Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Ninachosema ni kwamba huwezi kujenga uchumi kwa njia za kufikirika...kwamba kwavile (say) Air Tanzania haina ndege wakati hata Rwanda wana ndege ndo basi tena nasi tununue ndege bila kufanya prioritization...huo utakuwa ni uchumi wa ajabu! Ninachosema ni kwamba we've already messed up for the past 50 years kwahiyo katika mazingira kama hayo ni lazima ufahamu uanze na nini kisha ufuate nini!
...tuliposema tunafufua shirika na tukaweka mkuu "mpya", kumbe haikuwa priority? what are you trying to say? we are jokers? or am i missing the point here.

Umechukulia mfano wa umeme....kuna watu wanadai zamani hapakuwa na matatizo ya umeme huku wakisahau kwamba enzi hizo hatukuwa na demand kubwa ya umeme!!
...umeme unatolewa bure? kama unatolewa bure -kwa watu kutolipa bill zao- tunafanyaje? tunaacha ku fulfill mahitaji yaliyopo na yajayo?
...kwa mtindo huo, tutavutia wawekezaji wa aina gani?

Baada ya economic liberalization, demand ya umeme ikaongezeka maradufu ndani ya kipindi kifupi wakati uzalishaji ulikuwa ni uleule! Demand ikaendelea ku-shoot year after year na hivi sasa umeme ni moja ya zile multiple objectives ambazo nimezisema awali! Sasa unapokuwa katika mazingira kama hayo ni lazima u-choose among the best alternatives! Huku hakuna umeme, kule hakuna barabara, upande wa pili hakuna maji; mtaa wa tatu, shule na idadi ya wanafunzi vimeongezeka maradufu; ukigeuka upande mwingine unakuta unalazimika kuongeza vituo vya afya...and so on!! Katika mazingira kama hayo, lazima uchague, uanze na kipi na kwa ukubwa gani unless kama kuna sehemu ambako unaweza kwenda kuchota fedha na kumaliza yote hayo kwa pamoja!
...kama movie ati eeh! and unafikiri hivi vyote vilitokea kwa overnight?
...kwa ufupi, unasema there is none we can do about it.

trust me bado nchi hii ina matatizo ambayo wala watu hatujadili ufumbuzi wake! Wanasiasa na wasomi tumekuwa hodari sana wa kukosoa na kullalamika lakini sijapata kusikia msomi wala mwanasiasa yeyote akitoa suluhisho la maana!Kwamba nchi hii kuna rushwa, ni jambo ambalo hakuna anayepinga! Kwamba nchi hii watu ni wazembe
...NasDaz, umekuwa humu kipindi sasa, unataka kusema hujawahi ona mjadala unaoongelea nini kifanyike kuhusiana na suala fulani?

...suluhisho la maana ni lipi?

...nadhani, uzembe mwingi ni ule wa kutumia akili.

Hayo yote yanashiria jambo moja kwamba bado kabisa hatujafahamu vyanzo vya msingi vya umaskini wetu na matokeo yake tunaishia kutoa sababu za jumla jumla na hivyo kushindwa kuyaona matatizo ya msingi! TUnaambiwa kwamba wakati wa awamu ya kwanza, kiwango cha rushwa/ufisadi nchini kilikuwa chini sana; lakini bado Tanzania ilikuwa masikini wa kutupwa!
...vyanzo vinafahamika! angalia ubora na ufaulu katika elimu, ubora na upana wa huduma za msingi za afya. angalia vikwazo katika umiliki mali, na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

...nigusie zao moja tu, korosho. tunajua jinsi gani mkulima wa zao hili huko nyuma alifaidika na hivi sasa hali ikoje? hapa ndipo kilipo chanzo cha umasikini katika eneo hili.

Lakini pamoja na yote hayo, bado tatizo la msingi litabaki palepale kwamba tunahitaji vyanzo vingi na vikubwa zaidi vya mapato na ku-prioritize our objectives. Hili la vyanzo vya mapato huwa hatulijadili kabisa, mara zote tunajadili matatizo!
...matumizi ndugu, matumizi! hata kama tukipata fedha wanayopata Saudia, haitasaidia kama matumizi yatakuwa ya hovyo hovyo na yasiyo na ufuatiliaji wala kuwajibishana. unasoma ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali? unajua ni kiasi gani cha fedha kinapotea katika halmashauri zetu? hebu tuanzie hapo!
 
Jenga hoja kijana badala ya kuongea kiujumla bila kuonyesha kujadili kwa kina nini unapinga na nini unakubaliana nacho.

MIMI NIMESHAWAAMBIA MNAPENDA KUJADILI KISIASA SIASA NDIO MAANA HUWEZI KUWA OBJECTIVE SINCE YOU HAVE POLITICAL EMOTIONS. Jisome hapa uone
Mkuu naona umegonga mahali panapouma. Ni kweli kwa kumsoma huyu ndugu yetu unafahamu mtazamo wake ni wa kuwatetea watawala badala ya wananchi. Yawezekana kwa namna moja na nyingine anafaidika na utawala wa sasa!
 
