Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Kwa Rais wetu mambo ya kugawa pipi kwa watoto, kumwaga minoti mikoani (mabilioni ya Kikwete), kutoa pesa kwa disable (sometimes back around Samora or somewhere else in Dar) na mengineyo ndiyo style ya mkuu wetu. Kwa mtizamo wangu naona mambo kama haya hayasaidii kuondoa matatizo ya msingi yanayoikabili jamii bali ni njia ya kujipata umaarufu ama kulazimisha kupendwa.

BRAVO MUKULU!!!!!!!!
 
Dah! Hii scenario yako Companero akiiona lazima akununulie bia....si unamjua alivyo?

Ningeshapata kopo la wanzuki. Tatizo hapa watu wanataka wote tuwe CHADEMA kind of thing. Kuvaa magwanda ya mgambo kwenye mikutano hili kuonyesha seriousness.
 
Ningeshapata kopo la wanzuki. Tatizo hapa watu wanataka wote tuwe CHADEMA kind of thing. Kuvaa magwanda ya mgambo kwenye mikutano hili kuonyesha seriousness.

Jamani Kutoka Mabilioni ya Kikwete hadi mapipi?
 
dah waTZ bado tupo nyuma yaani muda wote mnajadili pipi kha!
 
Kwa Rais wetu mambo ya kugawa pipi kwa watoto, kumwaga minoti mikoani (mabilioni ya Kikwete), kutoa pesa kwa disable (sometimes back around Samora or somewhere else in Dar) na mengineyo ndiyo style ya mkuu wetu. Kwa mtizamo wangu naona mambo kama haya hayasaidii kuondoa matatizo ya msingi yanayoikabili jamii bali ni njia ya kujipata umaarufu ama kulazimisha kupendwa.

BRAVO MUKULU!!!!!!!!

Hata angekuwa serious kama unavyotaka wewe, matatizo mengine ya Tanzania ni ya kudumu.
 
JF inafurahisha!

Raisi anasafiri na mapipi kwenye gari, mabaki anagawia watoto ambao anajua kabisa kama kiongozi wa nchi wanahitaji zaidi ya pipi....

Ulitaka agawe nini? na angegawa kwa wangapi? si ndo watu wangekuwa wanakaa tu na kusubiria zawadi za raisi na ndo ingekuwa JK anapendelea na vitu kama hivyo jamani..
Leave out Sarkozy na huyo Barak, huwezi fananisha na JK pia Tanzania yetu kabisa. Hapo ndo tunapokosea sometimes kwenye mifano.
Sema ulitaka ampe nini huyo mtoto ha hivi ni mpita njia tu?
Sikutegemea Raisi awe anakwenda kufanya shopping ya kununua mipipi kwa ajili ya kuwagawia watoto fukara atakaokutana nao barabarani.

Nani atujulishe ikiwa amewahi kumwona babake akikatiza mitaani kugawia pipi watoto fukara asiowajua ambao sio wake au walau basi wa jirani yake?

Kikwete anasoma vitabu gani kwenye muda wake wa spare - maana inaonesha anao muda mwingi wa kufanya shopping ya pipi. (Hata kama shopping amefanya USA, haijalishi) Hii mambo ya ku-chat na watoto omba-omba kwa kuchungulia dirishani imekaa kushoto.

Kikwete alimtembelea mtu walau mmoja kweye mabomu ya mbagala? Alitoa tamko lolote? Mi nakumbuka kumwona mkuu wa mkoa tu!
 
Kwa rais wa nchi hii aingii akilini hizo pipi alibeba intentionally kwa ajili ya watoto au alikuwa anatumia mwenyewe?!Tusiyachukulie mambo simple simple tu angefanya hivyo mpita njia kusingekuwa na shida but Prezdent hii imekaa kushoto wana JF.

Katika ziara zake mikoani anatakiwa kufikiria mambo ya msingi ya kuwasaidia watanzania sio kuwaza abebe pipi ngapi kwa ajili ya watoto huo muda anaupata wapi wakati waTz tunateketea kwenye dimbwi la ufukara halafu rais anafikiria kupeleka zawadi ya pipi kwa jamii.
 
dah waTZ bado tupo nyuma yaani muda wote mnajadili pipi kha!

