Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo

Chipsi yaipembeni

Senior Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
128
Reaction score
92
Rais Jakaya Kikwete, Alhamis Wiki Hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florence Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.

Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

“Pamoja na Bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano,” alisema Dk. Turuka.

Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

Kwa mujibu wa Dk. Turuka, wazo la kuwepo mradi huo limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.

Kuanzishwa kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008 wakati Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.

Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Sheikh Abdullah Al Saadi.

Ujumbe kutoka China utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
 
Utakuwa wa maana kama tutakuwa wasemaji kwenye huo mradi ila ikiwa ni kuwapa mbwa chakula cha watoto,nkimaanisha ile mikataba ya miaka 100 bila kulipa kodi.
 
safiiii sanaaaaa! Kikwete asinge hujumiwa na alio wa amini, nchi hii ingepiga hatua sana katika miaka yake 10 ya utawala.

hata hivyo nina msifu hii kasi ya staili yake ya umaliziaji kipindi chake cha utawala.
 
Mimi nilifikiri ndio anakwenda kuzindua bandari, kwamba iko tayari imeshajengwa. Kumbe ni siasa za kwenda kuzindua vitu vya kufikirika!! vinavyotarajiwa kuja.

Hizo ndio cheap politics.
 
Nina hakika yeyeto kati ya Pombe na Ngoyai mmoja wao atakua rais wa Bongo, mradi huo hautaendelezwa. Wataalamu wengi na hata wasafirishaji wa meli walipinga mradi huo so sidhani kama utaendelea. JK mwenyewe kabakiza wiki 2 tu za kukaa Ikulu. Ghrama hizo zingeelekezwa bandari za Tanga na Mtwara hayo yote yanayosemwa kwamba eti ni faida basi huko hizo faida zinge double.
 
True!. Kwanza waweke wazi mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo wananchi tuone kama unamaslahi. Dola bl 10 ni zaidi ya trillion 20 tshs. Hizo ni fedha nyingi sana ukizingatia deni la taifa ni trillioni 40.
 
Nina hakika yeyeto kati ya Pombe na Ngoyai mmoja wao atakua rais wa Bongo, mradi huo hautaendelezwa. Wataalamu wengi na hata wasafirishaji wa meli walipinga mradi huo so sidhani kama utaendelea. JK mwenyewe kabakiza wiki 2 tu za kukaa Ikulu. Ghrama hizo zingeelekezwa bandari za Tanga na Mtwara hayo yote yanayosemwa kwamba eti ni faida basi huko hizo faida zinge double.

Kweli kabisa mkuu..tanga na mtwara kuna kina kirefu cha baharini hivyo meli kubwa zaweza Tia nanga apo...kuhusu viwanda..tanga kuna zaidi ya viwanda 100 alivyojenga nyerere vilivyokufa..hvyo ujenzi wa hiyo bandari ungevifufua viwanda vyote hvyo.
 
Kwa hili naunga mkono 200%, kwanza huu mradi umechelewa, ulitakiwa uwe tayari, jamani ndugu zangu watanzania huu mradi ni mzuri, let's support.
 
Hivi hii bandari si ndio ile wataalamu walishauri isijengwe kwani itaendeshwa kwa hasara badala yake ufanyike upanuzi wa bandari ya Kurasini?
 
Rais Jakaya Kikwete, Alhamis Wiki Hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florence Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.

Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

“Pamoja na Bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano,” alisema Dk. Turuka.

Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

Kwa mujibu wa Dk. Turuka, wazo la kuwepo mradi huo limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.

Kuanzishwa kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008 wakati Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.

Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Sheikh Abdullah Al Saadi.

Ujumbe kutoka China utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.

Hizi ni siasa tu,kisa katoka bagamoyo anasema atawafanyia nini wana bagamoyo.kulikua hakuna haja ya kitumia pesa mingi hivo wakati ingetumika nusu ya hiyo pesa kuongeza berths bandari ya dar na kuwekeza katika mashine na sio porojo eti bandari mpya.
 
