Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Hii iliyopo licha ya upungufu wa injini na behewa hata kokoto (ballast) tu hakuna, sasa hivi hakuna tofauti na kusafiri na lori kwenye barabara ya vumbi. Inasikitisha mno.
 
JokaKuu,
Sina shaka kwamba tunapoteza mapato mengi sana, hilo halina ubishi. Kwamba hivi sasa serikali hawajui au wanafanya makusudi jibu ni kwamba wanafahamu na ndio maana wakati tunaingia kwenye mining economy, hapakuwa na taasisi inayohusika na ukaguzi ndipo baadae baada ya kugundua tunaibiwa ndipo wakaanzisha Mining Audit Agency. Aidha, kwavile serikali iligundua kwamba vidani ni moja ya njia zinazotumika kuiba ndipo ikapitishwa sheria ni gramu ngapi za vidani zinakuwa accepted kama ni for personal use na ikizidi, unahesabika kwamba ulitaka kutorosha madini! Na kwa kupitia njia hii, kuna vidani vya billions of TZS pale Airport vimekamatwa ambavyo zamani vingehesabika kwamba ni vidani for personal use.
Pamoja na yote hayo bado am very certain kwamba bado tunapoteza mapato mengi kwenye sekta ya madini. Nimekupa mifano ya hapo juu ili kujibu hoja yako kwamba je, serikali haifahamu au wanafanya makusudi! Lakini hata hivyo, bado mkuu wangu tatizo lako ni lile lile…..hujioni kabisa kwamba nawe(kama Mtanzania) ni sehemu ya tatizo la nchi hii! Wengi tunalalamika serikali serikali huku tukisahau wajibu wetu! Kama utakumbuka mimi na wewe tulishawahi kuwa kwenye mjadala mzito kuhusu ufaulu Tanzania….wengi wetu kama ilivyo ada, tukasahau wajibu wetu tukawa tunabaki kulalama kuhusu serikali. Kama unakumbuka, wakati tunahitimisha mjadala ule, uliniuliza nina maoni gani kuhusu nini kifanyike ili kuongeza ufaulu. Nikakujibu kwamba lazima kila mmoja atimize wajibu wake! Mwanafunzi lazima atimize wajibu wake wa kusoma kwa bidii. Mzazi lazima atimize wajibu wake wa kumsimamia mwanae na kuhakikisha ana-behave like a student. Mwalimu nae atimize wajibu wake badala ya kuendelea kusingizia maslahi madogo kama kigezo cha kutotimiza wajibu! Mwisho serikali nayo itimize wajibu wake! Aidha nika-conclude kwamba hata kama utakuwa na shule bora kuliko zote duniani zenye kila kitu lakini mwalimu, mzazi na mwanafunzi wakishindwa kutimiza wajibu wao; itakuwa ni kazi bure! Kwa bahati mzuri, ukiangalia matangazo ya HakiElimu hivi sasa yanasisitiza uwajibikaji wa wadau tofauti kabisa na zamani ambapo matangazo yao yalikuwa ni kama vile wanafunzi walikuwa perfect, walimu perfect, wazazi perfect lakini tatizo lilikuwa serikalini pake yake! HakiElimu kwa sasa nao wamegundua kwamba pamoja na matatizo yote ya serikali lakini bado kuna tatizo la wadau (wanafunzi, wazazi na walimu) kutowajibika! JokaKuu, sio kwamba nataka kujifagilia lakini nitasema na kama utaona najifagilia, kimpango wako. Kuna wakati mimi niliwahi kufanya kazi NMB na kwa bahati mbaya kabisa nilikuwa nalazimika kufanya kazi nyingi zaidi peke yangu. Ilipokuwa inafika mwisho wa mwezi, nilikuwa naingia ofisini saa kumi, nimechelewa sana saa kumi na moja alfajiri. Nilikuwa nalazimika kufanya hivyo kv nilikuwa nalazimika mishahara ya wafanyakazi inalipwa on time na vile vile nihakikishe naandaa na kuwakilisha monthly reports on time! Na wala si kwamba nilikuwa nafanya hayo kwa ajili ya posho; manake hadi natimuliwa NMB, hakuna kitu ambacho nilikuwa naona uvivu kufanya kama kuandikia Claim ya Sitting Allowance! Simple rule, hakuna atakayekuandikia Sitting Allowance wakati pesa ni zako mwenyewe!! Lakini pamoja na yote hay ohayo, huwezi amini, kuna wapumbavu pale ofisni walikuwa wanasema napenda sifa kwavile tu nilichokuwa nafanya ni wajibu wangu! Hili ndilo tatizo letu, hatupendi kuwajibika lakini ni wepesi sana wa kuilalamikia serikali! With due respect Sir, mkuu wangu JokaKuu nawe ni hodari sana wa kuilalamikia serikali! Je, huwa unatimiza wajibu wako? Na uki-maximize uwajibikaji, kuna wapumbavu watakuchukia na kukuona mpenda sifa!
NasDaz,

..bado tunaendelea kupoteza mapato hata baada ya kuunda mining audit agency.

..as a country we need to do more kuhakikisha tunapata mapato zaidi kutoka ktk sekta hiyo.

..kwa kifupi serikali inatakiwa iongeze vyanzo vya mapato, ipunguze upotevu wa mapato, na zaidi ipunguze matumizi.

..Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani, Dr.Ndalichako, alisema serikali ilifanya makosa kufungua shule za sekondari bila kuwa na waalimu na vitabu na maabara. Hilo ndilo tatizo la msingi kabisa la elimu nchini kwetu, hayo mengine unayozungumzia ni secondary tu.

NB:

..kuna tofauti kati ya kutekeleza wajibu wako ktk nafasi yako ya kazi, na kutekeleza wajibu wako kama raia wa kawaida.

..mimi natekeleza wajibu wangu kama raia kwa kuikosoa, kuishauiri, na kuihimiza serikali yetu na Chama tawala. tatizo ni kuwa wakati tunatekeleza wajibu wetu wanatokea wakina NasDaz wanatuchukia na kutuona walalamishi.
 
Last edited by a moderator:
Thnx! ndg yangu NasDaz kwa ufafanuzi Nimetolea mfano wawa2 weupe 7bu wao wameshauzoea mfumo huo kila uchaguzi wananchi wanapima km chama chenu kilivurunda mnakula za USO! hata hapo GHANA wanajua wakivurunda kipindi cha 1 watang'olewa! nikweli maBADILIKO yanaanza namimi Ila ninavyokusoma km umekata tamaa! kwamba hakuna kipya kitakachotokea hapana cc wanaNCH 2natakiwa 2lazimishe watawala wafanye 2navyotaka!
 
Thnx! ndg yangu NasDaz kwa ufafanuzi Nimetolea mfano wa wa2 weupe 7bu wao wameshauzoea mfumo huo naamini pia unawasaidia kila uchaguzi wananchi wanapima Utendaji hata hapo GHANA wanaotawala sasa wanajua wakivurunda kipindi cha 1 watang'olewa! maBADILIKO yanaanza na mtu 1 Ila ninavyokusoma km umekata tamaa! kwamba hata 2kibadili CHAMA hakuna kipya kitakachotokea hapana cc wanaNCH 2natakiwa 2lazimishe watawala wafanye 2navyotaka sio wanavyotaka! 7bu % Kubwa ya waAFRICA ni waLEVI wamadaraka so yapasa 2wamulike
 
NasDaz,

..bado tunaendelea kupoteza mapato hata baada ya kuunda mining audit agency.

..as a country we need to do more kuhakikisha tunapata mapato zaidi kutoka ktk sekta hiyo.

..kwa kifupi serikali inatakiwa iongeze vyanzo vya mapato, ipunguze upotevu wa mapato, na zaidi ipunguze matumizi.

..Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani, Dr.Ndalichako, alisema serikali ilifanya makosa kufungua shule za sekondari bila kuwa na waalimu na vitabu na maabara. Hilo ndilo tatizo la msingi kabisa la elimu nchini kwetu, hayo mengine unayozungumzia ni secondary tu.

NB:

..kuna tofauti kati ya kutekeleza wajibu wako ktk nafasi yako ya kazi, na kutekeleza wajibu wako kama raia wa kawaida.

..mimi natekeleza wajibu wangu kama raia kwa kuikosoa, kuishauiri, na kuihimiza serikali yetu na Chama tawala. tatizo ni kuwa wakati tunatekeleza wajibu wetu wanatokea wakina NasDaz wanatuchukia na kutuona walalamishi.
JokaKuu,
Kwamba serikali bado inapoteza mapato kwenye sekta ya madini hata baada ya kuunda mining audit agency, nakubali na ndio maana hata kwenye post yangu nilisema pamoja na yote hayo bado upotevu wa mapato kwenye sekta hiyo upo. On top of that, nilikupa mfano wa mining audit agency kv ulihoji ina maana serikali haijui kwamba kuna upotevu; nikakujibu wanafahamu ndio maana wakaunda audit agency na kuweka maximum weight for personal jewelry.

Tukija hoja ya Ndalichako, niseme tu kwamba Watanzania tumekumbwa na upofu....tunakumbuka tu failure ya 2012 kv ni mass failure na ilikuwa ni talk of town. Failure Tanzania haijaanza leo....! Mie nilimaliza form four st antony's sec 1996...more than 75% ya darasa letu tulienda form v....lilikuwa ni commited class na shule yenyewe ilikuwa committed in terms of administration; wanafunzi, wazazi na walimu walifahamu wajibu wao. Darasa letu kulikuwa na zero mbili tu! Majirani zetu, Jitegemee secondary school, shule mzima kulikuwa na Zero karibu 400!! Pale Jitegemee walikuwa na kila kitu, bonge la maktaba kuliko st anthony's, mahabara iliyoenda shule, walikuwa na walimu wa kutosha! Lakini Jitegemee hadi leo wanafunzi wanafeli vibaya mno! WHY? Wanafunzi wengi wa Jitegemee hawapo responsible! Sisi wenyewe enzi zile tulikuwa tunaenda pale na Tape zetu mifukoni kwenda kushindana ku-rap....upuuzi kama huo huwezi hata siku moja kuukuta pale st. anthony's. Now tell me, ikiwa shule kama Jitegemee iliyopo Dar es salaam ilipata Zero 400, what about shule za kule ndani ndani? Ukienda pale Al Haramain Kariakoo walikuwa na kila kitu; wanafunzi wengi Dar walikuwa wanaenda pale kwa ajili ya practical!! Al Haramain labda kama wameacha leo kufeli lakini na wenyewe walikuwa wanafeli vibaya mno!! Administration na wazazi wenye watoto pale Al haramain hawapo responsible! Na hivi ndivyo ilivyo kwa shule nyingi za Kiislamu!!! Tafuta matokeo ya NECTA for the past 15 years kisha uyaangalie kwa makini....ni failure failure failure ingawaje watu wanadhani kufeli kumeanza jana au juzi; ni tangu zamani tatizo watu hatufuatilii mambo!! Now tell me, Far back 1996 kulikuwa na shule za kata ambazo zilijengwa kabla ya walimu?! Hapa tatizo kubwa ni uwajibikaji! Kama sio uwajibikaji, kwanini basi zile shule za tangu zamani zisifaulishe?! Walimu wamefanikiwa kuwa-manipulate Watanzania kiasi kwamba kila mmoja hivi sasa anaamini Mwalimu ndie mfanyakazi wa serikali aliye dhalili na anayelipwa mshahara mdogo zaidi kwahiyo wana haki ya kutotimiza wajibu wao huku wengine wakilalamika kwamba hawathaminiwi!! Nani akuthamini wakati shule yako kila mwaka inatoa zero darasa zima huku wakati wa kazi unaenda kwenye shughuli zako!!!!

