Alikuwa mzee wa michakato tupu, nchi ilipata hasara sana kuwa na huyu uongozini
..hakuna awamu ambayo hajafanya maamu
Alifanya mengi ila sio kwenye ujenzi wa strategic infrastructures kama reli, bandari na bwawa la umeme. Mi sikuzote nawaza kama Magufuli angekuwa na access ya matrillion anayopewa mama kila kona ya dunia nadhani bongo ndani ya miaka 20 ingekuwa kama Dubai. Angalia wanaopewa hayo mahela sasa nini wanafanya zaidi ya kugawana hovyo hovyo na wizi na kubadilisha magari ya kifahari. Kila mtu anapambana adokoe fungu katika eneo lake.
We imagine JPM katengeneza vitu vingapi kwa wakati mfupi namna hio. Mengine wana CCM waliona kama hatustahili au hayawezekani ila Magufuli alithubutu na yanaonekana leo na yatanufaisha vizazi na vizazi.
Na hio ni sababu hakukuwa na mtu wa kumzinga zinga mbele. It means toka akiwa waziri wa ujenzi alikuwa na vision ya mambo makubwa ila kulikuwa na mtu mbele anamwambia ngoja kwanza tutafanya tu. Miaka nenda rudi subiri subiri haziishi.
..waliowezesha nchi kuwa na access na matrilion ni Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa.
..Mwinyi na Mkapa walikuta serikali ina matatizo makubwa ya kifedha na ina wakati mgumu sana kupata misaada au mikopo.
..Mzee Kikwete, Magufuli, na Mama Samia, wao wamekuta nchi inaweza kukopeshwa, na kupata misaada toka nje.
..hakuna Raisi ambaye hakujenga mradi wa umeme, daraja la kimkakati, au kuendeleza bandari.
..kwa mfano, daraja la mto Rufiji, ujenzi wake ulianza wakati wa Mzee Mwinyi ukakamilika wakati wa Mzee Mkapa. Wananchi wa mikoa ya kusini walikuwa na shida kubwa ya usafiri wa barabara wakati wa Rais Nyerere, na Mwinyi, wamepata nafuu wakati wa Mkapa.
..Mkapa ndio alikamilisha ujenzi wa daraja la Mto Rufiji lakini hawezi kubeza jitihada za Nyerere na Mwinyi kupeleka barabara kusini.
NB:
..Wazo la kujenga bwawa la umeme Stieglers lilikuwepo toka wakati wa Mwalimu Nyerere.
..pia kulikuwa na wazo barabara ya kwenda mikoa ya kusini ipite ktk mradi wa Stieglers.
..Mradi wa ujenzi wa reli toka Tanga kwenda Musoma uko kwenye mipango ya serikali toka wakati wa Mwalimu Nyerere. Na una kikwazo kikubwa kwamba unaepuka vipi kupita ktk mbuga ya Serengeti.