Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Na wewe bana.....nani anataka kumuua Kikwete?

Siyo lazima iwe security concern in the sense ya mtu kumuua, kuna vitu kama ajali etc. Kwa nini watoto huwekwa nyuma? Hii inaonyesha utovu sio tu wa itifaki, bali pia wa kanuni za usalama.

On the pipi tip, hapo naona kamjazia pipi kiasi kwamba ma dentist wanaweza ku take issue with the president's awareness when it comes to dental hygiene and health issues.
 
Kaazi kweli kweli.

Maswali ya Mzazi kuulizwa RAIS? Kweli vichwa vinatofautiana.
 
JK ZILE PIPI ALIPEWA YEYE ALIVYOKUWA ANAFUNGUA HOTELI, LAKINI KWA SABABU ZA KIUSALAMA HAWEZI KUZILA ZILE PIPI LABDA WATU WAMEMTEGESHEA KITU.
NINACHOLAANI MIMI ZILE PIPI ANGETAKIWA KUZITUPA NA SIO KUZIFANYIA MAJARIBIO KWA KUMPA MTOTO.
KAMA HIZO PIPI ALIKUWA KATEGESHEWA YEYE INAMAANISHA YULE MTOTO NDIO ATAUMIA

YAANI HUYU KIKWETE AMESHINDWA KUFUNGUA MLANGO NA KUMPA MTOTO PIPI. ANAMPA KWA DIRISHANI KAMA NDEGE
ALAFU NDIO WANASEMA MTU WA WATU.
mtoto amekuja kukulaki, fungua mlango na wewe umuonyeshe mapendo
 
Dah! Hii scenario yako Companero akiiona lazima akununulie bia....si unamjua alivyo?

Aisee mimi mlokole, kileo mwiko. Hakika Scenario building ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Laiti tungejenga scenario ya nchi tuitakayo miaka 50 ijayo. Siku hizi scenario building zetu zinaangalia miaka 5 ijayo tu!

Scenario hiyo ilitakiwa iishie hivi ili ilete inspiration endelevu:

Soma kwa bidii. Shirikiana na wenzako. Gawana nao pipi. Huo ndio Ujamaa. Tutawaletea vitabu mashuleni. Walimu nao tutawaongezea. Madarasa bora tutawajengea. Tutahakikisha mnafika sekondari. Na chuo pia. Umeniambia unapenda sayansi. Tutawajengea maabara shuleni. Hakika utakuwa mwanasayansi. Na utaisadia Tanzania. Kazana utaweza tu!

Mtoto ataondoka na hamasa. Mwaka 2050 atavumbua Nadharia ya Kulima kwa Nyuklia. Hatimaye Tanzania bila njaa na umaskini itakuwa imewezekana.
 
Mambo mengine yanachekesha kwa kweli naona watu wanapoteza muda kujadili mambo yasiyo namsingi
...................................................

maana tunaacha kupigania mambo ya maana tunajadili pipi doh

Wewe mwenyewe hapo hujajadili pipi? Kati yako na sisi, sijui nani anaechekesha kwa kweli.

dah waTZ bado tupo nyuma yaani muda wote mnajadili pipi kha!

Na wewe pia, hujapenda majadiliano ya pipi, lakini hukuivuka thread ya pipi. Umevutiwa?
 
Goja tuchambue

1)Kama alikua amevaakofia ya baba wakati anatoa zawadi na alikua ameamua kutoa zawadi ya kitu cha kula basi baba mwema huto matunda ili mtoto wake ajifunze kula matunda na kujenga afya.Sio pipi aharibu meno FOR THAT AMEFELI

2)Kama alikua ameva kofia ya kiongozi wa nchi basi tuseme amemuona yule mwananchi ni cheap sana mpaka amakua kulahai kwa pipi kama wanavyofanya wakati wa kampeni kugawa kanga na miatano..Yule mtoto natataka elimu ajenge future FOR THAT AMEFELI TENA

kama kawaida yake mzee wa kufeli
 
'security breached'! huh,...acheni kuiangalia picha kiuoga uoga... msafara huo ulikuwa hata kuondoka bado.