Pole yako na wewe...na pole sana!! Mahali panapouma ni wapi? Kwani kuwa CCM ni dhambi? Kwa taarifa yako mimi sishikiwi akili na wanasiasa kama mlivyo nyinyi! Humu nishasema mara kibao tu na nitaendelea kusema wazi bila kung'ata maneno kwamba CCM na CHADEMA wote ni wale wale! Tofauti yenu kubwa ni kwamba mmoja ndie fisadi na mwizi wa sasa na mwingine ni fisadi na mwizi wa baadae. Nikiona watu walio kwenye official political system kama vile (say) akina Heche or Mnyika wanatoka mapovu basi huwa nawaelewa sana kwavile nafahamu wanatetea kula yao; wanatetea matumbo yao; wanatetea wapate nafasi ili nao wakaibe vizuri kama wanavyoiba wenzao lakini kwa upande mwingine ninapokuta mtu ambae hayupo kwenye official channel halafu, yaani labda ni mwanachama wa kawaida tu au si ajabu hata kadi yenyewe hana halafu bado anakuja hapa na kutoka mapovu; kwa kawaida mtu kama huyo huwa namdharau kwavile hajitambui na wala hajui anapigania nini! Kwahiyo nawe jichunguze, kama upo kwenye proper channel basi nitakuelewa kwavile nafahamu unapigia kelele ugali wako wa kila siku lakini ikiwa ni shabiki tu basi nakuhurumia kwavile hujitambui! Narudia, kwangu mimi CCM na CHADEMA wote ni wezi tu....hili sijaanza kusema leo!!
 
Ni juzi juzi tu Waziri Mwakyembe alisema kuwa reli ya kati itaimarishwa kwa kuweka reli nzito katika zile sehemu zenye reli nyepesi.

Leo JK anasema kuna mpango wa kubadili reli ya kati kuwa ya kimataifa (standard gauge).

Kwa sasa, kuna injini za treni (8 kama sikosei) zinafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni kutoka Malasyia katika karakana ya Reli Morogoro.

Vile vile, kuna injini nyingine mpya na behewa ambazo nasikia zimeagizwa.

Sasa kama kuna mpango wa kupanua reli ya nini kuingia gharama za kuimarisha reli iliyopo, na kununua behewa mpya pamoja na injini ambazo hazitaweza kutumika katika reli pana?!

Ni nani kati ya JK na Mwakyembe anasema ukweli?
Wanatudanganya.
Sasa sijui ni kwa manufaa ya nani
 
Kenyatta hana longolongo kwenye masuala ya kitaifa hasa eneo la uchumi kama reli wetu huyu JK ni siasa tu hata kwenye mambo sensitive ya kiuchumi kama haya.
 
Mjadala huu unaelekea kwenye JAZBA mkuu NasDaz tulia kdg! SIASA ndo inajenga nakuboamoa NCH umeongea mengi kwann hatujafanikiwa sn above50 yrs! Kwann unawaponda wanaolaumu utawala uliopo? ukweli nihuu na hili wa2 wengi 2najifanya MBUNI hakuna NCH imeendelea kwa kuwa na CHAMA 1 milele hata wazungu wanendelea 7bu hiyo! lkn huku km ndo hv then 2nategemea Maendeleo 2tangoja sn itafika 100yrs 2tajivunia kuwa na wahitimu wengi wasiojua KUSOMA nabado 2tashangilia hapa ndo kwenye Tatizo!
 
DAR si LAMU,
Nikukumbushe tu kwamba aina ya quotation uliyofanya inapendeza zaidi kwa kujibu hoja badala ya kujibu hoja na kuchomekea maswali kwavile inakuwa headache kujibu kila kipengele hasa kv ukishafanya quotation; maelezo zile individual quotation huwa zinachanganyika. Hata hivyo, acha nijibu machache.
Mimi nilisema hivi:
Ninachosema ni kwamba huwezi kujenga uchumi kwa njia za kufikirika...kwamba kwavile (say) Air Tanzania haina ndege wakati hata Rwanda wana ndege ndo basi tena nasi tununue ndege bila kufanya prioritization...huo utakuwa ni uchumi wa ajabu! Ninachosema ni kwamba we've already messed up for the past 50 years kwahiyo katika mazingira kama hayo ni lazima ufahamu uanze na nini kisha ufuate nini!
Kisha wewe unahoji:
..tuliposema tunafufua shirika na tukaweka mkuu "mpya", kumbe haikuwa priority? what are you trying to say? we are jokers? or am i missing the point here.

Ngoja nikuulize; yaani unaamini hoja yako inafanana na nilichosema mimi? Mimi nimezungumzia suala la ku-prioritize…kwamba kwavile kunakuwa na multiple objectives wakati resources haziwezi kukidhi mahitaji yote, basi busara zakiuchumi ni ku-choose among multiple objectives! Na ndio maana nikasema, huwezi kununua ndege kwavile tu umeona Rwanda nchi ndogo wana ndege. Inawezekana wao ndege ndiyo kipaumbele!

Baadae uka-quote kipengele kidogo tu katika hoja mzima. Ulicho-quote ni:
Umechukulia mfano wa umeme....kuna watu wanadai zamani hapakuwa na matatizo ya umeme huku wakisahau kwamba enzi hizo hatukuwa na demand kubwa ya umeme!!

Ulichohoji ni:
..umeme unatolewa bure? kama unatolewa bure -kwa watu kutolipa bill zao- tunafanyaje? tunaacha ku fulfill mahitaji yaliyopo na yajayo?
...kwa mtindo huo, tutavutia wawekezaji wa aina gani?
Lazima niseme wazi wala sijaipata hoja yako hasa nikizingatia kwamba hakuna uhusiano kati ya nilichosema na ulichohoji. JokaKuu alihoji nchi kuwa na uhaba wa umeme kwa muda mrefu sasa nami nikaeleza demand ya umeme before economic liberalization kwamba ingawaje tulikuwa hatuzalishi umeme mwingi kabla ya mageuzi ya kiuchumi lakini bado umeme huo huo kidogo ulionekana kutosha na hivyo nchi kutokuwa na mgao. Umeme ulikuwa unatosha kv hapakuwa na demand ya umeme even at household level; na ndio maana nikatoa mfano wa pasi ya umeme, kwamba ungeweza kuzunguka mtaa mzima (tena mahali kama Dar) lakini bado usikute nyumba yenye pasi ya umeme! Kwa bahati mbaya au mzuri, tuka-liberalize our economy; demand ya umeme ika-shoot ghafla not only at commercial level bali hata kwenye household level! Matokeo yake wakati zamani ungeweza kuzunguka mtaa mzima usikute nyumba yenye pasi ya umeme, leo kwa mji kama Dar unaweza kukuta nyumba yenye familia tano nayo ina pasi tano za umeme, mafriji matano, majiko matano ya umeme and so on!! Haya yalitokea kabla hatujajiandaa na matokeo yake umeme nao ukawa ni among of multiple objectives! Huku tunahitaji umeme, kule tunahitaji barabara! Huku tunahitaji hospitali na madawa kule hakuna shule. Hizo ndizo multiple objectives. Sasa basi, katika mazingira kama hayo ni lazima uangalie uanze na kipi na kwa kiasi gani kisha kifuate kipi na kwa level gani. Unatakiwa kuangalia uanze na kipi na kwa level gani kwavile huna resources za kutosha ku-cover yote kwa pamoja! Wewe wa mjini unaweza kuona kipaumbele chako ni umeme wakati wa kijijini kipaumbele chake ni angalau zahanati!

