Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Kuna vichwa vya treni vilikutwa bandarini vimeandikwa TRC lakini mwenyewe alitafutwa hakujitokeza mpaka sasa ndio hiyo SGR
 
huyu mzee anatakiwa ayajue haya maandiko:

“Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

— Mithali 17:28 (Biblia Takatifu)
 

..kuna Jiwe la msingi la SGR liliwekwa na Waziri wa Miundombinu Samuel Sitta na wakandarasi wa mradi walitoka China.

..Sasa nini kilitokea toka wakati huo mpaka wakaja wakandarasi wa Kituruki na Kireno, na baadae tukabakia na wakandarasi wa Kituruki mpaka sasa hivi?
 
Simple hakukuwa na hela ya kujenga mradi.

Mpaka mkandarasi anaingia site kuna processes. Kuona tu mkandarasi wakati hakuna kilichofanyika ni sinema tu.

Ideas za SGR zinaweza kuwa zimetoka mbali, lakini mradi umeanza kutekelezwa na Magufuli na Samia anauendeleza; hao ndio watu wakuchukua credit ya mradi.
 

Hata mimi sijui ana matatizo gani; nadhani sehemu kubwa ni kujaribu kuonyeshakuwa Magufuri hakufanya lolote.
 
Watu husifiwa kwa mambo waliyotekeleza, sio waliyopanga au kuacha katika makaratasi, Elon Musk anajulikana kama yeye ndio kila kitu Tesla wakati alinunua kampuni kutoka kwa watu waliokuwa wanambwelambwela kibiashara, hakuna mtu anayekumbuka tena hata majina tu ya hao ambao kampuni ilichukuliwa kutoka mikononi mwao.
 
mbona Stiegler's Gorge imechukuwa zaidi ya miaka 40?
 
mzee kafeli sana kwenye hilo, hakuna legacy yake iliyobaki hata moja, zaidi sana nakumbuka tu maneno kwamba ukitaka kula ukubali kuliwa. jiwe alipokuja ndio maana aliamua kuvuruga kila kitu chake kwasababu havikuwa na maana yeyote. nyerere aliona mbali sana juu yake kweli alikuwa hatoshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…