Hamuwezi hata kuangalia reflection kwenye gari? Red Carpet, security staff,... Mungu wangu, are we serious hatuwezi kuangalia 'nje ya box' kiasi hiki?

kweli reflection inaonyesha gari limesimama na inaonyesha "red carpet" na watu ambao nadhani ni walinzi.

lakini siachi kujiuliza je katika hali kama hiyo
- huyo mtoto aliitwa na mheshimiwa kutoka kwenye kundi la watu?
- aliandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo ya kupokea zawadi?
- alichomoka tu mwenyewe kwa ujasiri wake na kumsogelea
mheshimiwa na walinzi walipojaribu kumzuia mheshimiwa akasema
"mwacheni mtoto aje kwangu..."
- je inawezekana ndio mheshimiwa alikuwa anawasili na kijana alikuwa
ameandaliwa kumpokea kiongozi hivyo kabla ya kuteremka
mheshimiwa akatoa zawadi n.k

ningekuwa na majibu ya uhakika ya maswali haya ndipo ningeweza kusema zaidi kuhusu ugawaji huo wa pipi. kwa vile majibu hayo sina inabidi nibakie nashangaa kuhusu masuala ya usalama wa rais. yaani anasafiri kiti cha mbele? kweli bongo tambarare
 
...inabidi nibakie nashangaa kuhusu masuala ya usalama wa rais. yaani anasafiri kiti cha mbele? kweli bongo tambarare

...ni kawaida hiyo kila wakitumia gari za 4WD, msiniulize kwanini. Halafu mnaolalamika, mmeshasahau Mzee Mwinyi alivyochapwa kibao? mbona mnamng'ang'ania ashuke kwenye gari?

Friday, 10 October 2008
RAIS KIKWETE ZIARANI MBEYA

...wasiwasi wangu, mikoa mingine kama hii wananchi hurusha mawe...!
 
Siyo lazima iwe security concern in the sense ya mtu kumuua, kuna vitu kama ajali etc. Kwa nini watoto huwekwa nyuma? Hii inaonyesha utovu sio tu wa itifaki, bali pia wa kanuni za usalama.

On the pipi tip, hapo naona kamjazia pipi kiasi kwamba ma dentist wanaweza ku take issue with the president's awareness when it comes to dental hygiene and health issues.

Back on the pipi issue, I'm sure dentists would be out of business but for pipi and other kinds of sweets. Very petty and trivial.

The security concern issue is more of a valid issue than who he gave pipi to.
 
Aisee mimi mlokole, kileo mwiko. Hakika Scenario building ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Laiti tungejenga scenario ya nchi tuitakayo miaka 50 ijayo. Siku hizi scenario building zetu zinaangalia miaka 5 ijayo tu!

Scenario hiyo ilitakiwa iishie hivi ili ilete inspiration endelevu:

Soma kwa bidii. Shirikiana na wenzako. Gawana nao pipi. Huo ndio Ujamaa. Tutawaletea vitabu mashuleni. Walimu nao tutawaongezea. Madarasa bora tutawajengea. Tutahakikisha mnafika sekondari. Na chuo pia. Umeniambia unapenda sayansi. Tutawajengea maabara shuleni. Hakika utakuwa mwanasayansi. Na utaisadia Tanzania. Kazana utaweza tu!

Mtoto ataondoka na hamasa. Mwaka 2050 atavumbua Nadharia ya Kulima kwa Nyuklia. Hatimaye Tanzania bila njaa na umaskini itakuwa imewezekana.

Oh man oh man! That scenario is quintessentially Companeronian...Lol..but don't get me wrong..I like it.
 
Aisee mimi mlokole, kileo mwiko. Hakika Scenario building ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Laiti tungejenga scenario ya nchi tuitakayo miaka 50 ijayo. Siku hizi scenario building zetu zinaangalia miaka 5 ijayo tu!

Scenario hiyo ilitakiwa iishie hivi ili ilete inspiration endelevu:

Soma kwa bidii. Shirikiana na wenzako. Gawana nao pipi. Huo ndio Ujamaa. Tutawaletea vitabu mashuleni. Walimu nao tutawaongezea. Madarasa bora tutawajengea. Tutahakikisha mnafika sekondari. Na chuo pia. Umeniambia unapenda sayansi. Tutawajengea maabara shuleni. Hakika utakuwa mwanasayansi. Na utaisadia Tanzania. Kazana utaweza tu!

Mtoto ataondoka na hamasa. Mwaka 2050 atavumbua Nadharia ya Kulima kwa Nyuklia. Hatimaye Tanzania bila njaa na umaskini itakuwa imewezekana.

Commandante:

Hiyo scenario angekuwa anazungumza na watoto wa darasa la saba. Huyo dogo bado sana.

Anyway, kuna siku Nyerere alipita kijiji kwetu akiwa safarini. Akasimamisha msafara na kumwita mzee wa kijiji. Basi Nyerere akatoa instant camera na kupiga picha na mzee wa kijiji na kumwachia mzee hile picha.

Mzee wa kijiji akaipiga picha yake kwenye frame na kuanza kuifanya kama mtaji.