Kisha uka-quote hii:
Baada ya economic liberalization, demand ya umeme ikaongezeka maradufu ndani ya kipindi kifupi wakati uzalishaji ulikuwa ni uleule! Demand ikaendelea ku-shoot year after year na hivi sasa umeme ni moja ya zile multiple objectives ambazo nimezisema awali! Sasa unapokuwa katika mazingira kama hayo ni lazima u-choose among the best alternatives! Huku hakuna umeme, kule hakuna barabara, upande wa pili hakuna maji; mtaa wa tatu, shule na idadi ya wanafunzi vimeongezeka maradufu; ukigeuka upande mwingine unakuta unalazimika kuongeza vituo vya afya...and so on!! Katika mazingira kama hayo, lazima uchague, uanze na kipi na kwa ukubwa gani unless kama kuna sehemu ambako unaweza kwenda kuchota fedha na kumaliza yote hayo kwa pamoja!
Kisha na wewe unahoji:
...kama movie ati eeh! and unafikiri hivi vyote vilitokea kwa overnight?
...kwa ufupi, unasema there is none we can do about it.

Hiyo hoja yako ya kwamba "kwa ufupi, unasema there's none we can do it about!" Are serious? Kwanini unasoma vitu nusunusu? Ni kweli unasoma nusunusu au unaamua tu kupotosha? Ina maana hujasoma kipengele cha chini nilichosema: "Katika mazingira kama hayo, lazima uchague, uanze na kipi." Kwahiyo according to you, ku-prioritize mambo ni sawa na nothing we can do?!

Kisha ukaja hoji tena kwa kusema:
..NasDaz, umekuwa humu kipindi sasa, unataka kusema hujawahi ona mjadala unaoongelea nini kifanyike kuhusiana na suala fulani?

...suluhisho la maana ni lipi?

...nadhani, uzembe mwingi ni ule wa kutumia akili.

Kama umenisoma vizuri nimesema kwamba watu tunajadili mambo yale yale tena kijumla jumla. BInafsi niliweka tatizo kubwa la msingi kwamba ubongo wetu ume-stuck na tumeshindwa kuwa na vyanzo vikubwa vya mapato. Sijaona mjadala wa kina unaozungumzia vyanzo vikubwa vya mapato. Kama upo, nipe link.

Kisha tena ukaja na hoja hii:
...vyanzo (vya umasikini) vinafahamika! angalia ubora na ufaulu katika elimu, ubora na upana wa huduma za msingi za afya. angalia vikwazo katika umiliki mali, na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Tunaambiwa kwamba zamani tulikuwa na ubora mkubwa sana wa elimu; je tulikuwa katika hali gani kiuchumi kwa kulinganisha na ubora wa elimu ambao tulikuwa nao? Unapozungumzia vikwazo ktk umiliki mali unamaanisha nini hasa? Unataka kuniambia kwamba unakatazwa kumiliki mali au unazungumzia wale wanaotaka kuwa madalali wa vitalu vya gesi?

Kisha ukahoji:

...nigusie zao moja tu, korosho. tunajua jinsi gani mkulima wa zao hili huko nyuma alifaidika na hivi sasa hali ikoje? hapa ndipo kilipo chanzo cha umasikini katika eneo hili.
Hiyo neema ya zao la korosho ilidumu kwa muda gani? Mimi natokea Lindi, moja ya mkoa ambao unazalisha korosho lakini hiyo neema ya korosho inayozungumzwa wala sikuikuta! Which means, hata kama neema hiyo ilikuwepo lakini haiku-exist kwa muda mrefu.

Hoja yako nyingine:
...matumizi ndugu, matumizi! hata kama tukipata fedha wanayopata Saudia, haitasaidia kama matumizi yatakuwa ya hovyo hovyo na yasiyo na ufuatiliaji wala kuwajibishana. unasoma ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali? unajua ni kiasi gani cha fedha kinapotea katika halmashauri zetu? hebu tuanzie hapo!

Hilo la ufisadi nimeshalisema sana hadi nikatoa thread zaidi ya tatu humu jamvini nikishauri tuachane na na what's so called Good Governance na badala yake tuwe na Approved Dictatorship Governance. Nilitoa hoja kama hiyo kwavile mimi naamini Tanzania kuna tatizo kubwa sana la ufisadi…jamii yote imeoza bila kujali dini wala itikadi za kisiasa; wengi wetu ni watu wa hovyo sana! Tanzania ni jamii ya watu tusiokuwa na maadili; in short wengi ni wezi! Kwa bahati mbaya wezi hawa wanalindwa na Mfumo wa Utawala Bora! Moja ya misingi mikuu ya Utawala Bora ni Utawala wa Sheria! Katika Utawala wa Sheria mtu ataonekana ana hatia provided imekuwa proved beyond reasonable doubt in the court of law kwamba muhusika ametenda kosa! Ni nani basi anaweza ku-prove beyond reasonable doubt kwamba mtuhumiwa ametenda kosa wakati jamii yenyewe imeoza kwa ukosefu wa maadili?

