Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Rais anapoteua watu then KM au Waziri akaelekeza wawasilishe vyeti au CV haileti tafsir kwamba Rais anakosolewa kwa maamuzi ya uteuzi aliyofanya?

Lakini napenda kujua, kwa kazi zinazohitaji wasomi Ni kipi kinatangulia kupeleka vyeti au kuteuliwa? Kama tunateua ndipo walete vyeti tunatumia sifa gani?
Hatusemi kwamba nchi hii ni "Banana Republic" kwa makosa.

Tuna hali mbaya sana kama nchi. Sijui kama siku moja tutabahatika kutoka huku shimoni tulikojichimbia wakati huu.

Unaweza kuikuta Tanzania ya 2050 ikiwa haina tofauti yoyote na kama ilivyo Haiti tokea ipate uhuru wake miaka mia na zaidi sasa.
 
Lakini nakumbuka baada ya kuapishwa, Katibu Kiongozi ambaye ndiye mhusika mkuu wa masuala ya kiutendaji, alisema kati ya tatizo aliliona kwenye serikali lilikuwa ni hili unalosema la serikali kufanya kazi' in silos'.

Sasa sijui naona kwa yanayoendelea hadi sasa,labda naona kashindwa kutatua changamoto hiyo kaazi kwelikweli.
Ukiwa nje ya.... kila kitu hua rahisi tofauti na uhalisia, mpaka sasa hii ndo serikali ilionesha kufeli karibu kila kona ndani ya muda mfupi. Inshort serikali kwa sasa inatia huruma.
 
Unapomweka mfanyakazi mwenye uzoefu wa kuwa mjumbe wa uvccm kwa kazi inayohitaji utaalamu wa kiserikali wa miaka 10 sijui tunategemea miujiza????

Na huyo wa chini aliyekuwa anastahili hiyo nafasi atamwelekeza kwa vipi???

Hii ni kutengeneza shida kuanzia siku ya kwanza!! UDC afadhali lakini siyo UDED !!
 
Hivyo vibinti unaweza kukuta vinaenda kuwa chakula ya baadhi ya wakuu wa idara maana bado vinawashwa washwa.
 
Hako cha juu kabisa kamefikisha miaka 18? anyway kwa record zake sitashangaa huyu Rais akimpa ajira under age.

Tuseme ukweli tu, Samia amechoka sana akili ndio maana mambo yake mengi anakosea tu.
Hahaha 😂😂😂Joan mtoto wa anko wangu mzee Kataraia. Amewahi kuwa mbunge mkoani Kagera na M/kiti au Naibu kama sikosei CCM Mwanza. Now yupo Marekani
 
View attachment 1877625
View attachment 1877629
View attachment 1877630

Hawa ni baadhi ya vijana wadogo kabisa toka UVCCM walioteuliwa kuwa makurugenzi.

KWA MUJIBU WA MEMORANDA YA FEDHA SERIKALI ZA MITAA(LGA) HAYA NDIO MAJUMKUMU MAZITO YA DED

1. Ensuring the existence of a formal and satisfactory system of financial administration;

2. Securing compliance with the prescribed financial procedures by operating departments;

3. Directing the work of the Internal Audit section, receiving their reports and after consultation with relevant head of departments, ensuring recommendations and acted upon and submitted to relevant authorities;

4. Overall management of Council’s expenditures, revenues, and all assets and liabilities;

5. Ensuring compliance of all statutory guidelines for the financial Management of Council affairs;

6. Responding to queries within given deadlines from the Office of the Controller and Auditor General, the Local Authority Account Committee (LAAC) and the Minister;

7. Making certain that councillors are kept regularly informed of the financial affairs of the Council;

8. Being secretary to the finance Committee;

9. Making sure that computerized system operates;

10. Keeping under good Custody all assets and property of the Council; and

11. Adhering to procurement functions stipulated in Public Procurement Act and its related

KWA TAFSIRI ISIYO RASMI

1. Kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na wakuridhisha katika usimamizi wa fedha

2. Kuhakikisha idara zinafanya matumizi kwa mujibu wa taratibu za fedha

3. Kuhakikisha kitengo cha ukaguzi wa ndani kinafanya kazi vyema, kupokea taarifa za ukaguzi wa ndani, na kwa kushirikiana na wakuu wa idara ahakikishe maoni ya mkaguzi wa ndani yanajibiwa na kutekelezwa na anawasilisha majibu hayo kwa mamlaka husika ambazo ni CAG, RAS na Chief Internal Auditor