Hivyo basi, hoja ya Ndalichako kwamba serikali ilifanya kosa kujenga shule nyingi kabla ya walimu ni sahihi kwa maana moja kubwa; ilichangia kuongeza mass failure lakini sio msingi wa tatizo....msingi wa tatizo ni wadau kutokuwa RESPONSIBLE!!

Now turudi kwenye hoja yenyewe ya Ndalichako! You have limited budget, you either start building schools or start training teachers! Acording to Ndalichako and many others, unaanza ku-train teachers! Then ushakuwa na (say) 10,000 teachers at disposal; then what next? Unawamwaga mtaani wakati mnasubiria shule kujengwa or what? Or hata shule ambayo requirement ni walimu 20, unapeleka walimu 40 ili mradi kila mmoja awe na ajira ili wasiwa-disappoint wengine wanaotaka kuingia Ualimu kwa kuona pamoja na kwamba vyuo vinadahili walimu wengi lakini wote wanaishia mtaani? Sio siri, Ualimu ni taaluma isiyopendwa na wengi lakini cku hizi wengi wanaenda Ualimu kwa sababu wanafahamu kuna uhakika wa ajira.....so, ni situation gani ingekuwa created kwa kusomesha walimu wengi halafu hawana kazi kwa sababu wanasubiri shule zijengwe? By the way, anakaa mtaani halafu miaka minne baadae ndo anaenda kwenye shule; huyo atakuwa mwalimu tena au mhitimu wa chuo kikuu mwenye cheti cha ualimu?!
 
Last edited by a moderator:
Kikwete unafanya kazi na kazi inaonekana Mungu akubariki. Ndugu Salary Slip ahadi zinatekeleka. Hapo kibaha maeneo ya viziwaziwa Rais alikuwa ameahidi maji na kweli tenda ilitangazwa mwezi julai mwaka huu na tayari mkandarasi keshaanza kupima. Naamini hata kwa maeneo mengine kazi zinafanyika. chama je huko gongo la mboto hali ikoje. Ritz atatujuza ya town senta.
 
Kila sehemu mambo yanaenda spidi huku simiyu tenda zinatangazwa kibao ujenzi na uthamii kila kona unaendelea hakika jk anafanya kazi kweli kathubutu kaweza na sasa anazidi kusonga mbele.
 
Thnx! ndg yangu NasDaz kwa ufafanuzi Nimetolea mfano wa wa2 weupe 7bu wao wameshauzoea mfumo huo naamini pia unawasaidia kila uchaguzi wananchi wanapima Utendaji hata hapo GHANA wanaotawala sasa wanajua wakivurunda kipindi cha 1 watang'olewa! maBADILIKO yanaanza na mtu 1 Ila ninavyokusoma km umekata tamaa! kwamba hata 2kibadili CHAMA hakuna kipya kitakachotokea hapana cc wanaNCH 2natakiwa 2lazimishe watawala wafanye 2navyotaka sio wanavyotaka! 7bu % Kubwa ya waAFRICA ni waLEVI wamadaraka so yapasa 2wamulike
Kukata tamaa? Come on men, sina huo msamiati akilini mwangu....nafanyaga kuusikia tu kutoka kwa watu!! Ninachosema na ambacho nitaendelea kusisitiza ni Watanzania kuwajibika; wengi wetu hatupo responsible na tunaamini uwepo wa serikali ndo basi tumekasimu kila kitu....mambo yakienda hovyo, tunalalamika kwamba serikali hii wakati wenyewe hatutekelezi wajibu wetu!! GOvernment performance is all about collective individual responsibility, accountability and commitment to what everyone does! Hii collective individual responsibility, accountability and commitment ndiyo inazalisha aggregate government/country performance. Dunia hii hakuna sehemu ambako hakuna rushwa lakini kwanini wengine wanaendelea ingawaje kuna rushwa na ufisadi? Asian countries ni very corrupt, tena kule ni hizi grand corruption as compared na zilizojaa huku za polisi, mahakamani na hospitalini lakini bado wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo compared to African countries; WHY? The answe is simple, jamaa wapo responsible and commited!! Wanachukua chao mapema na bado wanapiga mzigo!!!

