Rais kusema hatoacha kufanya Mabadiliko katika Serikali yake ni Udhaifu usiovumilika na wenye Akili

Rais kusema hatoacha kufanya Mabadiliko katika Serikali yake ni Udhaifu usiovumilika na wenye Akili

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Na kwa wenye Akili tukiona Mabadiliko ya mara kwa mara tunathibitisha kuwa huenda kuna Watu wako mahala kwa bahati mbaya / Fluku.

Ngoja tuendelee Kunywa Mtori taratibu na huenda Nyama tunazozitaka tutazikuta chini.
 
Ye anaona ni sifa lakini ilitakiwa aseme hapendi kuteua na kutengua kila mara sababu inadhoofisha utendaji.

Hii maana yake ni kuwa;

1. Mtu hana uhakika wa kudumu kwenye nafasi aliyoteuliwa.
2. Watu wataogopa kufanya maamuzi kwa kuogopa kutenguliwa.
3. Watu watatumia nafasi kupiga dili maana wanajua hawatadumu na wanaweza tenguliwa kwa makosa ya wengine au kwa majungu tu.
4. Kawaida mtu akiajiliwa huchukua muda ili kujifunza na kudeliver. Kwa huyu ni ngumu kudeliver kwa sababu anabadili kila mara.
5. Lakini inaonyesha kuna upungufu kwenye kuteua. Hakuna screening. Ni kama kupeana kwa kufurahishana. Tukishindwana nakutengua.
6. Inaondoa heshima ya hizo nafasi na hata yeye raisi kuonekana mtu dhaifu na asiyeelewa anataka nini.
 
Back
Top Bottom