Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Mkuu Hebu tuwekee hapa japo Mafanikio katika nafasi walizokuwanazo kabla ya Uteuzi na ni nini wameifanyia Tanzania hao unaowaita Seasoned Diplomatics waliobobea.
 
- Mh. JK anastahili pongezi sana kwa uteuzi wa hawa Mabalozi wawili, Le Mutuz Big Show ninakubali kwamba huu ulikuwa ni uteuzi makini sana. Hawa wawili ni Seasoned Diplomats waliobobea sana na pia inatia moyo kwa maofisa wengine huko foreign kwamba hard work pays.

- HOWEVER: I have a big problem na uteuzi wa Balozi mpya China, I mean kweli kwenye Super Economy tunapeleka Old Guard ambaye hana record yoyote on Economy yetu hapa Tanzania? Wala hata jimboni kwake?

- I mean ishu kama hizi ndio hasa the case ya why tunahitaji kuwa makini na Katiba mpya on Checks and Balance to the Executive Powers.

William @..NYC,USA: Mutuz Big Show!


Mwaha hapo ktk uteuzi wa barozi huyu hapa china kweli ni tatizo na sijui ni nani anaemshauri Raisi ktk michakato kama hii,kwani kuna haja ya kulindana hata ktk nafasi nyeti kama hizi,nchi kama uchina ilihitaji Balozi mwenye uwezo mkubwa ktk issue za kiuchumi,labda Raisi hakuona umuhimu huo tunaouona sisi,

tunapongeza kwa wale wachapakazi waliopata nafasi hizi lakini bado tutaendelea kulaumu kama nafasi hizi zitakuwa ni za kulindani kila wakati

jamani tusione vyaelea,vimeundwa(namaanisha ktk hili)
 
Mwaha hapo ktk uteuzi wa barozi huyu hapa china kweli ni tatizo na sijui ni nani anaemshauri Raisi ktk michakato kama hii,kwani kuna haja ya kulindana hata ktk nafasi nyeti kama hizi,nchi kama uchina ilihitaji Balozi mwenye uwezo mkubwa ktk issue za kiuchumi,labda Raisi hakuona umuhimu huo tunaouona sisi,

tunapongeza kwa wale wachapakazi waliopata nafasi hizi lakini bado tutaendelea kulaumu kama nafasi hizi zitakuwa ni za kulindani kila wakati

jamani tusione vyaelea,vimeundwa(namaanisha ktk hili)
Balozi hahusiani na mambo ya kiuchumi, hayo yalikuwa ya kizamani. Acheni kusisitiza mambo ambayo haya make real sense in real life....
Thats too obsolete.
 
Soby kabla Balozi hajaenda wenyeji hudai CV yake kwanza na ni hapo na wao huamua kama tupo serious as a Nation! - William
 
Kivumah na wewe nenda ucheck web ya Foreign utaona vitu vyao yaani Super tupu, ila sina clue na Mzee wa China! - William
 
Kuna vitu vingine vigumu kueleweka. Umemteua Batilda awe mbunge, ukampa uwaziri. Akawatumikia wananchi kisha akaona asogee

karibu nao kwa kugombea ubunge wa kuchaguliwa. Wakamkataa. Kwa kura nyingi. Wakimaanisha hatukuona kazi zake akiwa waziri.

Raisi anaona haitoshi. Anamteua Balozi. Maana yake nini? MIMI RAISI NAKUHITAJI SANA NA NAKUONA UNAFAA KULIKO WANANCHI

WALIOKUKATAA.
 
Soby kabla Balozi hajaenda wenyeji hudai CV yake kwanza na ni hapo na wao huamua kama tupo serious as a Nation! - William
Just a formality, a protocol thing..... most of them are retired top spies na kabla nchi yeyote haijakupa diplomatic immunity, lazima wajue wewe uko vipi. Hata ukitaka kusafiri nje mataifa mengine hukucheck out.

Siku hizi kuna PR companies ambazo zipo chini ya lobbyists wa US, EU, China, Japan.. etc na ukitaka connections za kuonana na Obama, sarkozy, Merkel, Hu Juntao etc, unawalipa half a million halafu unasukiwa connection.

