Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Rais Kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa. Rais amesema reli nyembamba inapatikana eneo la Afrika Mashariki tu.

Mh. Rais kayasema hayo mkoani Simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani.

View: https://youtu.be/CAe_1eN8VAM?si=V_nFyEigpZq3r2_u

CHANZO: ITV

MY TAKE:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!
 
Inatakiwa wafanye mambo chapuchapu na sio kutangaza nia. Inatakiwa mtu kutangaza uwe tayari na pesa LLD na HLD ziko in place tayari. Unatangaza hivyo na kuwaambia ujenzi unaanza tarehe fulani. Huo ndo muono wangu.
 
Ni juzi juzi tu Waziri Mwakyembe alisema kuwa reli ya kati itaimarishwa kwa kuweka reli nzito katika zile sehemu zenye reli nyepesi.

Leo JK anasema kuna mpango wa kubadili reli ya kati kuwa ya kimataifa (standard gauge).

Kwa sasa, kuna injini za treni (8 kama sikosei) zinafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni kutoka Malasyia katika karakana ya Reli Morogoro.

Vile vile, kuna injini nyingine mpya na behewa ambazo nasikia zimeagizwa.

Sasa kama kuna mpango wa kupanua reli ya nini kuingia gharama za kuimarisha reli iliyopo, na kununua behewa mpya pamoja na injini ambazo hazitaweza kutumika katika reli pana?!

Ni nani kati ya JK na Mwakyembe anasema ukweli?
 
MkamaP, Salary Slip

..lakini JK alishatangaza hii "nia" in 2011.

..sasa tangu wakati huo serikali imefanya nini?

..kwanini in 2013 anarudia kutangaza "nia" aliyokwisha tangaza hapo awali??

..kwanini hatendi??

..wakati mwingine nalazimika kukubali kwamba kuna justification ktk hizi dharau na kejeli toka kwa majirani zetu wa Afrika Mashariki. Uongozi wetu umekuwa wa maneno-maneno tu kama hizo "nia" zinazotangazwa na viongozi wetu.

..someni hapa:Tanzania, Rwanda, Burundi team up on $5bn rail proposal

cc Geza Ulole, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Salary Slip,

..wakati Raisi Kikwete anatangaza "nia" ya kujenga reli, Raisi Uhuru Kenyatta atakuwa na ground breaking ceremony ya ujenzi wa reli toka Mombasa kuelekea Uganda na Rwanda kesho.

cc Koba, Ritz, Mchambuzi, Kubwajinga
Mkuu JokaKuu

Tanzania hatufanyi mashindano na Kenya kila nchi inaangalia maitaji yake. Kenya wanahangaika wanajidanganya sana wakifanya miradi mingi watazidi kuwa super power afrika mashariki.

Wanaufanyia marekebisho ya uwanja wao Jomo Kenyatta airport kwa mwaka wawe wanapitisha watu milioni 40 hizo ni akili waka Dubai ndiyo wanakimbilia 40/50 sijui abiria watawatoa wapi, wanadhani kila siku Tanzania na Uganda watakuwa na airport mbovu.

Nampongeza rais wetu kwa ujenzi huo utapunguza gharama.
 
Last edited by a moderator:
Mh.Raisi Kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa.Raisi amesema reli nyembamba inapatikana eneo la Afrka mashariki tu.

Mh.Raisi kayasema hayo mkoani Simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!
Kwa nini isitekelezeke, na nia ipo.
 
JokaKuu

Mie kwa kweli sio mfuasi wa kutangaza nia, haya mambo yanatakiwa uanze kufanya ama ukija kutangaza nia basi una tarehe ya kuanza. Hii ni kwa sababu,
a) Mataifa ya magharibi hayataki waafrika waendele ili wawe na upenyo wa ku dictate terms zao.
b)Baadhi ya mataifa jirani pia hayapendi mtanzania aendelee ili nao wanufaika wajuavyo.
Hivyo ukitangaza nia kwa jambo la maendeleo kabla halijaanza utapata vikwazo vingi, yapo mataifa mfano ya magharibi yataenda huko unakotegemea kupata fedha kuwashawishi wasitoe pesa ama nk.

Mfano mzuri ni barabara inayopita sengereti jinsi ilivyopingwa kila kona, inaweza kuwa kweli siyo nzuri kupitisha barabara ktk mbunga ile, lakini hapa ninajaribu kuonesha vulnerability ya kutangaza nia bila kuwa tayari resources ziko secured.

Mfano pia kutangaza nia kunawapa wanahakati wa ma roli kujiweka ktk nafasi nzuri ya kuhujumu juhudi hizo za ujenzi wa reli ya kati. Wakati ilitakiwa kuwapa suprise, wakija kuzinduka tayari reli ilishaanza kujengwa. Mambo ya kutangaza nia sio mazuri ktk project, yanakaribisha maadui kujipanga kwa mikakati ya kukwamisha. Ndo maana nafikiri wawe wanatangaza wakiwa wameshaanza ama wameshakwisha finalize kila kitu.
 
Mkuu JokaKuu

Tanzania hatufanyi mashindano na Kenya kila nchi inaangalia maitaji yake. Kenya wanahangaika wanajidanganya sana wakifanya miradi mingi watazidi kuwa super power afrika mashariki.

Wanaufanyia marekebisho ya uwanja wao Jomo Kenyatta airport kwa mwaka wawe wanapitisha watu milioni 40 hizo ni akili waka Dubai ndiyo wanakimbilia 40/50 sijui abiria watawatoa wapi, wanadhani kila siku Tanzania na Uganda watakuwa na airport mbovu.

