Ni bahati mbaya sana katika analysis zetu huwa tunajilinganisha na watu wengine; this's completely wrong!
...lazima tujilinganishe na wengine, kama tusipofanya hivyo, tutapima vipi maendeleo yetu. kuna kitu kinaitwa benchmaking, unakifahamu.
...sasa, Kenya ndio saizi yetu kujipima nayo, na hata baadhi ya nchi za asia.
...huwezi sema "mimi nafanya vizuri, napata asilimia 60" wakati mwenzako anapata mpaka 85. lazima ujiulize, yeye ana nini mpaka kanishinda/nipita miye? nifanyeje nimfikie au nimpite vilevile?
Watu wengi tumekuwa hodari wa kuponda linapokuja suala la kutokuwa na reli lakini wakati tunaponda tunaponda tunasahau mambo mengine ya msingi.
...reli tunayo! uliza iko wapi! tunakumbuka mambo ya msingi, ndio maana wewe unanun'gunika hapa.
...unafahamu, reli ya kati ilikuwa inabeba mizigo tani ngapi kwa muhula, katika enzi zake? hivi sasa inabeba kiasi gani? mambo ya abiria tuyasamehe kwanza.
The best manager ni yule anayefanya rational decision pale anapokabiliwa na multiple objectives...hili wengi wetu tunalisahau!
...what about the worst one? au hili umelisahau?
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa budget constraint; hili ndo tatizo la msingi hasa pale manager anapokabiliwa na multiple objectives! Tusijitie upofu, nchi hii ina matatizo lukuki(multiple objectives) na mengi yake kama sio yote tumetoka nayo tangu enzi za uhuru. Mambo ambayo labda yalitakiwa kufanyika in 1960's or 1970 or probably 1980's if not 1990's ndo yanafanyika sasa!
...hili la kushuka kwa ufaulu kwenye shule, tumetoka nalo enzi za uhuru? na la reli kutofanya kazi je? la umeme kukatika ovyo?
Sasa basi, a manager anajikuta kati kati ya nchi kutokuwa na barabara na nchi kutokuwa na reli....hakuna ubishi, yote yana umuhimu mkubwa kwa ustawi wa nchi lakini kwavile ana-operate under budget constraint, huyu manager anatakiwa ku-choose among multiple objectives. A rational manager hawezi ku-opt kujenga reli wakati nchi haina barabara kwa sababu maamuzi yake yanatakiwa kuwa na impact in both sides; economically and socially!
...a rational manager anabaini mahitaji na kufanya lile lenye faida zaidi, politics aside.
Mjerumani wakati anajenga Reli ya Kati hakuangalia social impact kwavile suala la Mnyamwezi kutoka Tabora kuja Dar atumie gari/treni au aje kwa mguu haikuwa juu yake(Mjerumani). Mjerumani huyu alichojali ni kuhakikisha mazao ya aina mbalimbali yanatoka bara hadi Dar es salaam(bandarini); basi! Lakini leo hii kunapokuwa na serikali ya wananchi, decision maker lazima ajiulize; kwamba hata kama tutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka na kwenda bara; what about usafirishaji wa watu/abiria? And what about sehemu zile ambazo reli haitapita hasa tukizingatia hatuna uwezo wa kutengeneza rail networks?
...ungekuwa na uchaguzi wa kurahisisha usafiri wa mizigo au abiria ungechagua upi? maana, huo wa mizigo -kwa maana ya reli au barabara- ndio abiria huutumia. au kuna tofauti siioni?
...nani kasema hatuna uwezo? can this be proven mathematically?
Kwa mtu anayezingatia socio-economic impacts lazima ata-opt kujenga barabara kwavile anafahamu akija kupata 900 billion zingine; hatazitumia kumalizia reli ya kwenda Mwanza tena bali atazitumia kwa ajili ya kuboresha route nyingine!
...nchi za ulaya zisingekuwa na reli, kwa tafsiri hii. reli hazijengwi ili kufurahisha mtu/watu na kupata mtaji wa kisiasa, bali kuleta maendeleo mapana zaidi, kama, kupunguza gharama na muda wa usafirishaji bidhaa, kubeba mizigo mingi na mikubwa kwa pamoja, na hivyo kupunguza gharama za ujenzi na marekebisho ya barabara.
Kwa bahati mbaya sana tunapenda kujilinganisha na Kenya huku tukisahau kwamba wakati Tanzania tunahangaika na barabara kuu, wenzetu Wakenya barabara hizo tayari wanazo miaka na miaka! Kwa maoni yangu, Wakenya wamechelewa sana kujenga railway ya kisasa kwavile uchumi wao tayari ungewaruhusu kufanya hivyo more than 20 years ago.
...where do you get your facts from? hebu tueleze, ukitaka kusema Tz imeendelea unailinganisha na nani? US?
...thika super highway imejengwa miaka na miaka ipi? sasa, kama hufahamu, Moi alipotoka, aliacha barabara nyingi Kenya zikiwa choka mbaya.
...kwa trend hiyo ya "......more than 20 years", nasi tutakuwa lini tayari "uchumi wetu ukiruhusu?"
Hivyo basi, mtazamo wangu ni kwamba serikali ilifanya uamuzi wa busara kuanza kuangalia roads network kabla ya kuanza na reli...nazungumza hili kwavile siwezi kujitia upofu na kudhani kwamba kuna billions of dollars outta there lakini zinawasubiria akina Kikwete wakazibebe kwenye mabegi na waje kujengea reli! Njia nyepesi ya kufahamu haya mambo ni kuangalia personal planning/budgeting/financing. Watu tujiangalie wenyewe kuna mambo mangapi tunakusudia kuyafanya na tunafanikiwa mambo mangapi na kwanini tumefanya hili na sio lile! Ukiangalia critically utagundua kwamba mara zote ulikutana na multiple objectives wakati upo constrained na bajeti.
...usitumia neno "busara" vibaya.
...watu ni tofauti na serikali in many ways! usilinganishe.