Kwahiyo tunarudi palepale, hata kama tutabadilisha viongozi maradufu, ikiwa jamii haibadiliki bado itakuwa ni kazi bure kv hao viongozi bado wanatoka kwenye jamii ile ile ya hovyo hovyo....jamii ya wezi na wala rushwa lakini isiyotaka kuwajibika na kuwa commited to what they're supposed to do.
 
Mkuu August,
Nimetaja mambo mengi ikiwa ni pamoja na hayo uliyoyataja hata kama nitakuwa nimeyataja in other way round. Tatizo letu ni kwamba tunasahau kwamba na sisi Watanzania ni sehemu ya Tanzania!! Hao viongozi unaowataja hawatoki mbinguni bali wanatoka miongoni mwetu....huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! Anakuwa sawa na wale wale kwa sababu nae ni sehemu ya tatizo lakini hajajigundua kwamba nae ni tatizo kubwa nchi hii! Hili halipo Tanzania tu bali karibu nchi zote za Afrika, utafikiri tumepigwa laana! Waafrika wote ni sehemu ya matatizo ya Afrika! Hata kule ambako wameshafanya mabadiliko mara kadhaa bado kuna matatizo kibao coz' wale wapya wanaopata nafasi ya kuongoza nao walikuwa ni sehemu ya tatizo!!

Mkuu Nas, kauli uliyo weka hapa ni ya kukataa tamaa kwamba hakuna mtu anayeweze ku mzuri au mtendaji mzuri, ndio maana umeweka mfano kwamba hata mimi nikipata hayo madaraka nitafanya hivyo, lakini ningependa kukuhakikishia licha ya binadamu wote kuwa na mapungufu yetu, lakini kwangu mimi, siwezi kuchukua rushwa hata ya 1m usd, or even 1m tshs, nitengeneza hasara kwa nchi kwa kutengeneza barabara mbovu, au kuuwa uchumi , au kwa kuleta dawa mbovu, ambayo ndio hulka ya viongozi wengi wa Tz, sijui Kenya, na hata Mwl alivyo kuwa south South commission aliwahi kuliongelea hilo kuwa ni weeakness kwa nchi nyingi za afrika, lakini niaminie kwamba kweangu mimi the Big picure ndio desire yangu na kujenga mahekalu nk kwa kuuwa uchumi ni uzumbukuku mkubwa ambao sote tuna takiwa tuupige vita. Commission siwezi kukata kupokea lakini sio Rushwa ambayo siwezi ku i declare,
 
Salary Slip,

..wakati Raisi Kikwete anatangaza "nia" ya kujenga reli, Raisi Uhuru Kenyatta atakuwa na ground breaking ceremony ya ujenzi wa reli toka Mombasa kuelekea Uganda na Rwanda kesho.

cc Koba, Ritz, Mchambuzi, Kubwajinga

Ilani ya ccm ilisema hivyo, Tulitarajia utekelezaji na sio blah blah tena. CCM inakuwa kama baraza la bibi vizee, wanasema lakini utekelezaji ni hafifu mno.
 
Hivyo basi, hoja ya Ndalichako kwamba serikali ilifanya kosa kujenga shule nyingi kabla ya walimu ni sahihi kwa maana moja kubwa; ilichangia kuongeza mass failure lakini sio msingi wa tatizo....msingi wa tatizo ni wadau kutokuwa RESPONSIBLE!!
...hapa nakubaliana nawe. na mdau mkubwa kwenye hili unamjua!

Now turudi kwenye hoja yenyewe ya Ndalichako! You have limited budget, you either start building schools or start training teachers! Acording to Ndalichako and many others, unaanza ku-train teachers! Then ushakuwa na (say) 10,000 teachers at disposal; then what next? Unawamwaga mtaani wakati mnasubiria shule kujengwa or what? Or hata shule ambayo requirement ni walimu 20, unapeleka walimu 40 ili mradi kila mmoja awe na ajira ili wasiwa-disappoint wengine wanaotaka kuingia Ualimu kwa kuona pamoja na kwamba vyuo vinadahili walimu wengi lakini wote wanaishia mtaani? Sio siri, Ualimu ni taaluma isiyopendwa na wengi lakini cku hizi wengi wanaenda Ualimu kwa sababu wanafahamu kuna uhakika wa ajira.....so, ni situation gani ingekuwa created kwa kusomesha walimu wengi halafu hawana kazi kwa sababu wanasubiri shule zijengwe? By the way, anakaa mtaani halafu miaka minne baadae ndo anaenda kwenye shule; huyo atakuwa mwalimu tena au mhitimu wa chuo kikuu mwenye cheti cha ualimu?!
...si kweli kwamba tuna limited budget, as far as tunataka kuboresha elimu nchini. tukipunguza upotevu wa fedha za serikali, refer report za CAG, itakuwa ni moja ya njia. pili, hata kwenye sekta yenyewe, kuna upotevu wa fedha za maendeleo. hakielimu wametafiti na kutoa repoti juu ya hili.

...taaluma hii haipendwi kwa kuwa tumeitelekeza. na majibu tunayaona kwenye kufeli wanafunzi, ubora hafifu wa mazao ya elimu, inayopelekea kuwa na upungufu wa skilled workers ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

...NazDaz, nadhani kimkakati, issue si kusomesha walimu, bali kuboresha mazingira ya sekta hii ili kuvutia watu wenye uwezo mzuri kuwa walimu au kusomea ualimu. in short, incentives.

