Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Hapa ndipo magamba huwa wananiacha hoi. Mtu anakataliwa kuwakilisha jimbo yaani anashindwa kwenye uchaguzi kisha anateuliwa kuwakilisha nchi. Shame on magamba

So what? Kwani ukishindwa jimbo moja ndiyo umeshindwa nchi nzima? Mbona yeye JK alishindwa urais na akapewa uwaziri na Mkapa?

Hayo mengine munapenda kulalamika hata kama hakuna msingi wo wote.
 
Ama kweli JK ni bonge la kilaza! Yaani watu ambao wameshindwa kukubalika na watu wao je nje watakubalika? Je watejenga mahusiano bora au watajenga mianya ya rushwa kwenye balozi zetu?

Kilaza wewe hapo usiyejua tafauti baina ya kushindwa kwenye jimbo na uteuzi wa ubalozi.

Rushwa hata wewe unachukua hapo kazini hata kama siyo directly. Ukienda kazini halafu usifanye kazi kwa masaa yapasayo yale malipo ya bure ni rushwa.
 
watu wale wale,cjui kama kuna mpya hapo, kwani wengi walikuwa nje ya system kwa muda na cha moto wamekiona mfano ni Dr.Kamala aliyekuwa anashinda pale Moro,nje ya nyumba ya kulala wageni inaitwa VANILA.je wataanza wataanza na lipi kuwakilisha au kutafuta posho?Kwani wengi walipigwa chini ubunge ambao kama sijakosea uliwaumiza kipesa na kimwili
 
Kwa upande mwingine unaweza ukamkufuru Mungu na kujuta kuwa mtanzania chini ya kiongozi Ki laaza kama JK
 
Hivi hizi pesa za kuhamishana kama nzige wanazipata wapi? Kila siku mara kateua wakuu wa mikoa wilaya tarafa kata vijiji balozi nyumba kumi kumi n.k kweli usiamshe waliolala naona bongo tumelazwa usingizi na usingizi wenyewe ni pono.
 
Kwa CCM huwa hakuna makapi, pamba ikichambuliwa mbegu zinakamuliwa mafuta mashudu yanakuwa chakula cha ng'ombe, ng'ombe akinya mavi yanakuwa mbolea and recycle goes on...

hahahahaaa hii nimeipenda
 
- Ndio maana tunasema tunahitaji katiba mpya makini maana tukiweza kuwa nayo hawa walioteuliwa wangetakiwa kupitia kamati ya Bunge kupitishwa, Wallahi tena wanaofaa hapo ni wawili tu, Mujuma na Shamin, wengine wote ni makatibu kata tu, I mean bongo bwana yaani bora liende tu!

- People the Word here ni Katiba Mpya!


William @..NYC,USA:

Badala ya kuteua balozi aliyebobea ktk masuhala ya uchumi na biashara za kimataifa atuwakilishe China,anapelekwa kada wa CCM Marmo! Kama ningepewa majina ya hawa wateule kama yalivyo,nikaulizwa nipendekeze nani awe balozi wetu Kenya,ningempendekeza Kamala.
 
Jk ameteua mabalozi wapya,ninayekumbuka vizuri ni philip marmo,anakwenda china. Mwenye habari nzima atumwagie. Source, tbc.
 
Jk ameteua mabalozi wapya,ninayekumbuka vizuri ni philip marmo,anakwenda china. Mwenye habari nzima atumwagie. Source, tbc.
Wacha kukurupuka ipo humu thread yenye orodha ya wateule wote wa nafasi za Ubalozi.
Ushauri: muwe mnasoma kwanza humu jukwaani kabla kukimbilia kupost thread ushuzi.
 
Jk ameteua mabalozi wapya,ninayekumbuka vizuri ni philip marmo,anakwenda china. Mwenye habari nzima atumwagie. Source, tbc.
Habari gani tena wakumwagie wakati mwenyewe umesema anakwenda china au unataka wakuambie anakwenda na mabegi matano ya nguo.
 
Hawa ndio mabalozi vijana aliokuwa akisema Membe
 
I hate to say this in public lakini it was not on our

1. NATIONAL INTEREST

2. PUBLIC INTEREST

3. COMMERCIAL INTEREST

4. FUTURE INTEREST

kumpeleka this OLD GUARD China. Are we really serious about cultivating our relationship with the this superpower or not?

Membe anahusika kwenye hili kwani JK kabla haja go public na hili lazima alipewa ushauri na waziri wake wa Mambo ya Nje kama huyu mtu anafaa kupelekwa China au la.

In short ni kuwa kuna uwezekano Mheshimiwa membe alisahau kumwambia JK kuwa China is THE great economic success story of the past 30 years. Na imeweza kuondoka kwenye umaskini watu zaidi ya milioni 600 toka kwenye umaskini na hawakufanya kwa kuwa na "OLD DINOSAURS" mithili ya Philip Marmo ambao hawana kipya kimawazo na kiakili


Wana JF ambao mshafika Guangzhou nadhani you all know well wa China walivyo wekeza kwenye manufacturing: Maybe Membe should have mentioned kama vile:


1. China is the largest global producer of toys, textiles, washing machines, cameras and computers (among hundreds of other products).

2. It is also the world’s largest consumer of iron, steel, coal and cement, and China’s hunger for raw materials continues. Over a million enterprises have flourished, and nearly 40 Chinese companies have entered the global Fortune 500 list.


3. Je Kwa nini hawakufikiria kufungua balozi ndogo Guanzshou, Shanghai au Hongkong?

4. Je Philip Marmo anazungumza Cantonese au Mandarin?

5. Je Marmo ameshakwenda China mara ngapi na ame cultivate business ngapi kule na zina net worth how much kwa Taifa?



Either way looks like decision makers wetu ambao wengi wao ni BABYBOOMERS na wako OUT OF TOUCH with 70% of the population (ambao ni under 30) kuwa hizi si zama za GEO POLITICS bali ni zama za GEO ECONOMICS and the old guards za akina Marmo & Co itakuwa ndio wale wale ambao watakaa pale Beijing na kazi kupokea wanasiasa badala ya ku broker major deals

Ushauri wa bure kwa mlio foreign. Nashauri muanze kuangalia Plan B kwani these old men are not ready to lleave anytime soon. Nashauri muangalie options zenu kwenye private sector na sio kukaa hapo mnaandika ma papers tuuu.

This is a sad day kwa kila kijana mwenye mwamko foreign lakini nawashauri uzalendo wenu ubaki pale pale japo si vibaya kuangalia options zilizopo
 
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kuwa, muda mfupi kuanzia sasa, kutakuwa na mabalozi vijana ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani, baada ya waliokuwapo kustaafu. Membe alitoa kauli hiyo, alipokuwa anagawa vyeti kwa maofisa wa wizara yake wanaofanya kazi hapa nchini na kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi, baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki tatu waliyoyapata katika Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.

Alisema kuanzia mwaka ujao kuna mabalozi mbalimbali wanaotarajiwa kustaafu, hivyo nafasi zao zitachukuliwa na maofisa vijana wanaofanya kazi ubalozini kwa kuwa wanazo sifa zinazotakiwa. Aliongeza kuwa mafunzo hayo ya wiki tatu waliyoyapata watumishi hao wa wizara yake, ni ya promosheni ya kuwatoa hapo walipo na kuwapandisha daraja jingine. Pia alisema mafunzo hayo yaliyotolewa ni muhimu kwa kuwa yanawawezesha wanadiplomasia hao kuielewa nchi yao na mambo yanayoendelea ulimwenguni hivi sasa.

Membe: Tutachagua mabalozi vijana
 
Back
Top Bottom