4. Usimamizi wa matumizi, mapato, mali na madeni yote ya halmashauri kwa ujumla

5. Kuhakikisha sharia, sera, kanuni na miongozo yote ya usimamizi wa fedha za halamashauri inafuatwa.

6. Kuhakikisha kuwa anajibu kwa wakati hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wizara

7. Kuhakikisha waheshimiwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halamashauri

8. Kuwa katibu wa Kamati ya fedha ya Halamshauri. Kamati hii wajumbe wake ni madiwani.

9. Kuhakikisha mifumo ya kompyuta inafanya kazi

10. Kuhakikisha utunzaji mzuri wa mali za Halmashauri

11. Kuhakisha sharia ya manunuzi ya umma na kanuni zake zinafuatwa

MAJUMKU MENGINEYO

1. Kuidhinisha malipo

2. Kuidhinisha mikataba yote ya halmashauri

3. Kuteua Bodi ya Zabuni kwa mujibu wa sharia

4. Kuteua Kamati ya Ukaguzi(Audit Committee) kwa mujibu wa sharia

5. Kuwa mkurugenzi wa uchaguzi ngazi ya wilaya pale inapotokea

6. Kuteua kamati ya upembuzi wakati wa manunuzi makubwa

MY TAKE

Hii kazi sio rahisi kama mashabiki wa mwendo kasi mnavyodhani. Huyu mtu anaenda kuwa msimamizi wa idara 19 pale halmashauri. Ikiwepo idara ya elimu na afya zenye changamoto za kufa mtu. Huyu mtu ndio anaenda kukuza uchumi wa wilaya na kuongeza pato la taifa kupitia wilaya yake. Mikataba mikubwa ya mabilioni ya fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo inaenda kuidhinishwa na yeye baada ya kujiridhisha kila kitu kiko sawa.

Anakwenda kusimamia matumizi ya mapato ya ndani ya zaidi ya bilioni 20 mfano Manispaa ya Kinondoni mpaka milioni 500 kwa halmashauri mpya. Anakwenda kusimamia ruzuku ya serikali mabilioni ya fedha.

Anakwenda kusimamia ufungaji wa hesabu na kujibu hoja ngumu za CAG kama tulivyoona hapo juu, matokeo yake unashindwa kuzuia au kujibu hoja unaanda maburungutu ya kuhonga wakaguzi

Kwa maoni yangu, serikali isione aibu, pangia hawa watu wasio na sifa majuku mengine mara moja. System inajua nani mwenye uwezo na asiye na uwezo

Mjadala
Je, huku ni kunajisi utumishi wa umma?

Thanks

Tatizo kubwa, dhana ya “serikali za mitaa” ni kama haikubaliki kabisa Tanzania. Bila shaka hii inatokana na dhamira ya CCM kutaka kuhakikisha inatawala katika mfumo wa “dola moja tu” (TOTALITARIAN STATE). Hakuna kugawa au kupunguzia madaraka ya Rais kwa mtu au taasisi nyingine.

Nyerere mwenyewe alichukua hatua kadhaa kunyang’ang’anya madaraka ya serikali za mitaa kwa kuhakikisha viongozi wa serikali za mitaa wanadhibitiwa na chama na Ofisi ya Rais kupitia Waziri Mkuu. Lakini hakubadili utaratibu wa utumishi wa serikali hizo na hierarchy yake katika kupata wakurugenzi na viongozi wengine wa halmashauri.

Magufuli yeye aliweka soni pembeni akapangua kila kitu. Akahamishia TAMISEMI Ofisi ya Rais moja kwa moja - kama kuua dhana ya serikali za mitaa - na kuteua yoyote toka popote kuwa DED!

Hata kwenye serikali kuu alipangua kabisa kanuni za teuzi zilizokuwepo na kujipa uhuru wa kuteua na kufukuza anavyojisikia.

Nionavyo, Magufuli aliamua kabisa kubomoa mfumo, kanuni na taratibu za serikali yote ili kuuandaa kisaikolojia umma wa Watanzania kwamba wasahau na kuachana na serikali kama walivyoifahamu na kutambua kwamba sasa “serikali ni Magufuli”. Absolute powers consolidation. Hiyo ndiyo legacy yake kuu.

Mh. SSH, ama kwa utashi wake mwenyewe au kwa kushauriwa na wasiotaka demokrasia kabisa, kaamua kukamatia yale mambo ya Magufuli yatakayomhakikishia yeye na CCM yake hawataachia madaraka kirahisi. Sijui atawezaje kuweka balance kati ya kuua demokrasia nchini huku akitaka kukubalika kimataifa na kuaminika na wawekezaji.
 