Mtu yoyote akija kijijini na kuleta longolongo. Mzee anakuja na kukupiga mkwara kuwa atamwambia Nyerere ukamatwe. Ukiendeleza longolongo anakwenda ndani na kukuletea picha kuwa yeye na Nyerere ni damudamu na walishawahi kupiga picha pamoja.
 
yani umewakilisha point wala sina cha kuongeza zaidi.alichofanya jk anajua na ndio maana kuna wengine wamemsifia humu ndani.wengine wanawashutumu wazazi kuhusu matatizo ya huyo mtoto,je na wale wazazi wanaopoteza maisha wakati wa kujifungua wamlaumu nani kwa huduma zetu mbovu za hospitali? serikali iliweza kutenga bil 19 kwa ajili ya chai kwenye wizara zao lakini serika hio hio haina hela kutoa japo glasi moja ya maziwa kwa wiki kwa watoto mashuleni? mpaka wale watoto wanaokaa chini mashuleni tuwalaumu wazazi ambao wengi wao tunajua hali ngumu ya maisha hilivyo lakini hela ya mafisadi kuiba hipo na bila mchukuaji kujulikana.
kinachofanya tumlaumu jk kwenye hili swala ni uongozi wao mbovu na anajua kwamba watoto wanahitaji zaidi ya pipi. watoto pipi,wakubwa pilau huku mambo muhimu yameachwa tu.

Really huna la kuongezea? mbona umejaza mistari. Anyway, hakuna aliyemsifia JK kwa kitendo chake. Tunachosema kuwa kwa kutoa pipi hakuna lawama yoyote hile.

Kuhusu mambo muhimu kuachwa tu, ukweli wa mambo hilo ni collective responsibility. Huwezi kudai glass moja ya maziwa wakati uzalishaji wa maziwa ni kazi ya wananchi. Kama hamzalishi maziwa, yeye akatoe wapi?
 
Commandante:

Hiyo scenario angekuwa anazungumza na watoto wa darasa la saba. Huyo dogo bado sana.

Anyway, kuna siku Nyerere alipita kijiji kwetu akiwa safarini. Akasimamisha msafara na kumwita mzee wa kijiji. Basi Nyerere akatoa instant camera na kupiga picha na mzee wa kijiji na kumwachia mzee hile picha.

Mzee wa kijiji akaipiga picha yake kwenye frame na kuanza kuifanya kama mtaji.

Mtu yoyote akija kijijini na kuleta longolongo. Mzee anakuja na kukupiga mkwara kuwa atamwambia Nyerere ukamatwe. Ukiendeleza longolongo anakwenda ndani na kukuletea picha kuwa yeye na Nyerere ni damudamu na walishawahi kupiga picha pamoja.

Mkuu hiyo majuu wanaiiita urban legend. Bongo tunaiita nyepesi nyepesi. Anyway, ujumbe wako umefika. Na umenisaidia kulinganisha zawadi ya picha, pipi na pembejeo.

Inspiration huanza kutolewa kwa mtoto toka akiwa mdogo. Huo ndio umri wa kuanza kumrithisha vision ya Taifa aanze ku-imagine Taifa litavyokuwa miaka 50 ijayo na atakavyochangia kulifikisha huko. Pipi sio visheni. Heri hata angempa toy la kisayansi hivi. Au kalamu na kitabu cha kuchora/kuandika. Hebu tengeneza scenario ya mtoto aliyeachiwa/zawadiwa na Rais kitu cha kudumu cha kujenga ufahamu/maarifa na kuchochoea tafakuri/uvumbuzi. Just Imagine! If we could just envision the future that we really want to build and how to do so innovatively and reastically! Talking of scenario building I am reminded of this 'Tutafika: Tanzania Scenario Project':

The project seeks to provoke wide ranging conversations on the issues and challenges that Tanzania must face in the coming decades. Using scenarios - fables of the future - the project imagines three possible futures for the country: Yale Yale - a stagnant country in which nothing changes, certainly not for the better; Mibaka Uchumi - a nation owned by Big Thieves who capture political power and economic resources for private benefit and finally, Amka Kumekucha - a future shaped by adversity but founded on the strengths of social networks and created by a shared commitment to respond with imagination.

We cannot predict the future, but we can imagine it. These three stories describe what might happen in Tanzania in the
kweli.JPG
coming years. How will you prepare your family, or organization, or village, or town, or country to respond? Tanzania’s future depends critically on the choices made today. These choices are being shaped by individual and collective determination to overcome fear, inertia and complacency. We, as Tanzanians, hold our future in our hands.

