayo wala watu hatujadili ufumbuzi wake! Wanasiasa na wasomi tumekuwa hodari sana wa kukosoa na kullalamika lakini sijapata kusikia msomi wala mwanasiasa yeyote akitoa suluhisho la maana!Kwamba nchi hii kuna rushwa, ni jambo ambalo hakuna anayepinga! Kwamba nchi hii watu ni wazembe, hakuna anayekataa! Kwamba CCM imepoteza mwelekeo, yote sawa tu! hayo ndo maneno ambayo kila siku tunayasewa na lakini wote hawa wanaacha kutaja tatizo la msingi...HATUNA VYANZO VIKUBWA VYA MAPATO! Na ndio maana nikakupa mfano wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani ambayo ilikuwa na nyongeza ya sh. 1 trillion peke yake; hii maana yake ni kwamba kumbe hata wao hawana jipya kv hata kama bajeti yetu leo hii itapata nyongeza ya Sh. 10 trillion, bado ni sawa sawa na hakuna! Itakuwa ni sawa sawa na hakuna kv itakuwa tu ndo inakaribiana na Kenya! Huwezi kusema kwamba Kenya mambo yao mazuri! Hata bajeti yetu leo hii ikiongezeka kwa Sh. 20 trillion, bado hatutaifikia wala kuikaribia angalau bajeti ya South Africa! Lakini bado sehemu kubwa ya SA ni ya watu maskini!!

Hayo yote yanashiria jambo moja kwamba bado kabisa hatujafahamu vyanzo vya msingi vya umaskini wetu na matokeo yake tunaishia kutoa sababu za jumla jumla na hivyo kushindwa kuyaona matatizo ya msingi! TUnaambiwa kwamba wakati wa awamu ya kwanza, kiwango cha rushwa/ufisadi nchini kilikuwa chini sana; lakini bado Tanzania ilikuwa masikini wa kutupwa! Tumeambiwa kwamba kuna karibu Trillion 10 huko Uswisi ambazo zimefichwa....hii maana yake ni kwamba hata kama leo tutazileta zote nchini, bado umaskini utakuwa pale pale! Nikisema hivi si kwamba naweka mawazo kwamba HATUWEZI bali natoa changamoto ya watu kufahamu matatizo ya msingi!

So, nakubali kabisa kwamba Tanzania kuna tatizo kubwa la ufisadi na ukosefu wa uwajibikaji....haya hata mimi nimeyasema sana kiasi cha kutoa threads kadhaa humu jamvini na ku-suggest kufuta mfumo wa Utawala wa Bora kv naamini Utawala Bora kwenye jamii isiyo na maadili kama Tanzania unaweza kutumika kama kichaka cha wezi, wala rushwa, wasiopenda kuwajibika na mafisadi wa aina nyingine. Kama ulishawahi kupitia hizo threads nilishauri Good Governance iwe replaced na Approved Dictatorship Governance! Lakini pamoja na yote hayo, bado tatizo la msingi litabaki palepale kwamba tunahitaji vyanzo vingi na vikubwa zaidi vya mapato na ku-prioritize our objectives. Hili la vyanzo vya mapato huwa hatulijadili kabisa, mara zote tunajadili matatizo!
 
Last edited by a moderator:
Umeekeza kwa kirefu kuhusu mtazamo wako kwa watanzania na wanasiasa wa kitanzania bila kuweka wazi itikadi yako ya kisiasa.Lakini kwa mtu makini atagundua wewe ni mwana-CCM tena mwenye chuki dhidi ya CHADEMA.

Nyinyi ndio wale ambao mkiulizwa uko chama gani unajibu "mimi sina chama"!
Nilikuwa sijafahamu kwamba kumbe nawe ni mtu wa hovyo hovyo sana humu jamvini! Eti nina chuki na CHADEMA, pyuuuu!!! Pole sana, usidhan kwavile wewe unashikiwa akili na wanasiasa basi ndo kila mmoja yupo kama wewe!
 