Komredi...watu wanasahau kuwa JK alikuwa katoka kufungua hoteli mpya ya kitalii hapo mkoani Lindi na badala yake wameshikia bango yeye kumpa dogo pipi. Badala ya kujadili vipi hoteli hiyo itakuwa na manufaa kwa Lindi n.k. Lol....
 
Mambo mengine yanachekesha kwa kweli naona watu wanapoteza muda kujadili mambo yasiyo namsingi, hivi ile tabia ya mabasi ya hapo nyumbani yale yanayoenda mkoani huwa wanagawa pipi wameacha?? mimi na fikiri kwa kukusaidia tu we mtoa mada ni kwamba..

Pipi zinasaidia kuchangamsha mdomo na kufanya mdomo usitoe harufu mbaya wakati wa safari ndefu na ninafikiri kwa picha yenyewe inavyojionyesha ni wazi kuwa mh alikuwa safarini na hapo gari inaonekana imepark sasa kama huyo mtoto alisogolea gari ya rais na watu wa usalama hawakuona kama anaweza akawa na athari zozote kuna ubaya kwa raisi kumpatia pipi huyo mtoto? Kwani raisi haruhusiwi kula pipi?

Hebu acheni vichekesho jamani tunalalamika sana pasipo na sababu za msingi mambo mengine ni kichekesho, hii nchi toka imekombolewa kutoka kwa wakoloni ni awamu nne sasa za uraisi zimepita sasa kama hao huko nyuma walishindwa kuweka misingi mizuri ya elimu na huyu naye aliyepo tunategemea ataweza kuweka? Mi nafikiri tuwe tunalalamika na kurusi kwenye historia kidogo,,, eti unauliza raisi anafanya shopping ya kununua mapipi hahahaha nani aliyekwambia raisi anakwenda dukani kwa mangi na kumwambia aloo shirima hebu nipagtie pipi na bazoka hahahaha wacha nicheke mie maana tunaacha kupigania mambo ya maana tunajadili pipi doh
 
It shows how superficial he is; anaangalia matatizo na mambo kijuujuu bila kuwa analytical na kujua implications zake!! Hypothetically, suppose huyu mtoto angekuwa anaumwa kisukali, je angekuwa anamsaidia au kumuua? On the other hand angempa kalamu au daftari huoni kuwa hiyo ingekuwa motivation kwa mtoto kujifunza? Wamezowea kuhadaa watu kwahiyo mambo yao yote ni ya Kisanii Sanii!!
 
Hebu tujenge scenario hapa inayomake sense. Raisi anafanya ziara akiwa ndani ya moja ya mashangingi yake. Njiani anakutana na katoto ambako kwa dalili zote na za wazi kabisa kanareflect hali za watoto wengi vijijini. Kitu anachofanya Raisi ni kungiza mkono mfukoni au ndani ya boksi la pipi analotembea nalo kwenye gari na kukapa katoto haka pipi.

Katoto kanatoka mbio kwa furaha hadi kwa wazazi wake ambao kwa wakati huo labda hawajui hata mlo wa siku hiyo utapatikanaje. Wazazi wanamwuliza mtoto hizo pipi katoa wapi na mtoto anasema kapewa na Raisi ! Ghafla mzazi anakumbuka kwa mbali kuwa mwaka 2005 walipewa kanga, fulana na kofia wakati wa kampeni ili wampe kura mgombea Uraisi !

Baba anamgeukia mkewe huku macho yakilengalenga machozi na kwa huzuni anatikisa kichwa - anakumbuka jinsi maisha tangu siku hiyo yalivyozidi kuwa ya dhiki siku hadi siku !

Raisi aliyewaahidi maisha bora leo, miaka mitano baadaye, anapita akigawa pipi kwa watoto !

...Scenario yako inanikumbusha David Banda-Madonna alivyomuuliza baba yake, "why are you poor?" baba mtu akabakia anacheka cheka tu.

Umasikini ni matokeo ya uvivu wa kufikiri!

Maisha bora hayaji kwa kusubiria ahadi zilizoahidiwa. Maisha bora ni nguvu ya pamoja baina ya mtoa ahadi na muahidiwa. Kulia lia hakutotufikisha popote. Walioukimbia umande na kukosa elimu ya msingi, sekondari na vyuo (enzi hizo elimu ulivyokuwa bure), ndio wengi wanao warithisha umasikini vizazi na vizazi vyao!
 