Nampongeza rais wetu kwa ujenzi huo utapunguza gharama.

..unampongeza kwa ujenzi au kurudia kutangaza "nia" aliyotangaza mwaka 2011??

..sasa hata kama hatushindani na Kenya, je sisi wenyewe hatuhitaji bandari, reli, na viwanja vya ndege vya kisasa??

..kwanini miradi hiyo inabakia kwenye "nia" tu miaka nenda rudi??
 
Salary Slip,

..wakati Raisi Kikwete anatangaza "nia" ya kujenga reli, Raisi Uhuru Kenyatta atakuwa na ground breaking ceremony ya ujenzi wa reli toka Mombasa kuelekea Uganda na Rwanda kesho.

cc Koba, Ritz, Mchambuzi, Kubwajinga

Hii mbona ilikuwa tayari ianze kujengwa lakini Rwanda ndio wamechelewesha kwa visa vyao, lakini naona Tanzania na Burundi will go ahead kwani feasibilty imeshafanywa na ujenzi wake hautochukuwa muda mrefu, jisomee zaidi; Canarail reveals Tanzania-Rwanda railway construction underway
 
Mkuu JokaKuu

Tanzania hatufanyi mashindano na Kenya kila nchi inaangalia maitaji yake. Kenya wanahangaika wanajidanganya sana wakifanya miradi mingi watazidi kuwa super power afrika mashariki.

Wanaufanyia marekebisho ya uwanja wao Jomo Kenyatta airport kwa mwaka wawe wanapitisha watu milioni 40 hizo ni akili waka Dubai ndiyo wanakimbilia 40/50 sijui abiria watawatoa wapi, wanadhani kila siku Tanzania na Uganda watakuwa na airport mbovu.

Nampongeza rais wetu kwa ujenzi huo utapunguza gharama.
Msemaji wa JMT jibu na Kigoma kuww Dubai, lini? Au baga ndio panakuwa Dubai. Sema tumeshindwa na kukubali ukweli sio dhambi
 
Last edited by a moderator:
..unampongeza kwa ujenzi au kurudia kutangaza "nia" aliyotangaza mwaka 2011??

..sasa hata kama hatushindani na Kenya, je sisi wenyewe hatuhitaji bandari, reli, na viwanja vya ndege vya kisasa??

..kwanini miradi hiyo inabakia kwenye "nia" tu miaka nenda rudi??
Rais lazima atangaze nia ndiyo ujenzi uanze bandari tayari wameishaingia mkataba na makampuni ya China wanajenga Bagamoyo.

Tanzania wanajenga airport Dar es Salaam Third Terminal kampuni mbili za Uingereza na Ujerumani wameishaingia mikataba.

Reli hiyo inajengwa mradi unaanza wakati wowote kuanzia sasa.
 
Hii mbona ilikuwa tayari ianze kujengwa lakini Rwanda ndio wamechelewesha kwa visa vyao, lakini naona Tanzania na Burundi will go ahead kwani feasibilty imeshafanywa na ujenzi wake hautochukuwa muda mrefu, jisomee zaidi; Canarail reveals Tanzania-Rwanda railway construction underway

..kipande kikubwa cha reli kiko upande wa Tanzania.

..pia kama Rwanda wameleta longolongo, mbona kipande cha kwenda Burundi nako hamna kinachoendelea?

..jamani kila siku ni maneno-maneno tu?? Tangu wakati waziri ni Dr.Kawambwa, akaja Omari Nundu, sasa hivi Dr.Mwakyembe, ni "nia", "nia", "nia."

..tukilemaa mpaka Rwanda na Burundi wakajenga reli kuelekea Uganda then Kenya, itakuwa ndiyo imetoka hiyo kwa upande wa Tanzania. Unless tutakuwa na pesa za kuwajengea reli mpaka Kigali na Bujumbura.

..lakini hata bila ya kufikiria ku-extend reli kwenda Kigali, bado pale Isaka kuna kituo[dry port] cha mizigo ya kwenda Rwanda. Lakini kwasababu reli ya kati imekufa basi kituo hicho nacho kimedorora.
 
mh.raisi kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa.raisi amesema reli nyembamba inapatikana eneo la afrka mashariki tu.

Mh.raisi kayasema hayo mkoani simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa simiyu na mikoa ya jirani.

Chanzo:itv

my take:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!

sawasaw raisi wangu uliejaa katika mioyo ya watanzania kwa uttendaji wako uliotukuka.
 
Rais lazima atangaze nia ndiyo ujenzi uanze bandari tayari wameishaingia mkataba na makampuni ya China wanajenga Bagamoyo.

Tanzania wanajenga airport Dar es Salaam Third Terminal kampuni mbili za Uingereza na Ujerumani wameishaingia mikataba.

Reli hiyo inajengwa mradi unaanza wakati wowote kuanzia sasa.

..mkataba wa bandari ya Bagamoyo ulisainiwa wakati Raisi wa China ametembelea Tz.

..sasa tangu wakati Raisi wa China amekuja hapa ni muda gani?

..majuzi PM Pinda alikuwa China anazungumzia bandari ya Mtwara.

..hawa watu wako very efficient ktk kusafiri tu, lakini ni zero kwenye kufanya kitu kikaonekana.

..tukubali ukweli kwamba JK na serikali yake wako too slow, na ndiyo maana nikatoa mfano wa Raisi Uhuru Kenyatta.
 
Back
Top Bottom