Kama haya ndiyo majukumu ya DED basi maDED wote wawe either WACHUMI ama WAHASIBU.
Ndivyo ilivyokuwa zamani...Multiparty ilipoanza na kura zilipokuwa ndiyo moja ya mambo ya mkurugenzi tukapoteza kabisa focus
 
Wengine bila kutafsiriwa hayo majukumu hawalewi kitu. Hapo sasa kosa ni la mteuzi siyo mteuliwa
 
Hizi nafasi zilipaswa kupewa watumishi waandamizi wa serikali siyo wasanii mitaani na vijana ambao hawajawahi kuajiriwa serikalini. Nafikiri mteuzi ndiye tatizo hajui uzito wa majukumu hayo
View attachment 1877625
View attachment 1877629
View attachment 1877630

Hawa ni baadhi ya vijana wadogo kabisa toka UVCCM walioteuliwa kuwa makurugenzi.

KWA MUJIBU WA MEMORANDA YA FEDHA SERIKALI ZA MITAA(LGA) HAYA NDIO MAJUMKUMU MAZITO YA DED

1. Ensuring the existence of a formal and satisfactory system of financial administration;

2. Securing compliance with the prescribed financial procedures by operating departments;

3. Directing the work of the Internal Audit section, receiving their reports and after consultation with relevant head of departments, ensuring recommendations and acted upon and submitted to relevant authorities;

4. Overall management of Council’s expenditures, revenues, and all assets and liabilities;

5. Ensuring compliance of all statutory guidelines for the financial Management of Council affairs;

6. Responding to queries within given deadlines from the Office of the Controller and Auditor General, the Local Authority Account Committee (LAAC) and the Minister;

7. Making certain that councillors are kept regularly informed of the financial affairs of the Council;

8. Being secretary to the finance Committee;

9. Making sure that computerized system operates;

10. Keeping under good Custody all assets and property of the Council; and

11. Adhering to procurement functions stipulated in Public Procurement Act and its related

KWA TAFSIRI ISIYO RASMI

1. Kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na wakuridhisha katika usimamizi wa fedha

2. Kuhakikisha idara zinafanya matumizi kwa mujibu wa taratibu za fedha

3. Kuhakikisha kitengo cha ukaguzi wa ndani kinafanya kazi vyema, kupokea taarifa za ukaguzi wa ndani, na kwa kushirikiana na wakuu wa idara ahakikishe maoni ya mkaguzi wa ndani yanajibiwa na kutekelezwa na anawasilisha majibu hayo kwa mamlaka husika ambazo ni CAG, RAS na Chief Internal Auditor

4. Usimamizi wa matumizi, mapato, mali na madeni yote ya halmashauri kwa ujumla

5. Kuhakikisha sharia, sera, kanuni na miongozo yote ya usimamizi wa fedha za halamashauri inafuatwa.

6. Kuhakikisha kuwa anajibu kwa wakati hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wizara

7. Kuhakikisha waheshimiwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halamashauri

8. Kuwa katibu wa Kamati ya fedha ya Halamshauri. Kamati hii wajumbe wake ni madiwani.

9. Kuhakikisha mifumo ya kompyuta inafanya kazi

10. Kuhakikisha utunzaji mzuri wa mali za Halmashauri

11. Kuhakisha sharia ya manunuzi ya umma na kanuni zake zinafuatwa

MAJUMKU MENGINEYO

1. Kuidhinisha malipo

2. Kuidhinisha mikataba yote ya halmashauri

3. Kuteua Bodi ya Zabuni kwa mujibu wa sharia

4. Kuteua Kamati ya Ukaguzi(Audit Committee) kwa mujibu wa sharia

5. Kuwa mkurugenzi wa uchaguzi ngazi ya wilaya pale inapotokea

6. Kuteua kamati ya upembuzi wakati wa manunuzi makubwa

MY TAKE

Hii kazi sio rahisi kama mashabiki wa mwendo kasi mnavyodhani. Huyu mtu anaenda kuwa msimamizi wa idara 19 pale halmashauri. Ikiwepo idara ya elimu na afya zenye changamoto za kufa mtu. Huyu mtu ndio anaenda kukuza uchumi wa wilaya na kuongeza pato la taifa kupitia wilaya yake. Mikataba mikubwa ya mabilioni ya fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo inaenda kuidhinishwa na yeye baada ya kujiridhisha kila kitu kiko sawa.

Anakwenda kusimamia matumizi ya mapato ya ndani ya zaidi ya bilioni 20 mfano Manispaa ya Kinondoni mpaka milioni 500 kwa halmashauri mpya. Anakwenda kusimamia ruzuku ya serikali mabilioni ya fedha.

