Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kuwa, muda mfupi kuanzia sasa, kutakuwa na mabalozi vijana ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani, baada ya waliokuwapo kustaafu. Membe alitoa kauli hiyo, alipokuwa anagawa vyeti kwa maofisa wa wizara yake wanaofanya kazi hapa nchini na kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi, baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki tatu waliyoyapata katika Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.
Alisema kuanzia mwaka ujao kuna mabalozi mbalimbali wanaotarajiwa kustaafu, hivyo nafasi zao zitachukuliwa na maofisa vijana wanaofanya kazi ubalozini kwa kuwa wanazo sifa zinazotakiwa. Aliongeza kuwa mafunzo hayo ya wiki tatu waliyoyapata watumishi hao wa wizara yake, ni ya promosheni ya kuwatoa hapo walipo na kuwapandisha daraja jingine. Pia alisema mafunzo hayo yaliyotolewa ni muhimu kwa kuwa yanawawezesha wanadiplomasia hao kuielewa nchi yao na mambo yanayoendelea ulimwenguni hivi sasa.
Naye Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dk. Mohamed Maundi, alisema kuwa madhumuni ya kozi hiyo iliyotolewa kwa maofisa hao ni kuwapatia njia mpya ya kuelewa shughuli zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ndani na nje ya nchi. Alisema kwa kuwa wengi wao wapo nje ya nchi, mafunzo hayo yatawasaidia kuwapatia mbinu mpya ya kuboresha masuala ya kidiplomasia.
Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi aliyeko nchini Uingereza, Amosi Msanjila, aliipongeza wizara yake na chuo hicho kwa kuwapatia mafunzo hayo, kwa kuwa hivi sasa wanastahili kupandishwa daraja kutoka hapo walipokuwa. "Kwa miaka 16 iliyopita mafunzo haya yalikuwa hayatolewi, hivyo kwa upande mwingine watu waliweza kupanda vyeo bila kupitia kozi hizi," alisema Msanjila.
Alisema wahitimu wote walipata fursa ya kuzungumza na watu kwenye taasisi mbalimbali ili kujua changamoto zilizoko kwenye maeneo muhimu ambazo Watanzania ama raia wa nchi nyingine wanazipata wanapotaka kuja Tanzania ama kwenda katika nchi nyingine.
Membe: Tutachagua mabalozi vijana
nakumbuka niliposema kuhusu membe nikaambiwa niliomba kazi foreign na kunyimwa
basically waziri membe alitoa kauli ya uwongo hapo na ukweli umejidhiri tofauri na ahadi alizozitoa
lakini inaonekana they dont really care much about China
I really feel sorry for young turks waliopo foreign. Sasa ngoja nikatembelee ile thread ya Foreign...nataka nione average age ya head of department na staff wao na achievements zao ni nini
halafu mnasangaa kwa nini Ikulu hawati kuwa na website....!