Lakini kwa upande mwingine, leo hii hata kama haitaibwa hata senti tano, lakini bado changamoto za umaskini hazitaisha kwavile bado mapato yetu ni madogo sana. TRA kwa mwaka wanakusanya kiasi cha Sh. Trillion 7 tu (and am afraid kama wanafika). Tuseme wamekwiba nusu, wameleta nusu na sasa tuseme wanakusanya Trillion 14 na kisha Bajeti yetu ipande kutoka kutoka Trillio 18 hadi Trillion 30! Hata hivyo, ni bado sana katika kuwa na uchumi bora.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu wangu, sio kwamba nawaponda wanaosema serikali iliyopo ni tatizo; kinachonikera mimi ni pale mtu ukiangea kile unachokiamini basi wanatokea wengine wanakumbia wewe ni chama hiki au chama kile kwavile unatofautiana nao kimtazamo! Huu ni ujinga!

Nikirudi kwenye hoja yako kwamba SIASA ndiyo inajenga na kubomoa nchi, nakubaliana na wewe kwa 100% lakini ninachosema mimi ni kwamba bado sijaona tofauti iliyopo kati ya CCM na CHADEMA, au CCM na CUF n.k! CCM, CUF, CHADEMA, NCCR n.k ni wale wale tu; at least for now, sioni chama chenye nia ya kweli ya kuondoa matatizo ya Mtanzania; wengi wa wanasiasa ni wachumia tumbo! Angalia hata hao wa upinzani wanavyoparuana wao kwa wao wakati msingi wa kuparuana kwao ni maslahi binafsi lakini bado watu wanataka kila mmoja aamini kwamba kikiingia chama fulani, basi nchi itabadilika....hakuna kitu kama hicho! Narudia, CCM na CHADEMA wote ni wale wale tu; CCM na CUF wote ni wale wale tu; hutaki unaacha!
 
Nguruvi3, NasDaz, DAR si LAMU,

..tumepoteza mapato kiasi gani kila mwaka ktk dhahabu, tanzanite, etc.

..hivi ina maana serikali hawalijui suala hili au wanafanya makusudi tu?
JokaKuu,
Sina shaka kwamba tunapoteza mapato mengi sana, hilo halina ubishi. Kwamba hivi sasa serikali hawajui au wanafanya makusudi jibu ni kwamba wanafahamu na ndio maana wakati tunaingia kwenye mining economy, hapakuwa na taasisi inayohusika na ukaguzi ndipo baadae baada ya kugundua tunaibiwa ndipo wakaanzisha Mining Audit Agency. Aidha, kwavile serikali iligundua kwamba vidani ni moja ya njia zinazotumika kuiba ndipo ikapitishwa sheria ni gramu ngapi za vidani zinakuwa accepted kama ni for personal use na ikizidi, unahesabika kwamba ulitaka kutorosha madini! Na kwa kupitia njia hii, kuna vidani vya billions of TZS pale Airport vimekamatwa ambavyo zamani vingehesabika kwamba ni vidani for personal use.
Pamoja na yote hayo bado am very certain kwamba bado tunapoteza mapato mengi kwenye sekta ya madini. Nimekupa mifano ya hapo juu ili kujibu hoja yako kwamba je, serikali haifahamu au wanafanya makusudi! Lakini hata hivyo, bado mkuu wangu tatizo lako ni lile lile…..hujioni kabisa kwamba nawe(kama Mtanzania) ni sehemu ya tatizo la nchi hii! Wengi tunalalamika serikali serikali huku tukisahau wajibu wetu! Kama utakumbuka mimi na wewe tulishawahi kuwa kwenye mjadala mzito kuhusu ufaulu Tanzania….wengi wetu kama ilivyo ada, tukasahau wajibu wetu tukawa tunabaki kulalama kuhusu serikali. Kama unakumbuka, wakati tunahitimisha mjadala ule, uliniuliza nina maoni gani kuhusu nini kifanyike ili kuongeza ufaulu. Nikakujibu kwamba lazima kila mmoja atimize wajibu wake! Mwanafunzi lazima atimize wajibu wake wa kusoma kwa bidii. Mzazi lazima atimize wajibu wake wa kumsimamia mwanae na kuhakikisha ana-behave like a student. Mwalimu nae atimize wajibu wake badala ya kuendelea kusingizia maslahi madogo kama kigezo cha kutotimiza wajibu! Mwisho serikali nayo itimize wajibu wake! Aidha nika-conclude kwamba hata kama utakuwa na shule bora kuliko zote duniani zenye kila kitu lakini mwalimu, mzazi na mwanafunzi wakishindwa kutimiza wajibu wao; itakuwa ni kazi bure! Kwa bahati mzuri, ukiangalia matangazo ya HakiElimu hivi sasa yanasisitiza uwajibikaji wa wadau tofauti kabisa na zamani ambapo matangazo yao yalikuwa ni kama vile wanafunzi walikuwa perfect, walimu perfect, wazazi perfect lakini tatizo lilikuwa serikalini pake yake! HakiElimu kwa sasa nao wamegundua kwamba pamoja na matatizo yote ya serikali lakini bado kuna tatizo la wadau (wanafunzi, wazazi na walimu) kutowajibika! JokaKuu, sio kwamba nataka kujifagilia lakini nitasema na kama utaona najifagilia, kimpango wako. Kuna wakati mimi niliwahi kufanya kazi NMB na kwa bahati mbaya kabisa nilikuwa nalazimika kufanya kazi nyingi zaidi peke yangu. Ilipokuwa inafika mwisho wa mwezi, nilikuwa naingia ofisini saa kumi, nimechelewa sana saa kumi na moja alfajiri. Nilikuwa nalazimika kufanya hivyo kv nilikuwa nalazimika mishahara ya wafanyakazi inalipwa on time na vile vile nihakikishe naandaa na kuwakilisha monthly reports on time! Na wala si kwamba nilikuwa nafanya hayo kwa ajili ya posho; manake hadi natimuliwa NMB, hakuna kitu ambacho nilikuwa naona uvivu kufanya kama kuandikia Claim ya Sitting Allowance! Simple rule, hakuna atakayekuandikia Sitting Allowance wakati pesa ni zako mwenyewe!! Lakini pamoja na yote hay ohayo, huwezi amini, kuna wapumbavu pale ofisni walikuwa wanasema napenda sifa kwavile tu nilichokuwa nafanya ni wajibu wangu! Hili ndilo tatizo letu, hatupendi kuwajibika lakini ni wepesi sana wa kuilalamikia serikali! With due respect Sir, mkuu wangu JokaKuu nawe ni hodari sana wa kuilalamikia serikali! Je, huwa unatimiza wajibu wako? Na uki-maximize uwajibikaji, kuna wapumbavu watakuchukia na kukuona mpenda sifa!
 