Source: http://www.tutafika.org/
 
Really huna la kuongezea? mbona umejaza mistari. Anyway, hakuna aliyemsifia JK kwa kitendo chake. Tunachosema kuwa kwa kutoa pipi hakuna lawama yoyote hile.

Kuhusu mambo muhimu kuachwa tu, ukweli wa mambo hilo ni collective responsibility. Huwezi kudai glass moja ya maziwa wakati uzalishaji wa maziwa ni kazi ya wananchi. Kama hamzalishi maziwa, yeye akatoe wapi?

Zakumi, heshima mbele mkuu.Sikuelewi hapo,anaedai glasi ya maziwa ni nani na kwanini awe tofauti na wananchi?Ili wananchi wazalishe maziwa ni lazima wawe na wanyama wanaotoa hayo maziwa; wanaweza kuwa ng'ombe, mbuzi, Ngamia hata nyati! Ili wananchi waweze kuwamiliki hawa wanyama wanahita kuwa na uwezo wa kuwanunua; hapo sasa ndipo kazi ya viongozi inapotakiwa kuwawezesha ili wapate mtaji wa kununua hao wazalisha maziwa. Mtaji sio lazima kutoa fedha taslimu a' la mamilioni ya Kikwete kuwagawia wananchi bali hata kuweka enabling environment itakayowawezesha wananchi kufanya kazi na kupata mitaji.
 
Pipi ya kikwete kwa mtoto kuna maswali mengi......wengine wanachukulia kirahisi rahisi tu......lol ati rahisi anampa mtoto pipi? aah haiwezekani aisee
 
Pipi ya kikwete kwa mtoto kuna maswali mengi......wengine wanachukulia kirahisi rahisi tu......lol ati rahisi anampa mtoto pipi? aah haiwezekani aisee

Shem niliisha kuambia kwenye PM wewe genius....leo nimedelete home boy wangu kwenye hard disc anatetea ujinga na upumbavu eti raisi ajichanganye! hii kugawa pipi binafsi naichukulia tofauti sana is not a pipi Sikonge amempa mtoto wa urambo! huyu ni head of state jamani angempa Ridhiwani no question about that....yule mtoto anawakilisha millions of pipo.....with pipi kweli kuna watu madwanzi na viazi wanakuja na simple logic eti ni kama mzazi wewe nephew....fuc k you am not a presidaa...na hata hao siwapi pipi!
 
Wewe mkuu unaonekana una chuki binafsi na rais kikwete hv usijifanye huna sababu ya msingi hayo mambo ya pipi ni vitu vya kawaida kwa m2 yeyote yule!
 
Sasa eff this na eff that za nini? Kama mtu hoja yako ina nguvu hakuna ulazima wa kutumia profanities. Jenga hoja yako na uitetee na kama ina nguvu itasimama yenyewe bila msaada wa profanity.

Mpaka sasa hamjaonyesha chochote kibaya kilichotokana na Kikwete kumpa pipi dogo. Je, taifa limeingia hasara? Je, Kikwete asingempa pipi dogo kungekuwa na tofauti gani? Ghafla bin vuu dogo angerudi nyumbani na kukuta almasi kwenye sakafu?

Kuna mambo na mambo ya kukosoa. Lakini haya mengine ya peremende kwa watoto ni mambo trivial kwa kweli. Mkomalieni kuhusu ununuzi wa rada mbovu. Mkomalieni kuhusu Meremeta. Mshikieni bango Buzwagi. Mshikieni bango kuhusu maswala muhimu ya kitaifa.

Mnamshikia bango kama vile aliamka siku nzima na kuanza kugawa pipi hadi machweo. Specifically nitajieni ubaya wa yeye kuchukua vi dakika vichache baada ya kufungua hoteli ya kitalii na kumpa dogo hivyo vipipi. Taifa liliingia hasara gani kwa yeye kugawa hizo pipi?

You guys are complaining about pipi? Really? Just a couple candies? It's just candy y'all....candy..that's all it is....candy....Please tell me it ain't so.
 
Pipi ya kikwete kwa mtoto kuna maswali mengi......wengine wanachukulia kirahisi rahisi tu......lol ati rahisi anampa mtoto pipi? aah haiwezekani aisee

Yaorodheshe hayo maswali yako mengi. Siyo kusema sema eti maswali mengi...maswali yepi hayo? Yaorodheshe hapa...
 
Yaorodheshe hayo maswali yako mengi. Siyo kusema sema eti maswali mengi...maswali yepi hayo? Yaorodheshe hapa...

....aisee achana nao hao........hivi umeshampigia kura homegirl kwenye Miss Universe?
 
Back
Top Bottom