Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)


Unaweza kuta hata baba yako alizungumza na Bakhresa waanzishe makampuni. Bakhresa akaanzisha wewe na baba yako mnapita mitaani kusema viwanda vya Bakhressa mlimshauri na kumpa ramani. Sijui kama umenielewa.
 
Kuongea mipango na kutenda (utekelezaji) vitu viwili tofauti wengi huwa wanaongea sana ila ikija kwenye utekelezaji kimbembe na sio wote wamejaaliwa kipawa cha kutekeleza kitu/vitu kutoka kwenye mipango mpaka kikaonekana (execution) wachache wenye hicho kipawa. Hasa hawa wanasiasa wa dunia ya tatu ni hatari kabisa wakuogopa kama ukoma maneno mengi vitendo haba yaani bora aonekane na yeye yumo tu na kauli zao mara sijui upembuzi yakinifu sijui mchakato maneno mengi yasiyo na tija kwenye miradi.​
 
Kikwete bado ana mchango pande zote, mazuri na mabaya,kwangu namwona ni kiongozi bora tofauti na yule mfalme juha
 
Safi sana. Umewafundisha kwani wanafikiri mipango ya serikali ni kama kwenda kununua nyanya sokoni. Ni shida kubwa sana ya wengine hawajui au hawafuatilii mipango ya serikali kutoka katika wizara husika Bali wamebaki kusikiliza maneno ya. Wanasiasa. Jiongezeni Kwa kujisomea wenyewe
 
Hujui lolote kuhusu nchi inavyoendeshwa. Nenda darasani Ili usiwe mtaji wa wanasiasa
 
chama cha mapinduzi kina dira juu ya hili taifa kwa kipindi kirefu mnoo hivyo usishangae ndugu
 
Mchakato mchakato mchakoto....miaka 20
 
Walipanga mipango ya miradi ya maendeleo kwa muda wa miaka 30 yaani kuanzia 1995 hadi 2025 na kila anayeingia madarakani atimize sehemu yake ila zigo kubwa alibebeshwa mwendazake. Reli ya SGR walitaka kuingia mkataba wa mkopo na Bank ya Exim lakin kwa sharti kwanza tenda ya ujenzi wapewe Wachina wenyewe,hapo JK akaamua ku-mute na zigo akamtupia mwendazake na yeye akawapa tenda Waturuki kutokana na gharama za ujenzi zilikuwa nafuu kuliko Mchina. Lakini Wachina hawakukubali,wamepigana sana hadi wamepewa vipande vingine wajenge.Reli ya Mwanza-Shinyanga-Kahama-Bandari Kavu ya Isaka wanajenga Wachina na Mwendazake aliwaambia "mtusamehe deni la TAZARA", kumbe deni la TAZARA hadi leo tunadaiwa.
 
Hakuna raia wa kawaida anajali au kujihangaisha na mipango na michakato, raia wanachotaka kuona ni utekelezaji na matokeo tu. Wanataka kuona vitu halisi sip story, maneno na ahadi.
 
Niweke hapa hiyo Ilani aliyoandika kikwete ikaja fanywa na Magufuli. Kikwete anajitutumua tu.
Ndugu yangu huo ndio ukweli, angalia Airport mpya, Makao makuu ya Dodoma, SGR, Bwawa la Nyerere na miradi mingi tu ni michakato ya muda mrefu huwezi mwezi tu ukasema tunaanza mradi mkubwa kama SGR kesho ni mambo yanapitia process ndefu kuandaa mradi. Hata Kikwete yeye alirithi mambo aliyoanza Mkapa. ILa JPM alikuwa na uthubutu na vilikuwa vipaumbele vyake. Kila Rais anakuja ndio ilani ipo labda ya miaka 5 na akafanya yale anayodhani muhumi kwake na mengine akaacha yaendelee akaja mwingine akaona hili muhimu kwake kuliko lile, ila ni Ilani ya chama tawala.
 
Unasahau Kikwete katika utawala wake barabara nyingi sana za lami alijenga awamu yake, Kitengo cha kusafisha figo ni Kikwete, kitengo cha moyo pale muhimbili ni Kikwete hivi vilikuwa vipaumbele vyake na vimeokoa maisha ya watu wengi sana pale. Kila awamu wamefanya sehemu ya hichi tunakiona leo, huwezi ukafanya yote wakati mmoja SGR, Lami nchi nzima, Bwawa la Nyerere sijui mji mpya wa serikali sijui ndege sasa pesa utazitoa wapi? ndio maana kila awamu imefanya na mengine yakaja kumaliziwa awamu nyingine na huko mbele watakuja kufanya yalionzishwa sasa kama LNG plant.... ndio maana ya kupokezana vijiti.
 
Anaona mmejitoa ufahamu maana sasa hivi sio "ILANI YA CHAMA" wala sio "JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" maana document za serikali zimejaa jina la Samia kuliko serikali ya jamhuri ya Muugano, mama ametoa fedha, tumetekeleza maoni ya mama etc ikumbukwe shughuli za serikali ni mambo mtambuka na ukiona project imeanza Leo ujue process imeanza zaidi ya miaka 5 nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…