Anakwenda kusimamia ufungaji wa hesabu na kujibu hoja ngumu za CAG kama tulivyoona hapo juu, matokeo yake unashindwa kuzuia au kujibu hoja unaanda maburungutu ya kuhonga wakaguzi

Kwa maoni yangu, serikali isione aibu, pangia hawa watu wasio na sifa majuku mengine mara moja. System inajua nani mwenye uwezo na asiye na uwezo

Mjadala
Je, huku ni kunajisi utumishi wa umma?

Thanks
 
Well said
Mm sipingi teuzi na si mshabiki wa siasa, ila Kwa majukumu haya nimeona Kwa wengine ni mazito hata kama sijui akili zao na uwezo wao. Kwa ushauri wangu wangekua na succession plan ya kuwandaa hawa watu ili wawe mentored kwenye majukumu (just a kind of an on job training) ili akiachiwa aje kuweza kujisimamia. Kumbuka anasimamia watu wazima wenye uzoefu na kona zote za idara, kuna watu ni mafisi kwenye swala la fedha na mambo mengine, hawa vijana fresh from school hizo kona hawazijui. So next time wawasaidie kuwafanyia a kind of mentorship, itawasadia.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Hako cha juu kabisa kamefikisha miaka 18? anyway kwa record zake sitashangaa huyu Rais akimpa ajira under age.

Tuseme ukweli tu, Samia amechoka sana akili ndio maana mambo yake mengi anakosea tu.
Hahaha 😂😂😂Joan mtoto wa anko wangu mzee Kataraia. Amewahi kuwa mbunge mkoani Kagera na M/kiti au Naibu kama sikosei CCM Mwanza. Now yupo Marekani
 
Hahaha 😂😂😂Joan mtoto wa anko wangu mzee Kataraia. Amewahi kuwa mbunge mkoani Kagera na M/kiti au Naibu kama sikosei CCM Mwanza. Now yupo Marekani
Huko Marekani yupo kazini au ameenda likizo kuwatembelea ndugu na jamaa? mbona kwenye list ya wabunge waliowahi kutokea Kagera hayupo? au ubunge gani unazungumzia.
 
Utakua wa juzi. Bukoba mjini amewahi kuwa mbunge anaitwa Mujuni Kataraia. Marekani kwa wanae. Yupo broke vibaya mno kwa sasa.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Hii nchi kuendelea itakua ngumu sana; asimilia kubwa ya wakurugenzi wanaotokana na wanasiasa mara nyingi kama siyo zote wanatumia muda mwingi kujipanga namna ya kupata jimbo uchaguzi ujao kwani wengi walikua ni washiriki kwenye mchakato wa uchaguzi uliopita.
Hii ni tofauti na watumishi walioteuliwa kua DED; sijajua nia hasahasa ya viongozi wanafanya teuzi ni wananchi kupata maendeleo au yeye kuendelea kubaki madarakani?
 
Utakua wa juzi. Bukoba mjini amewahi kuwa mbunge anaitwa Mujuni Kataraia. Marekani kwa wanae. Yupo broke vibaya mno kwa sasa.
Sorry! nilielewa kua Joan ndiye yupo Marekani na ndo aliwahi kua mbunge. Basi ungesema Joan ni mtoto wa Mbunge staafu wa Bukoba.
Asante nimekuelewa; vp Mh DED yeye anafanya mishe gani hapa mjini
 
Ah! Kweli imebidi nisome upya. Sikua nimeandika vema kweli hapo mwanzo kumuwia mtu ugumu kuelewa.
Joan alikua active na UVCCM sidhani aliwahi kufanya kazi sehemu. Ila ni humble sana na si mtoto kama wengi wanavyodhani.
Ila kwa hii nafasi hata mie natia shaka. Siwezi kusifia tu kisa nina nasaba naye. Namna hiyo tunaua nchi!
 
Waligombea viti maaluma na akina Halima Bulembo pamoja na mzazi mwenzangu mmoja hivi. Ila sijajua kwanini anachaguliwa mtu ambae hajawahi kua mtumishi wa umma/private kwa muda mrefu na mwenye kutolea maamuzi mambo magumu.

Fikiria watu wanavyopiga zile pesa za mikopo ya makundi mbalimbali zinazotolewa na manispaa au halmashauri kwa ajili ya kuinua wananchi ki mapato ndiyo uwapeleke watu kama hawa wakazisimamie.

Akiletewa vocha ya cheki ya 700bil na mhasibu ikiwa bado dk 10 benki ifungwe yeyeatasign tu bila kupitia vizuri.
Maendeleo bado sana.
 
Back
Top Bottom