Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

- Mh. JK anastahili pongezi sana kwa uteuzi wa hawa Mabalozi wawili, Le Mutuz Big Show ninakubali kwamba huu ulikuwa ni uteuzi makini sana. Hawa wawili ni Seasoned Diplomats waliobobea sana na pia inatia moyo kwa maofisa wengine huko foreign kwamba hard work pays.

- HOWEVER: I have a big problem na uteuzi wa Balozi mpya China, I mean kweli kwenye Super Economy tunapeleka Old Guard ambaye hana record yoyote on Economy yetu hapa Tanzania? Wala hata jimboni kwake?

- I mean ishu kama hizi ndio hasa the case ya why tunahitaji kuwa makini na Katiba mpya on Checks and Balance to the Executive Powers.

William @..NYC,USA: Mutuz Big Show!

Simple question?kwanini unasifia kuteuliwa kwa hao uliowataja bila kusema wasifu au uhodri wao uliokupelekea kuwasifia..angali unaowaponda una mention kuwa hawana record ya uchumi..hao wako wana record gani kwa uchumi wetu unaoyumba kila siku?au ndio hivyo wkiteuliwa rafiki au ndugu zako sawa..wasio wako ahh a ni makosa..
 
Urafiki,uswahiba,uhawara,ukada ndivyo vimeimaliza nchi na kuivuruga kabisa hasa kwenye awamu hii ya nne,kama kipimo cha uchapa kazi kwa manufaa ya wananchi ni wananchi wenyewe,na wananchi hao waliona hawafai hata kidogo leo unakuja wakota okota na kuanza kugawa ukuu wa mikioa,u-DC,na leo umeibuka na kugawa ubalozi,sasa najiuliza ni vigezo gani vinatumika?kama walio wengi wamewakataa kuwaongoza leo huko wanaenda kumwakilisha nani?to be honest ni JEY KEI.ila ingelikuwa vema kama angewalipa hela za mfukoni mwake na sio kodi za wanananchi.
  1. USWAHIBA
  2. URAFIKI
  3. U-HAWARA
  4. UKADA
HIVI VITU NI HATARI SANA KATIKA UTAWALA NA UONGOZI POPOTE,NA HII IMEPELEKEA KUSHINDWA HATA KUSHUGHULIKIA MAKOSA MAKUBWA YA UFISADI.HAYA BWANA !
 
Hapa hatubezi watu bali ni ile hali ya wazi ya ushikaji,ukada na mengineyo nimeshayataja,na hali hii imejitokeza kuanzia u-DC,ukuu wa mikoa na leo ubalozi kama huu,je hakuna watu wengine wenye uwezo wa kufanya kazi na ikaleta tija?maana hawa waliokuwa mawaziri hatukuona cha ajabu walichofanya,hatukuona creativity kwenye wizara zao,hatukuona kujituma kwao na hata kuonyesha badiliko katika wizara walizo kuwa wanaziongoza.
 
Watu ambao wananchi wamewaona wababaishaji, yeye ndo anawakumbatia, hii maana yake ni kama kawaona wananchi wajinga kwa kutataa kuongozwa na viongozi hawa.
 
UUUUHH!
hivi jamani kama mtu alikataliwa na wananci wa jimbo moja tu kuwawakilisha,
wewe leo unakuja vipi kumteua awakilishe nchi nzima......??
hvi mu anajiteteaje kua huu sio ujinga.. au basi kuchezea akili za watanzania??
unajua ni kweli mtu anashika mamlaka, lakin ni vyme kukumbuka amaekabidhiwa
na wat na wanaweza kuzinyakua siku wakitaka.
me naona hadi aibu kwa kweli..........!
 
Vitu kama hivi hunifanya nijiulize, hiivi mwananchi/wananchi tuna
nafasi gani katika kutaa mambo kama haya?
sisi ndio tunaowakiishwa, sasa hatutai kuwakilishwa na hao aliowateuwa.
tunakataa vip??
namwonea aibu baba idhi..............
kweli mswahili mswahilitu. kuna siku atacheza taarabu.
 
....Taarifa za muda mfupi ulipita ni kuwa Jk kateua mabalozi wa kutuwakilisha na wakimwemo B.Buriani aliyepigwa chini na Lema na Philip Marmo.....

Kwani kesi yake na Lema imeisha hadi awe balozi? au ndio imeisha kiaina hivyo??????????
 
jk akikujua kulala njaa hakuna tena wapi Lau Masha jamani

Haahaa🙂 kujuana naye ina maana kama ndoa nzuri-kukulinda na kukusaidia katika shida na raha....Hadi kifo kiwatenganishe🙂
 
Kwa kweli kwa hili Kikwete ameonekana hana akili kabisa. Tuko watanzania zaidi ya 40mil. Watu hao aliowateua wengine wamekaa serikalini wanakula kodi ya wananchi zaidi ya miaka 30 bado anaendelea kuwapa maisha mazuri tu wakati wako wasomi wazuri na ambao hata ajira hawana, kwa nini asiwagawie na wao wakaonja mema ya nchi hii? Marmo wa nini China? Batilda wa nini? Kamara wa nini? Kikwete kuna siku atajutia siku aliyozaliwa kwa uteuzi wa ovyo ovyo anaofanya. Kulipa fadhila siyo kwa jinsi hii. Laiti angejua ni chuki kiaisi gani anatengeneza ndani ya akili na mioyo ya watu. Nani asiyetaka familia yake iishi vizuri? Nani asiyetaka fedha? Kikwete nchi haiendeshwi hivi, najua katiba mnayong'ang'ania ndiyo inayokupa kiburi. Iko siku hutakuwepo madarakani na katiba itabadilishwa, tutakutafuta
 
hii inakatisha tamaa sana serikali legelege hii. hii mijitu yoote ilikataliwa na wananchi leo hii ndo wawakilishi wetu huko nje inatia kinyaaaa ptuuuuuuu! upuuzi wa mwaka huu
 
Tusilie. Tumnyang'anye haya madaraka kwenye katiba mpya! Tueleze namna ya kuwapata wafanyakazi hawa badala ya kupeana kiswahiba!
 
Jairo atateuliwa kuwa Balozi nchini Italia... ha, haT ngojeni nicheke! Tanzania hii! Mungu tu anajua hatima yake.
 
Mpe rais wetu heshima yake bwana mambo ya kumuita rais wetu kilaza sio heshima. Big up JK watu watakukumbuka sana ukitoka madarakani. Go go JK gooo............
 
Lau Masha katengewa nafasi ipi jamani! Nilidhani angekuwa balozi wetu Washington au UN.
 
Naupongeza uteuzi wa Mabalozi wapya uliofanywa na Rais Kikwete na kira gazes TBC1 hivi punde.

--------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-

i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

ii) Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

iii) Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

iv) Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

v) Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

vi) Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

vii) Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

viii) Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.

2. Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.

Mhhh jamani this is too much now. Hivi hakuna watu wengine wenye uwezo wa kushika nafasi hizo isipokuwa hao akina Marmo, Burian na akina Kamala?? Watu ambao wananchi waliwakaa katika uchaguzi, leo ndio wanapewa nafasi za kidiplomasia??? Ni lini hawa jamaa kweli wamejifunza masuala ya diplomasia???? Ndio maana akina sie tunasema KATIBA MPYAA IJE ILI TUWEKE WAZI MASUALA KAMA HAYA ya kufanya "RECYCLING" ya watu katika nafasi za uongozi as if hakuna wengine wenye uwezo wa kufanya kazi kwa nguvu, ari na kasi mpyaa zaidi.
 
Back
Top Bottom