...hakuna nchi duniani utaenda wakakwambia wana unlimited budget for education. its all about strategic management of these resources chache tulizonazo.
 
Government performance is all about collective individual responsibility, accountability and commitment to what everyone does! Hii collective individual responsibility, accountability and commitment ndiyo inazalisha aggregate government/country performance. Dunia hii hakuna sehemu ambako hakuna rushwa lakini kwanini wengine wanaendelea ingawaje kuna rushwa na ufisadi? Asian countries ni very corrupt, tena kule ni hizi grand corruption as compared na zilizojaa huku za polisi, mahakamani na hospitalini lakini bado wanapiga hatua kubwa za kimaendeleo compared to African countries; WHY? The answe is simple, jamaa wapo responsible and commited!! Wanachukua chao mapema na bado wanapiga mzigo!
...nadhani jibu la unlimited budget liko kwenye hii bolded point ya pili. hiyo ya kwanza ni tafakari ya muhimu sana, ambayo, luckly ni subject ya vitabu kadhaa siku hizi.
 
Niliamua kuwa member wa JF kwaajili ya Mijadala km hii yakuongezeana UFAHAM. ndg NasDaz,nikweli ili 2we na Taifa linalojitambua nilazima kila m2 awe7bu ya mabadiliko anayoyatamani lkn kwa Njia unayoipendekeza huoni km itachukua KARNE nyingi kufikia huko? ukichukulia kwa ss hakuna tena UZALENDO PESA MBELE kwanini 2sianzie angalau hii njia ya mkato yakuwatoa watawala kila wanapovurunda! Badala yakusema wt ni wale wale mfano CCM wanaoena AIBU cdhani chama kingine kitakuwa na Dhambi hiyo kwann 2sianzie hapo!!
 
NasDaz,

..waalimu mashuleni, hutaki.

..kubadilisha uongozi, hutaki.

..kila kitu wewe hutaki.

..maandiko yako yanaonyesha kwamba u dont want to try anything different frm what we r currently implementing.

..ndiyo maana wachangiaji wengine tunaona UMEKATA TAMAA.
 
Last edited by a moderator:
...si kweli kwamba tuna limited budget, as far as tunataka kuboresha elimu nchini. tukipunguza upotevu wa fedha za serikali, refer report za CAG, itakuwa ni moja ya njia. pili, hata kwenye sekta yenyewe, kuna upotevu wa fedha za maendeleo. hakielimu wametafiti na kutoa repoti juu ya hili.

...taaluma hii haipendwi kwa kuwa tumeitelekeza. na majibu tunayaona kwenye kufeli wanafunzi, ubora hafifu wa mazao ya elimu, inayopelekea kuwa na upungufu wa skilled workers ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

...NazDaz, nadhani kimkakati, issue si kusomesha walimu, bali kuboresha mazingira ya sekta hii ili kuvutia watu wenye uwezo mzuri kuwa walimu au kusomea ualimu. in short, incentives.

...hakuna nchi duniani utaenda wakakwambia wana unlimited budget for education. its all about strategic management of these resources chache tulizonazo.
Good, now let's do it this way....
Kwanza nitangulie kusema wazi kwamba am very confident we've very limited resources as compared to multiple objectives ambazo kwa kiasi kikubwa ziko down....but you believe otherwise! I hope hauleti politics kwenye serious issues. If so, then nisaidie yafuatayo.
A. What're our total revenues...(ambayo yanaingia kwenye vitabu)
B. Ni mapato kiasi gani yanapotea kwa njia mbalimbali kv wizi, corruption, ukwepaji kodi?
A+B=Mapato ambayo tulitakiwa kuwa nayo
C. nitajie bajeti ya vitu ambavyo ni vipaumbele na niambie vingetekelezeka kwa asilimia ngapi basing on Actual Revenues(A+B)
D. Kama hivyo vipaumbele visingeweza kuwa fully handled, tell me ni muda gani ungehitajika kukamilisha vipaumbele vyote basing on Actual Revenue (A+B)

NB: UKishindwa kujibu hayo maswali nitafahamu unaleta siasa kwenye serious issues.
 
NasDaz,

..waalimu mashuleni, hutaki.

..kubadilisha uongozi, hutaki.

..kila kitu wewe hutaki.

..maandiko yako yanaonyesha kwamba u dont want to try anything different frm what we r currently implementing.

