Wewe wacha porojo, kabla ya kushika uongozi Kikwete hata kwenda Mwanza kutokea Dar ilikuwa mpaka tupiptie Kenya. barabara nyang'a nyang'a toka wakati wa Nyerere. Leo unakwenda huku unakunywa gahwa ndani ya gari, hulijui hilo?
Miradi ya barabara Tanzania wakati huu ni mingi kuliko nchi yoyote ya Afrika chini ya Sahara.
Bandari usifikiri ni lelemama ile, usaini mkataba leo kesho uanze kujenga, kuna watu wa kuwahamisha, kuna miundo mbinu ya kutayarishwa, kuna logistics za kutayarishwa, kuna vifaa vya kukusanywa nje na ndani ya nchi, kuna upimaji wa kina cha maji, kuna upimaji wa udongo uliopo nje na na baharini kuna kila namna ya matayarisho (mobilization), na kwa mradi mkubwa haya matayarisho pekee huchukuwa si chini ya miaka miwili. Usifikiri kuna kucheza mdako pale.
Hivi hizo shule mlienda kufutwa ujinga au kujazwa ujinga?