Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Zakumi rejea tafsiri ya "luxury" hapo juu. Huu sio muda wa Rais ku-"indulge" watoto maskini wa Tanzania ambao kupata maji safi na salama ni ndoto, kusoma shule bora ni njozi, na kupata matibabu mazuri ni habari ya kufikirika na si ya kusadikika. Hiyo Watanzania tunaita 'danganya toto'. Utamu huo utamfanya mtoto huyo azubae na kupumbaa. Nasema hivi: Mpe zawadi itakayomhamasisha na kumchochea asirithi umaskini na uvivu wa kufikiri, kuhoji na kuvumbua ambao kizazi hiki kimeurithi.