..ndiyo maana wachangiaji wengine tunaona UMEKATA TAMAA.
Khaaa! Wee JokaKuu....mbona unaongea kama mwanasiasa wa kwenye majukwaa ambao kazi yao ni propaganda? Nani kasema mwalimu hataki? Nimesema walimu sitaki au nimesema nini kinatakiwa kuanza whn u've limited resources while facing multiple objectives?! Unaleta vituko vingine; kwamba sitaki uongozi ubadilike; mie ya kubadilika au kutobadilika yananihusu nini?! Mkuu wangu JokaKuu, am telling you from deep inside my heart; and am saying this in front of God and am very certain tht He(God) knows my conscious is clear. Ninachotaka kusema ni kwamba; I don't care who's in power....whether CCM or CHADEMA, I don't care! Kwangu mimi CCM na CHADEMA wote ni wale wale tu!! CCM mwizi na fisadi wa leo wakati CHADEMA some1 else ni mwizi na fisadi wa kesho!! Kama ni kuangalia political issues am more interested na combination ya bunge na wala sio nani yupo Ikulu! Am always praying isije kutokea tukawa na bunge ambalo limehodhiwa na chama kimoja kama ilivyo sasa....I believe, kukiwa na combination mzuri basi huko kutatokea watu wenye uchungu wa kweli na nchi hii; watu wanaotaka kuwajibika....kwa sababu tofauti yangu mimi na nyinyi ni moja na ndio maana hatufikii muafaka! Nyinyi mnaamini kwamba tatizo ni CCM na serikali yake kwahiyo mnajidanganya kwamba CCM wakiondoka nchi itabadilika kuwa ni nchi ya maziwa na asali....!! BInafsi mimi siamini katika hilo unless unitajie nchi moja ya mfano barani Afrika ambayo baada ya kubadilisha uongozi, nchi ikabadilika na kuwa inayotiririsha maziwa na asali!! BInafsi, naamini matatizo ya Waafrika yanafanana kutoka nchi moja hadi nyingine! Waafrika wengi ni watu wa hovyo hovyo, hatupo committed na responsible! wengi ni wezi na wala rushwa! Kwahiyo kitu cha kwanza muhimu kuliko vyote ni kubadilika..tukibadilika; jamii ina maana jamii mzima itabadilika na kuwa na responsible societies, committed societies, non-corrupt societies! Ukishakuwa na jamii kama hiyo basi hata viongozi watakaotoka kwenye jamii husika ni responsible nd committed leaders, non corrupt leaders...kinyume chake ni kama unamtoa fisadi nyangumi madarakani na kisha unamwingiza fisadi papa coz' hata wale unaowaingiza watakuwa wanatoka kwenye jamii ile ile ya hovyo hovyo....yaani jamii ya hovyo hovyo unaitarajia kutoa viongozi wenye maadili...gimme a break!!

JokaKuu na wenzako mnanishangaza kitu kimoja! Kila ninapokazinia suala la uwajibikaji nyie mnakimbilia kusema NIMEKATA TAMAA!! Mbona kana kwamba mnapinga suala la uwajibikaji?

Mwisho unamalizia kwamba inaelekea i don't wanna try anything! Hapo umeleta siasa; ulichotaka kusema ni kwamba I don't wanna try other parties....! Jibu nimeshakupa hapo juu....I DON'T CARE WHETHER CHADEMA, CUF, NCCR OR CCM coz' am not blinded by these politicians! I'll be the last person to be manipulated by these guys! Uchaguzi ukifika, nitaenda kumpigia yule(mtu, sio chama) ambae naamini ana something tangible lakini kama sioni yeyote; i can't waste my time in those voters queues just to vote for a party....kwamba, (say) hata kama Kitila Mkumbo naona hana sifa lakini nimpigie tu coz' anawakilisha chama X, tht will NEVER HAPPEN AND EVER!
 
Last edited by a moderator:
Niliamua kuwa member wa JF kwaajili ya Mijadala km hii yakuongezeana UFAHAM. ndg NasDaz,nikweli ili 2we na Taifa linalojitambua nilazima kila m2 awe7bu ya mabadiliko anayoyatamani lkn kwa Njia unayoipendekeza huoni km itachukua KARNE nyingi kufikia huko? ukichukulia kwa ss hakuna tena UZALENDO PESA MBELE kwanini 2sianzie angalau hii njia ya mkato yakuwatoa watawala kila wanapovurunda! Badala yakusema wt ni wale wale mfano CCM wanaoena AIBU cdhani chama kingine kitakuwa na Dhambi hiyo kwann 2sianzie hapo!!
Nafahamu kwamba it can take the time!! Ngoja nikuambie kitu kimoja! For those who believe in God, Mungu alimshushia Nabii Mussa Torati! God was very smart, aliishusha Torat kwa sababu za msingi....alifahamu wakati ule Wayahudi walikuwa mafedhuli kweli kweli; akafahamu kwamba hawa ukiwapekekea sheria laini laini hawa; hawatabadilika! Akawaletea TOrat,ambayo in fact, ni full dictatorship constitution! Akaja Yesu, Mungu akadhani wanadamu wameshabadilika, akashusha katiba laini laini ambayo tunaiita INJILI! Katiba ambayo inahubiri kwamba mwenzako akikupiga kofi shavu la mkono wa kushoto, mgeuzie na la kulia akupige! Baadae Mungu akashituka tena, akagundua wanadamu bado ni waovu; na ktk sisi tunaoamini in Islam, akaja Muhammad na Katiba kama ile ile ya Mussa...!! Now tell me; yale zile adhabu zilizo kwenye Torati au Quran ingekuwa ndo zinatekelezwa hapa hapa duniani, ni wangapi wangeiba wakati wanafahamu ukidakwa; watu wanakula mkono wako! Wangapi wangekuwa wazinzi wakati wanajua wakidakwa; you get stoned to death?