Last edited by a moderator:
Rais Kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa. Rais amesema reli nyembamba inapatikana eneo la Afrika Mashariki tu.

Mh. Rais kayasema hayo mkoani Simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani.

CHANZO: ITV

MY TAKE:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!

Tanzania nchi ya maneno mengi sana. Hivi kutangaza nia kuna maana gani? Kwa nini asitangaze tarehe ya kuanza ujenzi ? Tatizo nchi hii haijui vipaumbele vyake. Bila reli ya kati coalition if the wiling itapeta
 
Thnx ndg yangu NasDaz kwa maelezo! kumbe naww umeliona tatizo ss 2fanyeje? Bcz jamaa wanaolaumu CCM na Gvmnt wanaamini wakibadilisha CHAMA km wanavyofanya watu weupe wanaamini kutakuwa na Maendeleo! bzc wanaSIASA wanapenda sana Kuongoza so akiona kuna m2 mwingine anataka nafasi yake lazima atafanya kz ww unaonaje tueendelee kuiamini CCM? khs mahitaji ya umeme kwa kipindi hicho na sasa hilo ni Tatizo la watawala kutokuwa na Mipango ya muda mrefu cdhani km hili ongezeko limekuja GHAFLA maoni yako ndg!
 
Nas issue sio priority au kutokujua bali ni uzembe na ujinga, na bahati mbaya unafanywa na viongozi wetu.
mfano tuliwekeza kwenye Alliance Air tukaliwa, tukakodisha KIA tuna lipwa dollar 1000 kwa mwezi, huu mwaka wa 30 maendeleo ya majengo na ndege za kutua kuongezeka mmh kama tulivyo ambiwa sioni kama yamefikiwa??? ikaja Atc ya mattaka na kundi lake matokeo mpaka leo wewe unayajua, sasa kama ni , ikaja rites napo bomu, iptl bomu, netgroup bomu, richmond bomu, dowans bomu, sasa hapo suala ni priorities au?
ukaongezea na vitambulisho vya taifa miaka 20 sasa, na hela zimeliwa kwani kuna kampuni ya kenya ilishinda zabuni ya kwanza wakati wa Mwinyi/Mkapa, baadae zikaja story za Malasyia.
 
Watawala wetu huwa wanalenga UCHAGUZI tu. Hivi sasa wanalenga 2015 kwa ahadi kibao.
 
Thnx ndg yangu NasDaz kwa maelezo! kumbe naww umeliona tatizo ss 2fanyeje? Bcz jamaa wanaolaumu CCM na Gvmnt wanaamini wakibadilisha CHAMA km wanavyofanya watu weupe wanaamini kutakuwa na Maendeleo! bzc wanaSIASA wanapenda sana Kuongoza so akiona kuna m2 mwingine anataka nafasi yake lazima atafanya kz ww unaonaje tueendelee kuiamini CCM? khs mahitaji ya umeme kwa kipindi hicho na sasa hilo ni Tatizo la watawala kutokuwa na Mipango ya muda mrefu cdhani km hili ongezeko limekuja GHAFLA maoni yako ndg!
Umeona sasa...umesema kama "wanavyofanya weupe!!!!! Kwanini usiseme kama walivyofanya Zambia, Nigeria, Ivory Coast, Gambia na sehemu zingine kadhaa barani Africa? Kwani huko hawajafanya mabadiliko ya uongozi? Ndio maana nikasema sisi tuna matatizo kuliko tunavyodhania!! Hata kama tutabadilisha vyama kila uchaguzi sisi wenyewe tusipobadilika bado ni kazi bure coz' hao wa kwenye hivyo vyama wanatoka kwenye jamii ile ile ya hovyo hovyo!!!! Jamii ya watu wasiopenda kuwajibika, wezi na wala rushwa! Jamii ambayo leo inamwaga uchafu kwa makusudi kwenye mitaro na kesho ikija mvua na kuleta mafuriko wanaanza kuilalamikia serikali ni jamii isiyojitambua! Jamii isiyojitambua katu haiwezi kuwa na maendeleo kwani kutokana na kutojitambua inashindwa vilevile kufahamu inatakiwa kufanya nini kwavile wanaamini kila kitu kipo hovyohovyo kwa ajili ya serikali huku anasahau kwamba yeye mwenyewe na watu wa karibu ni miongoni mwa matatizo makubwa!!!