Hawa mabalozi hawan sana maana siku hizi, wala msilikuze hili, ni fadhila tu.
 
kiukweli hata mimi nimeshangazwa sana,kwani tunapeana vyeo kwa kuangaliana usoni na wala sio uwezo wa mtu husika? hivi kweli Marmo ataweza kututoa hapa tulipo na kutupeleka pale? nadhani hawajamaa wanakuja china kibiashara zaidi na sio kulisaidia Taifa hii inashangaza sana

ok,ngoja tusubiri tuone

Mkuu siyo kibiashara bali ni kichama.
 
Ndiyo maana wanasema rais ana mamlaka makubwa mtu amekataliwa
anapewa tena kazi ya ubalozi hivi hakuna wenye sifa kuliko hawoo??????????????
 
mkuu wala hana roho mbaya,kama ulianguka kwenye kura za maoni ndani ya chama kabla ya uchaguzi mkuu,na kama ulipita kwenye kura za maoni na ukaangukia pua hawezi kukutosa..nafasi za kula ziko kibao ukuu wa wilaya,mkoa na sasa ubalozii,eeee kweli this z tz
 
Ndiyo maana wanasema rais ana mamlaka makubwa mtu amekataliwa
anapewa tena kazi ya ubalozi hivi hakuna wenye sifa kuliko hawoo??????????????
Ubalozi ni kazi ya kwenda kupumzika tu! Mpaka sasa hizo nafasi hazina impact yoyote kwenye uchumi wetu.William hata tumpeleke Magufuli hatuoni faida ya balozi zetu na kibaya zaidi wanashindwa kuhandle hata usalama wa raia wetu waliohuko nje! Uchumi ndio kabisaaa wakijitahidi sana ni makongamano ya kupiga porojo tu!! Naomba Willy unisaidie jina la balozi yeyote ambaye kwa juhudi zake amefanikisha jambo linalooneka huku Tanzania!! nothing! ma secretary tu kwenye balozi zetu nyingi ni Miungu watu,hao Mabalozi ndio kabisaaa tabu tupu!
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Saturday, 17 December 2011 07:58[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
WAPANGIWA CHINA, UBELGIJI NA KENYA, WALIKOSA UBUNGE 2010

RAIS Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wapya wanane wakiwamo walikouwa mawaziri katika Serikali yake ya Awamu ya kwanza na kuwapangia vituo vyao vya kazi.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo jana, uteuzi huo ulianza rasmi Oktoba 12, mwaka huu na wataapishwa keshokutwa.

Walioteuliwa ni Phillip Marmo kuwa balozi nchini China, awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge. Marmo alianguka katika uchaguzi wa Jimbo la Mbulu ambalo lilichukuliwa na mgombea wa Chadema, Mustafa Akunaay,.
Kwa upande wake, Dk Deodorus Kamala ambaye awali alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki amepangiwa kuwa balozi nchini Ubelgiji. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Dk Kamala aliangushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chake, CCM

Wengine ni Dk Batilda S. Burian ameteuliwa kuwa Balozi nchini Kenya ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Katika uchaguzi wa mwaka jana, Dk Batilda aliangushwa na mgombea wa Chadema , Godbles Lema katika Jimbo la Arusha Mjini. Dk Ladislaus Komba ambaye ameteuliwa kuwa balozi nchini Uganda. Kabla ya hapo Dk Komba alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wenigne ni Shamim Nyanduga, anakwenda Msumbiji na kabla ya hapo alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Grace Mujuma ameteuliwa kuwa balozi nchini Zambia na kabla ya hapo alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Pia Rais Kikwete amemteua Mohamed Hamza kuwa balozi nchini Misri ambaye kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Zanzibar katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ali A. Saleheh ambaye alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) Dubai anakwenda nchini Oman.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Ona hii: Wengine wamekataliwa na wananchi wasiwawakilishe kwenye majimbo yao; lakini sasa wataiwakilisha nchi nzima uko ughaibuni!
 
Back
Top Bottom