You know what I mean kukupa hiyo mifano? I know, jamii ni ngumu kubadilika yenyewe lakini mfumo unaweza kubadilisha jamii!! Kama umenisoma kwenye post zangu zingine, nimesema Good Governance ni mfumo usiofaa kwenye jamii ovu; Good Governance ni kama Injili ya Yesu! Good Governance inafaa kwenye jamii iliyostaharabika, jamii isiyo ya wezi na wala rushwa kinyume chake Good Governance ni kichaka cha uovu!! Sina haja ya kurudia tena hoja hii maana yake nimeilezea kwa kirefu hapo kabla na ndio maana nikashauri kwamba Jamii Ovu inapaswa kuwa na mfumo utakaosaidia kui-shape jamii husika!! Nikapendekeza kwamba instead of Good Governance tuwe na Approved Dictatorship Governance or ADG!! Ninaposema ADG si kwamba kiongozi anaamka asubuhi anatangaza "watu wangu wameniambia fulani na fulani wamekula rushwa hivyo wawekwe ndani!" NO! ADG inatengeneza very STRICT LAW; kwamba assume NasDaz ameonekana ana utajiri mkubwa usiofanana na kipato chake halali; sasa badala ya kutaka upande wa mashitaka uthibitishe kwamba NasDaz amepata utajiri kwa Rushwa; inakuwa ni kazi ya NasDaz kuthibitisha kwambautajiri wake ni halali!! Kama ana jengo la sh. 500millio basi atupe huo mchanguno wa sh.500millionalivyozipatapata!! Atupe mchanganuo ndani ya siku chache kabisa coz' kama pesa zake ni halali basi ana kila kitu kwenye makabati yake...atuletee atuthibitishie otherwise, formular ni kwamba wizi wa milion 1, mwaka mmoja jela; 500 million; 500 years jela akafie huko huko bila kusahau kwamba tunarudisha mali zetu alizoiba!! Nasema ni Approved kv hizi zitakuwa ni sheria ambazo ni zipo kwa mujibu wa katiba na kupitishwa na bunge! Huo ni mfano tu!!

So, tukiamua inawezekana kabisa jamii kuibadilisha coz' hawatabadilika kwa kutaka bali mfumo unawalazimisha kufanya hivyo!
 
Mkuu Nas, kauli uliyo weka hapa ni ya kukataa tamaa kwamba hakuna mtu anayeweze ku mzuri au mtendaji mzuri, ndio maana umeweka mfano kwamba hata mimi nikipata hayo madaraka nitafanya hivyo, lakini ningependa kukuhakikishia licha ya binadamu wote kuwa na mapungufu yetu, lakini kwangu mimi, siwezi kuchukua rushwa hata ya 1m usd, or even 1m tshs, nitengeneza hasara kwa nchi kwa kutengeneza barabara mbovu, au kuuwa uchumi , au kwa kuleta dawa mbovu, ambayo ndio hulka ya viongozi wengi wa Tz, sijui Kenya, na hata Mwl alivyo kuwa south South commission aliwahi kuliongelea hilo kuwa ni weeakness kwa nchi nyingi za afrika, lakini niaminie kwamba kweangu mimi the Big picure ndio desire yangu na kujenga mahekalu nk kwa kuuwa uchumi ni uzumbukuku mkubwa ambao sote tuna takiwa tuupige vita. Commission siwezi kukata kupokea lakini sio Rushwa ambayo siwezi ku i declare,
Unajuwa wakati naisoma post yako, nikajiuliza "mbona mkuu August ame-personalize sana hoja yake?" Ikabidi nirejee nione nimeandika nini, nikakuta nimeandika "..huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! " Anyway, it's just an example, don't take it personal!!

Tukija hoja ya Kukata Tamaa naona wengi wanairudia rudia hadi najiuliza kwanini watu wanaona kama suala la kubadilika ambalo mimi nasisitiza watu hawalitaki!!!!! Ina maana hatuwezi kubadilika no matter what? Ina maana hatuwezi kuwa responsible society no matter what? Sasa huko si ndo kukata tamaa kwenyewe mkuu wangu???!! Let me put it this way, SIJAKATA TAMAA, but I don't trust many of African Politicians!!!! Most of these guys wanatoka kwenye jamii ambayo tayari ni ya hovyo.....jamii ambayo ukifanya kazi mwaka mmoja halafu ukajenga ghorofa, watu wanakusifia na kukuona una miakili ile mbaya! Wanakusifia ingawaje wanajuwa kwamba pesa zenyewe ni za magumashi!!! Hawa wanasiasa wetu wanatoka kwenye hizi jamii!! So, how do you expect the polluted society to give the good leader? Ndiyo unaweza kukutana na honest guys/leaders lakini wengi wanakuwa majanga!! Lakini jamii ikibadilika, ama kwa kutaka au kwa kulazimishwa na mfumo; basi tutapata good leaders coz' hawa watakuwa wanatoka kwenye good society!

Halafu kuna hoja yako juu kabisa ambayo umesema "kauli uliyo weka hapa ni ya kukataa tamaa kwamba hakuna mtu anayeweze ku mzuri au mtendaji mzur..." Hapo naomba niongee kwa kifupi sana! Hapa sio suala la kuwa na mtu mzuri na mtendaji mzuri but it's all about having GOOD SOCIETY ambayo ipo very commited, responsible and non corrupt society....SIO MTU!! YES, tunaweza kupata mtu mzuri na mwenye maadili kama MALAIKA, then What? Assume anakuwa ndo President, after 10 years, anaachia ngazi...then? Tunarudi business as usual!!! Au anakuwa mchapakazi na mkali kama Hayati Mwalimu Nyerere...after 10 years, anaondoka ofisini; then what? Business as usual kama ilivyokuwa baada ya kuondoka Nyerere!!! It's far better to have a bad leader in a good society than to have a good leader in a bad society! This bad leader can be held accountable by his good society but one good leader can't hold accountable the whole bad society.
 