Watu tunajadili mambo ya msingi kishabiki kanakwamba hili taifa linamilikiwa na kikundi flani na wengine ni wakimbizi. Siasa inapelekea watu kuweka akili zao mfukoni na kutoa mawazo ili mradi kuvutia kule mapenzi yake yalikolalia, kwa staili hii hatuwezi kusogea mbele hata kidogo. Mtu mwenye uwezo wa kukosoa tu bila kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ni mtu mbaya sana. Nawachukia watu wa aina hii.
 
Ni bahati mbaya sana katika analysis zetu huwa tunajilinganisha na watu wengine; this's completely wrong!
...lazima tujilinganishe na wengine, kama tusipofanya hivyo, tutapima vipi maendeleo yetu. kuna kitu kinaitwa benchmaking, unakifahamu.

...sasa, Kenya ndio saizi yetu kujipima nayo, na hata baadhi ya nchi za asia.

...huwezi sema "mimi nafanya vizuri, napata asilimia 60" wakati mwenzako anapata mpaka 85. lazima ujiulize, yeye ana nini mpaka kanishinda/nipita miye? nifanyeje nimfikie au nimpite vilevile?

Watu wengi tumekuwa hodari wa kuponda linapokuja suala la kutokuwa na reli lakini wakati tunaponda tunaponda tunasahau mambo mengine ya msingi.
...reli tunayo! uliza iko wapi! tunakumbuka mambo ya msingi, ndio maana wewe unanun'gunika hapa.

...unafahamu, reli ya kati ilikuwa inabeba mizigo tani ngapi kwa muhula, katika enzi zake? hivi sasa inabeba kiasi gani? mambo ya abiria tuyasamehe kwanza.

The best manager ni yule anayefanya rational decision pale anapokabiliwa na multiple objectives...hili wengi wetu tunalisahau!
...what about the worst one? au hili umelisahau?

Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa budget constraint; hili ndo tatizo la msingi hasa pale manager anapokabiliwa na multiple objectives! Tusijitie upofu, nchi hii ina matatizo lukuki(multiple objectives) na mengi yake kama sio yote tumetoka nayo tangu enzi za uhuru. Mambo ambayo labda yalitakiwa kufanyika in 1960's or 1970 or probably 1980's if not 1990's ndo yanafanyika sasa!
...hili la kushuka kwa ufaulu kwenye shule, tumetoka nalo enzi za uhuru? na la reli kutofanya kazi je? la umeme kukatika ovyo?

Sasa basi, a manager anajikuta kati kati ya nchi kutokuwa na barabara na nchi kutokuwa na reli....hakuna ubishi, yote yana umuhimu mkubwa kwa ustawi wa nchi lakini kwavile ana-operate under budget constraint, huyu manager anatakiwa ku-choose among multiple objectives. A rational manager hawezi ku-opt kujenga reli wakati nchi haina barabara kwa sababu maamuzi yake yanatakiwa kuwa na impact in both sides; economically and socially!
...a rational manager anabaini mahitaji na kufanya lile lenye faida zaidi, politics aside.

Mjerumani wakati anajenga Reli ya Kati hakuangalia social impact kwavile suala la Mnyamwezi kutoka Tabora kuja Dar atumie gari/treni au aje kwa mguu haikuwa juu yake(Mjerumani). Mjerumani huyu alichojali ni kuhakikisha mazao ya aina mbalimbali yanatoka bara hadi Dar es salaam(bandarini); basi! Lakini leo hii kunapokuwa na serikali ya wananchi, decision maker lazima ajiulize; kwamba hata kama tutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka na kwenda bara; what about usafirishaji wa watu/abiria? And what about sehemu zile ambazo reli haitapita hasa tukizingatia hatuna uwezo wa kutengeneza rail networks?
...ungekuwa na uchaguzi wa kurahisisha usafiri wa mizigo au abiria ungechagua upi? maana, huo wa mizigo -kwa maana ya reli au barabara- ndio abiria huutumia. au kuna tofauti siioni?

