Kwa hili naunga mkono 200%, kwanza huu mradi umechelewa, ulitakiwa uwe tayari, jamani ndugu zangu watanzania huu mradi ni mzuri, let's support.
Rais Jakaya Kikwete, Alhamis Wiki Hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florence Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.
Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.
Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).
Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.
Pamoja na Bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano, alisema Dk. Turuka.
Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.
Kwa mujibu wa Dk. Turuka, wazo la kuwepo mradi huo limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.
Kuanzishwa kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008 wakati Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.
Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.
Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Sheikh Abdullah Al Saadi.
Ujumbe kutoka China utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.

Hakuna kitu cha bure kutoka uchina. No free lunch. Hii ni mikopo na tutegemee kuumia sana kulipa kwa karne nzima
Hukukosea mkuu.mimi nilifikiri ndio anakwenda kuzindua bandari, kwamba iko tayari imeshajengwa...kumbe ni siasa za kwenda kuzindua vitu vya kufikirika!! vinavyotarajiwa kuja....
hizo ndio cheap politics.
Tukisema magufuli hamfikii kikwete hata nusu,mnatwambia tunaleta ubaguzi,Magufuli anatakiwa akasome Kwa mtoto wa mjini Mh Kikwete,personalty ya kikwete ni ya kimataifa.Aksante !! Ccm mbele kwa mbele
Tukisema magufuli hamfikii kikwete hata nusu,mnatwambia tunaleta ubaguzi,Magufuli anatakiwa akasome Kwa mtoto wa mjini Mh Kikwete,personalty ya kikwete ni ya kimataifa.
Uliona mbaaali Sana mkuuNina hakika yeyeto kati ya Pombe na Ngoyai mmoja wao atakua rais wa Bongo, mradi huo hautaendelezwa. Wataalamu wengi na hata wasafirishaji wa meli walipinga mradi huo so sidhani kama utaendelea. JK mwenyewe kabakiza wiki 2 tu za kukaa Ikulu. Ghrama hizo zingeelekezwa bandari za Tanga na Mtwara hayo yote yanayosemwa kwamba eti ni faida basi huko hizo faida zinge double.
Mradi ni wa kisiasa.