Kuhusu nini kifanyike ni kwamba mambo ya kufanyika yapo mengi lakini awali ya yote sisi wenyewe tunatakiwa kubadilika na kuacha kulialia! Kabla ya kulia lia jiulize mwenyewe kwanza ikiwa umefanya ulichotakiwa kufanya at the highest level. Mathalani unakuta mtu hana ajira kwa muda mrefu sana lakini out of 100% of possible organisations ambazo angeweza kwenda physically(recommended job search technique) kuomba kazi; hajaenda hata 5% ya hizo sehemu....sana sana anategemea kutuma CV kupitia email kisha anasikilizia kupigiwa simu ya kuitwa kwenye interview!!!! Nani akuite kirahisi rahisi hivyo halafu bado unakuta huyo huyo anakaa na kulalamikia serikali wakati mwenyewe hajafanya chochote cha maana ktk kutafuta kazi! So, lazima kwanza tubadilike sisi wenyewe! Jamii ikishabadilika nayo itatoa wanasiasa waliobadilika kifikra!!

Wataalamu wa mambo wanasema Shetani alifanya picnic siku ameumbwa mwanamke, fedha na pombe! Kwa wale wanaoamini ktk Mungu, basi atagundua wengi tutaenda motoni kupitia angalau kitu kimoja wapo kati ya hivyo ambavyo Shetani alivisherehekea uumbwaji wake! Maana yangu ni nini, wanadamu tuna hulka ya kupenda fedha na jamii isipokuwa na maadili hulka hiyo inatengeneza ugonjwa wa wizi, rushwa na ufisadi kwavile kila mtu anapenda fedha; hivyo akishindwa kuzipata kwa halali atazitafuta hata kwa njia za haramu(wizi, ufisadi, n.k). Jamii ya hovyo hovyo katu haiwezi kuongozwa na katiba laini laini kama Injili ya Yesu inayohubiri kwamba mwenzako akikupiga kofi shavu la mkono wa kushoto, mgeuzie na shavu la kulia akupige! Kimsingi tunahitaji mfumo wa utawala utaka-shape tabia zetu; mfumo huu katu hauwezi kuwa Utawala Bora kv utawala bora nao ni kichaka cha maovu na ndio maana viongozi karibu wote wa Afrika hawajawahi kuulalamikia mfumo wa utawala bora tofauti na mifuno mingine ambayo kila tulipoletewa; tiliitia kasoro na kuikejeli!

Watu tukishaanza kuwajibika, ndipo tutagundua kwamba vyanzo vya mapato ni vidogo mno hata kama rushwa itaisha! Hapo watu watawajibika kubuni mipango itakayoongeza mapato. Hapo ndipo watu watakapogundua kwamba ili uchumi uwe sustainable basi ni lazima tuangalie namna ya kuvigawa vipaumbele vyetu. Hapo ndipo mtu atakapogundua kwamba ikiwa nchi kwa upande mmoja haina barabara na kwa upande mwingie haina standard gauge railway; tuanze na nini na kwa kiwango gani na kwanini!
 
Mkuu August,
Nimetaja mambo mengi ikiwa ni pamoja na hayo uliyoyataja hata kama nitakuwa nimeyataja in other way round. Tatizo letu ni kwamba tunasahau kwamba na sisi Watanzania ni sehemu ya Tanzania!! Hao viongozi unaowataja hawatoki mbinguni bali wanatoka miongoni mwetu....huyu August ambae leo anaesema kuhusu matatizo ya uongozi, kesho akiupata uongozi nae anakuwa sawa na wale wale!! Anakuwa sawa na wale wale kwa sababu nae ni sehemu ya tatizo lakini hajajigundua kwamba nae ni tatizo kubwa nchi hii! Hili halipo Tanzania tu bali karibu nchi zote za Afrika, utafikiri tumepigwa laana! Waafrika wote ni sehemu ya matatizo ya Afrika! Hata kule ambako wameshafanya mabadiliko mara kadhaa bado kuna matatizo kibao coz' wale wapya wanaopata nafasi ya kuongoza nao walikuwa ni sehemu ya tatizo!!
 
Last edited by a moderator:
Nikukumbushe tu kwamba aina ya quotation uliyofanya inapendeza zaidi kwa kujibu hoja badala ya kujibu hoja na kuchomekea maswali kwavile inakuwa headache kujibu kila kipengele hasa kv ukishafanya quotation; maelezo zile individual quotation huwa zinachanganyika. Hata hivyo, acha nijibu machache.
...niwie radhi.
Mimi nilisema hivi:
Ninachosema ni kwamba huwezi kujenga uchumi kwa njia za kufikirika...kwamba kwavile (say) Air Tanzania haina ndege wakati hata Rwanda wana ndege ndo basi tena nasi tununue ndege bila kufanya prioritization...huo utakuwa ni uchumi wa ajabu! Ninachosema ni kwamba we've already messed up for the past 50 years kwahiyo katika mazingira kama hayo ni lazima ufahamu uanze na nini kisha ufuate nini!
Kisha wewe unahoji:
..tuliposema tunafufua shirika na tukaweka mkuu "mpya", kumbe haikuwa priority? what are you trying to say? we are jokers? or am i missing the point here.

Ngoja nikuulize; yaani unaamini hoja yako inafanana na nilichosema mimi? Mimi nimezungumzia suala la ku-prioritize…kwamba kwavile kunakuwa na multiple objectives wakati resources haziwezi kukidhi mahitaji yote, basi busara zakiuchumi ni ku-choose among multiple objectives! Na ndio maana nikasema, huwezi kununua ndege kwavile tu umeona Rwanda nchi ndogo wana ndege. Inawezekana wao ndege ndiyo kipaumbele!
...ndugu, ulipoweka mfano wa shirika la ndege tu, uliupeleka mjadala huko! sasa, labda tujadili au pengine tujiulize, nia ya kufufua shirika -ambapo kulikuwa na mpango wa kununua ndege- ilikuwa ni nini? je, hii haikuwa kipaumbele katika sekta husika?