...nani kasema hatuna uwezo? can this be proven mathematically?

Kwa mtu anayezingatia socio-economic impacts lazima ata-opt kujenga barabara kwavile anafahamu akija kupata 900 billion zingine; hatazitumia kumalizia reli ya kwenda Mwanza tena bali atazitumia kwa ajili ya kuboresha route nyingine!
...nchi za ulaya zisingekuwa na reli, kwa tafsiri hii. reli hazijengwi ili kufurahisha mtu/watu na kupata mtaji wa kisiasa, bali kuleta maendeleo mapana zaidi, kama, kupunguza gharama na muda wa usafirishaji bidhaa, kubeba mizigo mingi na mikubwa kwa pamoja, na hivyo kupunguza gharama za ujenzi na marekebisho ya barabara.

Kwa bahati mbaya sana tunapenda kujilinganisha na Kenya huku tukisahau kwamba wakati Tanzania tunahangaika na barabara kuu, wenzetu Wakenya barabara hizo tayari wanazo miaka na miaka! Kwa maoni yangu, Wakenya wamechelewa sana kujenga railway ya kisasa kwavile uchumi wao tayari ungewaruhusu kufanya hivyo more than 20 years ago.
...where do you get your facts from? hebu tueleze, ukitaka kusema Tz imeendelea unailinganisha na nani? US?

...thika super highway imejengwa miaka na miaka ipi? sasa, kama hufahamu, Moi alipotoka, aliacha barabara nyingi Kenya zikiwa choka mbaya.
...kwa trend hiyo ya "......more than 20 years", nasi tutakuwa lini tayari "uchumi wetu ukiruhusu?"

Hivyo basi, mtazamo wangu ni kwamba serikali ilifanya uamuzi wa busara kuanza kuangalia roads network kabla ya kuanza na reli...nazungumza hili kwavile siwezi kujitia upofu na kudhani kwamba kuna billions of dollars outta there lakini zinawasubiria akina Kikwete wakazibebe kwenye mabegi na waje kujengea reli! Njia nyepesi ya kufahamu haya mambo ni kuangalia personal planning/budgeting/financing. Watu tujiangalie wenyewe kuna mambo mangapi tunakusudia kuyafanya na tunafanikiwa mambo mangapi na kwanini tumefanya hili na sio lile! Ukiangalia critically utagundua kwamba mara zote ulikutana na multiple objectives wakati upo constrained na bajeti.
...usitumia neno "busara" vibaya.

...watu ni tofauti na serikali in many ways! usilinganishe.
 
Watu tunajadili mambo ya msingi kishabiki kanakwamba hili taifa linamilikiwa na kikundi flani na wengine ni wakimbizi. Siasa inapelekea watu kuweka akili zao mfukoni na kutoa mawazo ili mradi kuvutia kule mapenzi yake yalikolalia, kwa staili hii hatuwezi kusogea mbele hata kidogo. Mtu mwenye uwezo wa kukosoa tu bila kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ni mtu mbaya sana. Nawachukia watu wa aina hii.

Jenga hoja kijana badala ya kuongea kiujumla bila kuonyesha kujadili kwa kina nini unapinga na nini unakubaliana nacho.
 
Umeekeza kwa kirefu kuhusu mtazamo wako kwa watanzania na wanasiasa wa kitanzania bila kuweka wazi itikadi yako ya kisiasa.Lakini kwa mtu makini atagundua wewe ni mwana-CCM tena mwenye chuki dhidi ya CHADEMA.

Nyinyi ndio wale ambao mkiulizwa uko chama gani unajibu "mimi sina chama"!

Mkuu naona umegonga mahali panapouma. Ni kweli kwa kumsoma huyu ndugu yetu unafahamu mtazamo wake ni wa kuwatetea watawala badala ya wananchi. Yawezekana kwa namna moja na nyingine anafaidika na utawala wa sasa!
 
Back
Top Bottom