Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo

Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo

Kwa hili naunga mkono 200%, kwanza huu mradi umechelewa, ulitakiwa uwe tayari, jamani ndugu zangu watanzania huu mradi ni mzuri, let's support.

Hakuna kitu kama icho. Izo ni siasa za kutaka kuomba kura tu.hamna mradi hapo kwani ni muda umepita toka watiliane saini.izo ni maigizo ya ccm bado yanaendelea
 
Hivi ile meli ya MV Dar es Salaam iliyozinduliwa kwa mbwembwe na JPM ikitumia masaa 3 Magogoni mpaka Bagamoyo ipo wapi?.Hivi kwa nini tunaishia kuzindua vitu ambavyo tunashindwa kuvisimamia?
 
Utata mtupu.Hivi why this port at all.Repurcussions zake ni nyingi mno.
1.Kuua bandari ya Dar.which for me is too close.
2.Kuongeza bei ya bidhaa
3.Matumizi mabaya ya resources.Money for the port would be better spent in other development projects for the wananchi.Dar. Port inatosha.
4.Bagamoyo hakuna amenities za ku-support such a big port kwa muda huu.
5.Kushusha hadhi ya serikali kwa wananchi kwa kuwa this is seen as improper use of resources.Wananchi wengi wanaona kwamba there is a hidden agenda in building this port.
Rais Jakaya Kikwete, Alhamis Wiki Hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florence Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.

Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

“Pamoja na Bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano,” alisema Dk. Turuka.

Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

Kwa mujibu wa Dk. Turuka, wazo la kuwepo mradi huo limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.

Kuanzishwa kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008 wakati Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.

Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Sheikh Abdullah Al Saadi.

Ujumbe kutoka China utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
 
Huu mradi ndugu zangu una manufaa makubwa sana, bandari inayojengwa ni ya kisasa, largest port in AFRICA, na itakuwa na miundo mbinu ya kisasa hivyo itaongeza kasi ya maendeleo. Bandari zingine zote kama mtwara na Tanga pia zinaboreshwa. Jamani, bandari tu inaweza kuondoa umasikini Tanzania, tukiachia hayo madini, gesi, nk. Tunahitaji bandari ya kisasa, bandari ya Dar ni ndogo pia ipo mjini sana, hivyo kushindwa kwa meli kubwa kutua pale. Ndg zangu hii bandari nchi jirani baada ya kuona tumepata walifunga safari kwenda china to stop this so as can not happen to TZ na wakaomba ijengwe kwao, kwa bahati nzuri uhusiaono wa Tanzania na china ni mzuri and they were told no, sasa jamani angalieni hizi siasa siasa zisitufanye tukose hii bahati, tuwe ni watu wa kufocus. Kipindi reli ya kati inajengwa Tanzania na china, kulikuwa na njaa sana china, lakini raisi wa nchi hiyo aliwaambia wananchi wa china kuwa pamoja na njaa tuliyonayo lakini reli ya kati tanzania lazima ijengwe, itakuwa ni ajabu sana kwa wanatanzania wasipokubali bandari ya bagamoyo, labda kama tunatumika na nchi jirani kuzima jitihada hizi, lakini kwa mzawa sounds not good. Mimi nakubali sana mabadiliko lakini kwa bandari hii pia naikubali, ni chachu ya maendeleo. Kuna kipindi watanzania inabidi tuungane tufight for our country.
Kenya Fights Off Port Competition With $13 Billion Plan: Freight - Bloomberg Business
 
Rais Jakaya Kikwete, Alhamis Wiki Hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florence Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.

Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

“Pamoja na Bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano,” alisema Dk. Turuka.

Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

Kwa mujibu wa Dk. Turuka, wazo la kuwepo mradi huo limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.

Kuanzishwa kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008 wakati Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.

Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Sheikh Abdullah Al Saadi.

Ujumbe kutoka China utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya
Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake
Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa
kugharimu dola za Marekani bilioni 10.

Afrika Mashariki Na Kati...Kuna Bandari gani Afrika ya Kati?
 
Hakuna kitu cha bure kutoka uchina. No free lunch. Hii ni mikopo na tutegemee kuumia sana kulipa kwa karne nzima
 
Hakuna kitu cha bure kutoka uchina. No free lunch. Hii ni mikopo na tutegemee kuumia sana kulipa kwa karne nzima

Mbaya zaidi unawakopa wao,kazi wanafanya wao hela inarudi kwao.Then unawalipa na interest ya kutosha.sisi tunabaki na vijisenti tulivopata kwa kukodisha malori ya mchanga.
 
Naanza kuelewa kwanini Pembe za ndovu ni china na Twiga na wanyama hai ni oman pamoja na vitalu kibao vya uwindaji ambavyo mifugo na binadamu ukiingia kwa bahati mbaya unapigwa risasi.!! One day ukombozi utapatikana!!!
 
Kukopa na kujenga Bandari kama hiyo sio mbaya, mbaya kopeni na kuiba pesa zote na mradi usitekelezeke, kwani hizo nchi za jirani wanajenga reli hadi uganda, hadi sudani wametoa pesa zao ? pia ni mkopo, mkopo utalipwa pole pole, suala la usimamizi na usafirishwaji wa twiga sijui na madawa ni vitu viwili tofauti, bandari ijengwe, sio kuwa tunakwenda tu Dubai kuangalia vitu kama hivyo then tunarudi Tanzania na kusema vitu vya nje, we need to be proud of our country. Banadari haina uhusiano na siasa na ccm wala chadema, haya ni maendeleo kwa wote.
 
mimi nilifikiri ndio anakwenda kuzindua bandari, kwamba iko tayari imeshajengwa...kumbe ni siasa za kwenda kuzindua vitu vya kufikirika!! vinavyotarajiwa kuja....

hizo ndio cheap politics.
Hukukosea mkuu.
 
Aksante !! Ccm mbele kwa mbele
Tukisema magufuli hamfikii kikwete hata nusu,mnatwambia tunaleta ubaguzi,Magufuli anatakiwa akasome Kwa mtoto wa mjini Mh Kikwete,personalty ya kikwete ni ya kimataifa.
 
Tukisema magufuli hamfikii kikwete hata nusu,mnatwambia tunaleta ubaguzi,Magufuli anatakiwa akasome Kwa mtoto wa mjini Mh Kikwete,personalty ya kikwete ni ya kimataifa.

Baada Ya miaka minane....nitakuhtaji urud hapa
 
Nina hakika yeyeto kati ya Pombe na Ngoyai mmoja wao atakua rais wa Bongo, mradi huo hautaendelezwa. Wataalamu wengi na hata wasafirishaji wa meli walipinga mradi huo so sidhani kama utaendelea. JK mwenyewe kabakiza wiki 2 tu za kukaa Ikulu. Ghrama hizo zingeelekezwa bandari za Tanga na Mtwara hayo yote yanayosemwa kwamba eti ni faida basi huko hizo faida zinge double.
Uliona mbaaali Sana mkuu
 
Mbagamoyo aisome hii thread
 
Back
Top Bottom