...kwani, tuliposema tunafufua shirika la ndege, na tutanunua ndege, tulikuwa tunashindana na mtu? si tulikuwa tunatekeleza vipaumbele kwenye sekta hii.

...je, katika miaka ile, vipaumbele katika sekta ya usafirishaji vilikuwa ni vipi? sidhani kama ilikuwa ni barabara pekee. ila, unaweza argue kwamba, ukiangalia resource allocation, ilikuwa ni barabara pekee. but that is misleading, as far as mipango ya taifa inahusika.

Baadae uka-quote kipengele kidogo tu katika hoja mzima. Ulicho-quote ni:
Umechukulia mfano wa umeme....kuna watu wanadai zamani hapakuwa na matatizo ya umeme huku wakisahau kwamba enzi hizo hatukuwa na demand kubwa ya umeme!!

Ulichohoji ni:
..umeme unatolewa bure? kama unatolewa bure -kwa watu kutolipa bill zao- tunafanyaje? tunaacha ku fulfill mahitaji yaliyopo na yajayo?
...kwa mtindo huo, tutavutia wawekezaji wa aina gani?
Lazima niseme wazi wala sijaipata hoja yako hasa nikizingatia kwamba hakuna uhusiano kati ya nilichosema na ulichohoji. JokaKuu alihoji nchi kuwa na uhaba wa umeme kwa muda mrefu sasa nami nikaeleza demand ya umeme before economic liberalization kwamba ingawaje tulikuwa hatuzalishi umeme mwingi kabla ya mageuzi ya kiuchumi lakini bado umeme huo huo kidogo ulionekana kutosha na hivyo nchi kutokuwa na mgao. Umeme ulikuwa unatosha kv hapakuwa na demand ya umeme even at household level; na ndio maana nikatoa mfano wa pasi ya umeme, kwamba ungeweza kuzunguka mtaa mzima (tena mahali kama Dar) lakini bado usikute nyumba yenye pasi ya umeme! Kwa bahati mbaya au mzuri, tuka-liberalize our economy; demand ya umeme ika-shoot ghafla not only at commercial level bali hata kwenye household level! Matokeo yake wakati zamani ungeweza kuzunguka mtaa mzima usikute nyumba yenye pasi ya umeme, leo kwa mji kama Dar unaweza kukuta nyumba yenye familia tano nayo ina pasi tano za umeme, mafriji matano, majiko matano ya umeme and so on!! Haya yalitokea kabla hatujajiandaa na matokeo yake umeme nao ukawa ni among of multiple objectives! Huku tunahitaji umeme, kule tunahitaji barabara! Huku tunahitaji hospitali na madawa kule hakuna shule. Hizo ndizo multiple objectives. Sasa basi, katika mazingira kama hayo ni lazima uangalie uanze na kipi na kwa kiasi gani kisha kifuate kipi na kwa level gani. Unatakiwa kuangalia uanze na kipi na kwa level gani kwavile huna resources za kutosha ku-cover yote kwa pamoja! Wewe wa mjini unaweza kuona kipaumbele chako ni umeme wakati wa kijijini kipaumbele chake ni angalau zahanati!
...maana yangu, kwa ufupi, ni, kama kuna soko la kitu, halafu ni cha muhimu katika maendeleo, yeyote, nasisitiza!, yeyote ya nchi, hiyo huwa kipaumbele namba uno!

...infact, si kipaumbele, ni zaidi ya kipaumbele. ni msingi wa vipaumbele vyote!

...hatuwezi kujitetea tukatoka salama hapo. tukubali tu. tumefeli huo mtihani, ili, tuurudie vyema.

Kisha uka-quote hii:
Baada ya economic liberalization, demand ya umeme ikaongezeka maradufu ndani ya kipindi kifupi wakati uzalishaji ulikuwa ni uleule! Demand ikaendelea ku-shoot year after year na hivi sasa umeme ni moja ya zile multiple objectives ambazo nimezisema awali! Sasa unapokuwa katika mazingira kama hayo ni lazima u-choose among the best alternatives! Huku hakuna umeme, kule hakuna barabara, upande wa pili hakuna maji; mtaa wa tatu, shule na idadi ya wanafunzi vimeongezeka maradufu; ukigeuka upande mwingine unakuta unalazimika kuongeza vituo vya afya...and so on!! Katika mazingira kama hayo, lazima uchague, uanze na kipi na kwa ukubwa gani unless kama kuna sehemu ambako unaweza kwenda kuchota fedha na kumaliza yote hayo kwa pamoja!
Kisha na wewe unahoji:
...kama movie ati eeh! and unafikiri hivi vyote vilitokea kwa overnight?
...kwa ufupi, unasema there is none we can do about it.

Hiyo hoja yako ya kwamba "kwa ufupi, unasema there's none we can do it about!" Are serious? Kwanini unasoma vitu nusunusu? Ni kweli unasoma nusunusu au unaamua tu kupotosha? Ina maana hujasoma kipengele cha chini nilichosema: "Katika mazingira kama hayo, lazima uchague, uanze na kipi." Kwahiyo according to you, ku-prioritize mambo ni sawa na nothing we can do?!
...sikuamua kupotosha, si hulka yangu.

...nadhani, hili nimeshalijibu hapo juu.

Kisha ukaja hoji tena kwa kusema:
..NasDaz, umekuwa humu kipindi sasa, unataka kusema hujawahi ona mjadala unaoongelea nini kifanyike kuhusiana na suala fulani?

...suluhisho la maana ni lipi?

...nadhani, uzembe mwingi ni ule wa kutumia akili.