Last edited by a moderator:
...nadhani jibu la unlimited budget liko kwenye hii bolded point ya pili. hiyo ya kwanza ni tafakari ya muhimu sana, ambayo, luckly ni subject ya vitabu kadhaa siku hizi.
But sisi hatupo Responsible, from Top to Bottom....lakini yote kwa yote; niseme tu kwamba thx kwa kufanya quotation zisizoumiza kichwa kujibu manake kuna moja ya kwako ilibidi niipotezee....ilikuwa kila nikiingaliaaaaa; mnh! hamu inaisha hapo hapo ya kujibu....lol!
 
Unajuwa wakati naisoma post yako, nikajiuliza "mbona mkuu August ame-personalize sana hoja yake?" Ikabidi nirejee nione nimeandika nini, nikakuta nimeandika "..huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! " Anyway, it's just an example, don't take it personal!!

Tukija hoja ya Kukata Tamaa naona wengi wanairudia rudia hadi najiuliza kwanini watu wanaona kama suala la kubadilika ambalo mimi nasisitiza watu hawalitaki!!!!! Ina maana hatuwezi kubadilika no matter what? Ina maana hatuwezi kuwa responsible society no matter what? Sasa huko si ndo kukata tamaa kwenyewe mkuu wangu???!! Let me put it this way, SIJAKATA TAMAA, but I don't trust many of African Politicians!!!! Most of these guys wanatoka kwenye jamii ambayo tayari ni ya hovyo.....jamii ambayo ukifanya kazi mwaka mmoja halafu ukajenga ghorofa, watu wanakusifia na kukuona una miakili ile mbaya! Wanakusifia ingawaje wanajuwa kwamba pesa zenyewe ni za magumashi!!! Hawa wanasiasa wetu wanatoka kwenye hizi jamii!! So, how do you expect the polluted society to give the good leader? Ndiyo unaweza kukutana na honest guys/leaders lakini wengi wanakuwa majanga!! Lakini jamii ikibadilika, ama kwa kutaka au kwa kulazimishwa na mfumo; basi tutapata good leaders coz' hawa watakuwa wanatoka kwenye good society!

Halafu kuna hoja yako juu kabisa ambayo umesema "kauli uliyo weka hapa ni ya kukataa tamaa kwamba hakuna mtu anayeweze ku mzuri au mtendaji mzur..." Hapo naomba niongee kwa kifupi sana! Hapa sio suala la kuwa na mtu mzuri na mtendaji mzuri but it's all about having GOOD SOCIETY ambayo ipo very commited, responsible and non corrupt society....SIO MTU!! YES, tunaweza kupata mtu mzuri na mwenye maadili kama MALAIKA, then What? Assume anakuwa ndo President, after 10 years, anaachia ngazi...then? Tunarudi business as usual!!! Au anakuwa mchapakazi na mkali kama Hayati Mwalimu Nyerere...after 10 years, anaondoka ofisini; then what? Business as usual kama ilivyokuwa baada ya kuondoka Nyerere!!! It's far better to have a bad leader in a good society than to have a good leader in a bad society! This bad leader can be held accountable by his good society but one good leader can't hold accountable the whole bad society.
Ndugu yangu Nas huo mfano ulioweka hauniti hofu wa personalisation , hofu yangu ni pale mtu unapokosa kuangalia unapotoka na unaelekea wapi yaani kuwa na plan ya the way fwd.
pili unatakiwa ujue maisha ya mtu ni full of contradiction, from individual level, ukaja ya mke na mume, ukaongezea ukipata watoto, then ukawa na wazazi wa pande mbili, mashangazi etc, mpaka kimtaa mpaka kuwa na nchi, na kote huko tunapita katika kijitafutia maendeleo, ndio maana wewe umefikia hapo ulipo na unaendelea kuchanja mbuga.
sasa ya tanzania yapo kuanzia mjini mpaka vijijini, ya viongozi na wana jamii, ya nini kilianza kuku au mayai.
sasa in a nut shell tatizo kubwa la tanzania ni la viongozi, wasio taka kuimplement policy endelevu na institution zilizo stable ndio maana tunakuwa na tume nyingi ambazo mapendekezo yake hayafanyiwi kazi, takukuru yenye kubadilishwa jina kila kukisha, na kusema hapo mwanzo sheria ilikuwa haijitoshelezi etc, na mwishoe viongozi kuwaingiza watendaji katika coalition of the willing.
kwa hiyo la kwanza kabisa likiwezekana miongoni mwetu ni kumpata kiongozi mzuri.
ikishindikana hilo, basi ni kuwabadili jamii ili wawe wanaona kutetea ujinga/kiongozi mbaya athari wana zipata wenyewe, iwe kwa kukosa elimu bora , umeme, usafiri matibabu na makazi bora na lishe. sisi jamii tukijiweka sawa kwenye makazi bora na chakula basi tutakuwa na nguvu na nafasi ya kuona au kutatua matatizo mengine iwe ya kiongozi, elimu, umeme, usafiri, nini cha kuanza nk nk.
 
Back
Top Bottom