Sioni umuhimu WA bandari hii kabisa!!
-->>Endapo tu,tunashindwa kutumia bandari zilizopo
#MTWARA
#TANGA
#DAR ES SALAAM
KIKAMILIFU WHY NEW PROJECT?
JE HII NI HEKIMA?
**nadhani fedha hizi zingetosha mno ktk kumaliza tatizo LA;-
#AFYA
#UMEME
#MAJI SAFI
#
 
Kwa hili naunga mkono 200%, kwanza huu mradi umechelewa, ulitakiwa uwe tayari, jamani ndugu zangu watanzania huu mradi ni mzuri, let's support.

Let's support maana yake ni nini hatuwezi Ku support madudu Tanga na Mtwara zinaitaji hizo pesa hakuna sababu ya kuanzisha kitu kipya wakati tuna vile vinavyoitaji kuboleshwa na kukudhi mahitaji yetu.Maisha ya kufanya vitu kusudi uache nyumbani wananikumbuka ni vunjaji wa Mali za umma. Ukweli Bagamoyo hatukuitaji bandari kwa sasa.
 
Sioni umuhimu WA bandari hii kabisa!!
-->>Endapo tu,tunashindwa kutumia bandari zilizopo
#MTWARA
#TANGA
#DAR ES SALAAM
KIKAMILIFU WHY NEW PROJECT?
JE HII NI HEKIMA?
**nadhani fedha hizi zingetosha mno ktk kumaliza tatizo LA;-
#AFYA
#UMEME
#MAJI SAFI
#
 
Let's support maana yake ni nini hatuwezi Ku support madudu Tanga na Mtwara zinaitaji hizo pesa hakuna sababu ya kuanzisha kitu kipya wakati tuna vile vinavyoitaji kuboleshwa na kukudhi mahitaji yetu.Maisha ya kufanya vitu kusudi uache nyumbani wananikumbuka ni vunjaji wa Mali za umma. Ukweli Bagamoyo hatukuitaji bandari kwa sasa.

Bagamoyo tuliitaji mahoteli ya kitalii, kama bandari itajengwa kweli tujiandae na kazi ya kuwa tunajimba mchanga kuongeza kina kila baada ya miaka 10.
 
Mmeshindwa kuboresha Bandari za Mtwara na Tanga, mmeshindwa kupata suluhisho la matatizo ya umeme, mmeshindwa kuwapatia maji safi na salama wananchi, hspitali hazina dawa wala vifaa tiba, madai ya walimu na wafanyakazi wengine wa umma mmeshindwa kutatekeleza, mifuko ya penseni inawadai kiasi kikubwa cha fedha, sasa mnakimbilia mradi wa mamilioni wa bandai ya Bwagamoyo. Kweli hamuishi vituko.
 
Sioni umuhimu WA bandari hii kabisa!!
-->>Endapo tu,tunashindwa kutumia bandari zilizopo
#MTWARA
#TANGA
#DAR ES SALAAM
KIKAMILIFU WHY NEW PROJECT?
JE HII NI HEKIMA?
**nadhani fedha hizi zingetosha mno ktk kumaliza tatizo LA;-
#AFYA
#UMEME
#MAJI SAFI
#
 
Sioni umuhimu WA bandari hii kabisa!!
-->>Endapo tu,tunashindwa kutumia bandari zilizopo
#MTWARA
#TANGA
#DAR ES SALAAM
KIKAMILIFU WHY NEW PROJECT?
JE HII NI HEKIMA?
**nadhani fedha hizi zingetosha mno ktk kumaliza tatizo LA;-
#AFYA
#UMEME
#MAJI SAFI
#
Yaani umesema 7kweli mtupu naomba raisi ajae aweze ku- voke huko mradi hauna faida kwa sasa hizo pesa zitatuwe matatizo mingine kama ulivyo mention hapo huu. Kama tunajengewa bure sawa lakini kama ni mkopo tafadhali tutumie hizo pesa kwa shughuli nyingine ya maana zaidi kama vile Maji salama, madawati ya shule zetu na mahabara, pia afya.
 
Back
Top Bottom