Kama umenisoma vizuri nimesema kwamba watu tunajadili mambo yale yale tena kijumla jumla. BInafsi niliweka tatizo kubwa la msingi kwamba ubongo wetu ume-stuck na tumeshindwa kuwa na vyanzo vikubwa vya mapato. Sijaona mjadala wa kina unaozungumzia vyanzo vikubwa vya mapato. Kama upo, nipe link.
...wengi hujadili hivyo, ndio. ila, wapo wanaojadili to the word.

...vyanzo vya mapato vilivyopo havitumiki vizuri, or rather, mapato yenyewe. sidhani kama ubongo umekwama.

...hizo threads zipo, sina link zake.

Kisha tena ukaja na hoja hii:
...vyanzo (vya umasikini) vinafahamika! angalia ubora na ufaulu katika elimu, ubora na upana wa huduma za msingi za afya. angalia vikwazo katika umiliki mali, na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Tunaambiwa kwamba zamani tulikuwa na ubora mkubwa sana wa elimu; je tulikuwa katika hali gani kiuchumi kwa kulinganisha na ubora wa elimu ambao tulikuwa nao? Unapozungumzia vikwazo ktk umiliki mali unamaanisha nini hasa? Unataka kuniambia kwamba unakatazwa kumiliki mali au unazungumzia wale wanaotaka kuwa madalali wa vitalu vya gesi?
...ni kiasi gani iko rahisi kwa mwananchi wa kawaida kabisa aka masikini, kupimiwa ardhi na kuthaminishwa, kisha kupewa cheti cha umiliki na cha uthibitisho wa thamani yake? je, nyumba ya Abdallah pale kwa Mnyamani, haina thamani? au anawezaje kuithaminisha katika namna iliyo rahisi?

...MKURABITA uko wapi?

Kisha ukahoji:

...nigusie zao moja tu, korosho. tunajua jinsi gani mkulima wa zao hili huko nyuma alifaidika na hivi sasa hali ikoje? hapa ndipo kilipo chanzo cha umasikini katika eneo hili.
Hiyo neema ya zao la korosho ilidumu kwa muda gani? Mimi natokea Lindi, moja ya mkoa ambao unazalisha korosho lakini hiyo neema ya korosho inayozungumzwa wala sikuikuta! Which means, hata kama neema hiyo ilikuwepo lakini haiku-exist kwa muda mrefu.
...swali ni kwanini? je, utekelezaji wa zoezi la vijiji vya ujamaa ulichangia?

...hali hivi sasa ikoje? unapomkopa mkulima masikini unategemea nini?

Hoja yako nyingine:
...matumizi ndugu, matumizi! hata kama tukipata fedha wanayopata Saudia, haitasaidia kama matumizi yatakuwa ya hovyo hovyo na yasiyo na ufuatiliaji wala kuwajibishana. unasoma ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali? unajua ni kiasi gani cha fedha kinapotea katika halmashauri zetu? hebu tuanzie hapo!

Hilo la ufisadi nimeshalisema sana hadi nikatoa thread zaidi ya tatu humu jamvini nikishauri tuachane na na what's so called Good Governance na badala yake tuwe na Approved Dictatorship Governance. Nilitoa hoja kama hiyo kwavile mimi naamini Tanzania kuna tatizo kubwa sana la ufisadi…jamii yote imeoza bila kujali dini wala itikadi za kisiasa; wengi wetu ni watu wa hovyo sana! Tanzania ni jamii ya watu tusiokuwa na maadili; in short wengi ni wezi! Kwa bahati mbaya wezi hawa wanalindwa na Mfumo wa Utawala Bora! Moja ya misingi mikuu ya Utawala Bora ni Utawala wa Sheria! Katika Utawala wa Sheria mtu ataonekana ana hatia provided imekuwa proved beyond reasonable doubt in the court of law kwamba muhusika ametenda kosa! Ni nani basi anaweza ku-prove beyond reasonable doubt kwamba mtuhumiwa ametenda kosa wakati jamii yenyewe imeoza kwa ukosefu wa maadili?
...swali muhimu kabisa. nakubaliana nawe.

Lakini kwa upande mwingine, leo hii hata kama haitaibwa hata senti tano, lakini bado changamoto za umaskini hazitaisha kwavile bado mapato yetu ni madogo sana. TRA kwa mwaka wanakusanya kiasi cha Sh. Trillion 7 tu (and am afraid kama wanafika). Tuseme wamekwiba nusu, wameleta nusu na sasa tuseme wanakusanya Trillion 14 na kisha Bajeti yetu ipande kutoka kutoka Trillio 18 hadi Trillion 30! Hata hivyo, ni bado sana katika kuwa na uchumi bora.
...mapato yetu si madogo. na bado kuna uwanja wa kuyaongeza.

...kuna tatizo kwenye matumizi. don't ask me for details, zinaonekana wazi. nilikutolea mfano wa halmashauri zetu.
 
Pamoja na Utanzania wangu na kuipenda sana nchi yangu nakubaliana sana na ile "Coalition of the Willing" (CoW) ya Kenya, Uganda na Rwanda hata kama walikiuka taratibu za EAC lakini wako fast wanapopanga mipango yao. Hivi majuzi tu wameongelea reli ya kisasa itakayounganisha nchi zao, jana tumeona uzinduzi ukifanywa pale Mombasa na Rais Uhuru Kenyatta, sisi tatizo kila kitu siasa tu, maneno mengi ya kuwapa matumaini wananchi kwenye majukwaa na kutaka kupigiwa makofi na kulazimisha kuonyesha kwamba chama tawala kinafanya jitihada kubwa sana kuleta maendeleo lakini utekelezaji hakuna na kama utakuwepo basi utachukua miaka mingi sana ijayo. Kwa serikali isipange mipango yake kimya kimya na muiweke hadharani pale inapofikia utekelazaji?
 
Back
Top Bottom