It shows how superficial he is; anaangalia matatizo na mambo kijuujuu bila kuwa analytical na kujua implications zake!! Hypothetically, suppose huyu mtoto angekuwa anaumwa kisukali, je angekuwa anamsaidia au kumuua? On the other hand angempa kalamu au daftari huoni kuwa hiyo ingekuwa motivation kwa mtoto kujifunza? Wamezowea kuhadaa watu kwahiyo mambo yao yote ni ya Kisanii Sanii!!

Hivi wewe umeshawahi kutoa hata mchango wa mpira wa miguu katika shule uliyosoma? Kama wewe huwezi kutoa mchango wa maendeleo kwa kijiji chako au sehemu uliyotoka, unategemea rais afanye nini?
 
Sikutegemea Raisi awe anakwenda kufanya shopping ya kununua mipipi kwa ajili ya kuwagawia watoto fukara atakaokutana nao barabarani...

...matumizi ya political science kwa vitendo mkuu, hakuna cha ajabu hapo.
 
Chochote ambacho rasi angempa mtoto huyo ingekuwa issue..maswali hayakosekani hasa kwa watu wanaotaka kujua maana ya kila tendo!
Mabinti wa Kibongo ukimpa offer ya beer tayari wamekwisha judge unamtaka! ukimwambia karibu nyumbani utaulizwa kama una mke.. Ukimtongoza utaambiwa ngoja afikirie - ili mradi mchezo wa reality show imeanza...
 
Lol...Bob bana nazimia sana thinking yako saa ingine! Lakini uko sawa kabisa...JK hapo angempandishia kioo dogo watu wangemaindi kuwa anaringa. Either way he's damned...damned if you do damned if you don't.
 
Hivi wewe umeshawahi kutoa hata mchango wa mpira wa miguu katika shule uliyosoma? Kama wewe huwezi kutoa mchango wa maendeleo kwa kijiji chako au sehemu uliyotoka, unategemea rais afanye nini?

Rais hatakiwi kufuata mimi ninachofanya; yeye anatakiwa kuwa kiongozi ili mimi niige mfano wake, Rais anatakiwa kuonyesha njia! He is supposed to be our role model! Zakumi, heshima yako mkuu; mimi niko hapa hapa nyumbani na kila mwaka ninatoa zawadi za vifaa vya elimu kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye shule niliyosoma. Kumbuka kwamba Rais wa nchi sio sawa na mimi au wewe, whatever he does or says is up for scrutiny!!
 
It shows how superficial he is; anaangalia matatizo na mambo kijuujuu bila kuwa analytical na kujua implications zake!! Hypothetically, suppose huyu mtoto angekuwa anaumwa kisukali, je angekuwa anamsaidia au kumuua? On the other hand angempa kalamu au daftari huoni kuwa hiyo ingekuwa motivation kwa mtoto kujifunza? Wamezowea kuhadaa watu kwahiyo mambo yao yote ni ya Kisanii Sanii!!
yani umewakilisha point wala sina cha kuongeza zaidi.alichofanya jk anajua na ndio maana kuna wengine wamemsifia humu ndani.wengine wanawashutumu wazazi kuhusu matatizo ya huyo mtoto,je na wale wazazi wanaopoteza maisha wakati wa kujifungua wamlaumu nani kwa huduma zetu mbovu za hospitali? serikali iliweza kutenga bil 19 kwa ajili ya chai kwenye wizara zao lakini serika hio hio haina hela kutoa japo glasi moja ya maziwa kwa wiki kwa watoto mashuleni? mpaka wale watoto wanaokaa chini mashuleni tuwalaumu wazazi ambao wengi wao tunajua hali ngumu ya maisha hilivyo lakini hela ya mafisadi kuiba hipo na bila mchukuaji kujulikana.
kinachofanya tumlaumu jk kwenye hili swala ni uongozi wao mbovu na anajua kwamba watoto wanahitaji zaidi ya pipi. watoto pipi,wakubwa pilau huku mambo muhimu yameachwa tu.
 
Back
Top Bottom