Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Hatusemi kwamba nchi hii ni "Banana Republic" kwa makosa.

Tuna hali mbaya sana kama nchi. Sijui kama siku moja tutabahatika kutoka huku shimoni tulikojichimbia wakati huu.

Unaweza kuikuta Tanzania ya 2050 ikiwa haina tofauti yoyote na kama ilivyo Haiti tokea ipate uhuru wake miaka mia na zaidi sasa.
 
Ukiwa nje ya.... kila kitu hua rahisi tofauti na uhalisia, mpaka sasa hii ndo serikali ilionesha kufeli karibu kila kona ndani ya muda mfupi. Inshort serikali kwa sasa inatia huruma.
 
Unapomweka mfanyakazi mwenye uzoefu wa kuwa mjumbe wa uvccm kwa kazi inayohitaji utaalamu wa kiserikali wa miaka 10 sijui tunategemea miujiza????

Na huyo wa chini aliyekuwa anastahili hiyo nafasi atamwelekeza kwa vipi???

Hii ni kutengeneza shida kuanzia siku ya kwanza!! UDC afadhali lakini siyo UDED !!
 
Hivyo vibinti unaweza kukuta vinaenda kuwa chakula ya baadhi ya wakuu wa idara maana bado vinawashwa washwa.
 
Hako cha juu kabisa kamefikisha miaka 18? anyway kwa record zake sitashangaa huyu Rais akimpa ajira under age.

Tuseme ukweli tu, Samia amechoka sana akili ndio maana mambo yake mengi anakosea tu.
Hahaha ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Joan mtoto wa anko wangu mzee Kataraia. Amewahi kuwa mbunge mkoani Kagera na M/kiti au Naibu kama sikosei CCM Mwanza. Now yupo Marekani
 
Tatizo kubwa, dhana ya โ€œserikali za mitaaโ€ ni kama haikubaliki kabisa Tanzania. Bila shaka hii inatokana na dhamira ya CCM kutaka kuhakikisha inatawala katika mfumo wa โ€œdola moja tuโ€ (TOTALITARIAN STATE). Hakuna kugawa au kupunguzia madaraka ya Rais kwa mtu au taasisi nyingine.

Nyerere mwenyewe alichukua hatua kadhaa kunyangโ€™angโ€™anya madaraka ya serikali za mitaa kwa kuhakikisha viongozi wa serikali za mitaa wanadhibitiwa na chama na Ofisi ya Rais kupitia Waziri Mkuu. Lakini hakubadili utaratibu wa utumishi wa serikali hizo na hierarchy yake katika kupata wakurugenzi na viongozi wengine wa halmashauri.

Magufuli yeye aliweka soni pembeni akapangua kila kitu. Akahamishia TAMISEMI Ofisi ya Rais moja kwa moja - kama kuua dhana ya serikali za mitaa - na kuteua yoyote toka popote kuwa DED!

Hata kwenye serikali kuu alipangua kabisa kanuni za teuzi zilizokuwepo na kujipa uhuru wa kuteua na kufukuza anavyojisikia.

Nionavyo, Magufuli aliamua kabisa kubomoa mfumo, kanuni na taratibu za serikali yote ili kuuandaa kisaikolojia umma wa Watanzania kwamba wasahau na kuachana na serikali kama walivyoifahamu na kutambua kwamba sasa โ€œserikali ni Magufuliโ€. Absolute powers consolidation. Hiyo ndiyo legacy yake kuu.

Mh. SSH, ama kwa utashi wake mwenyewe au kwa kushauriwa na wasiotaka demokrasia kabisa, kaamua kukamatia yale mambo ya Magufuli yatakayomhakikishia yeye na CCM yake hawataachia madaraka kirahisi. Sijui atawezaje kuweka balance kati ya kuua demokrasia nchini huku akitaka kukubalika kimataifa na kuaminika na wawekezaji.
 
Kama haya ndiyo majukumu ya DED basi maDED wote wawe either WACHUMI ama WAHASIBU.
Ndivyo ilivyokuwa zamani...Multiparty ilipoanza na kura zilipokuwa ndiyo moja ya mambo ya mkurugenzi tukapoteza kabisa focus
 
Wengine bila kutafsiriwa hayo majukumu hawalewi kitu. Hapo sasa kosa ni la mteuzi siyo mteuliwa
 
Hizi nafasi zilipaswa kupewa watumishi waandamizi wa serikali siyo wasanii mitaani na vijana ambao hawajawahi kuajiriwa serikalini. Nafikiri mteuzi ndiye tatizo hajui uzito wa majukumu hayo
 
Well said
 
Reactions: Qwy
Hako cha juu kabisa kamefikisha miaka 18? anyway kwa record zake sitashangaa huyu Rais akimpa ajira under age.

Tuseme ukweli tu, Samia amechoka sana akili ndio maana mambo yake mengi anakosea tu.
Hahaha ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Joan mtoto wa anko wangu mzee Kataraia. Amewahi kuwa mbunge mkoani Kagera na M/kiti au Naibu kama sikosei CCM Mwanza. Now yupo Marekani
 
Hahaha ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Joan mtoto wa anko wangu mzee Kataraia. Amewahi kuwa mbunge mkoani Kagera na M/kiti au Naibu kama sikosei CCM Mwanza. Now yupo Marekani
Huko Marekani yupo kazini au ameenda likizo kuwatembelea ndugu na jamaa? mbona kwenye list ya wabunge waliowahi kutokea Kagera hayupo? au ubunge gani unazungumzia.
 
Huko Marekani yupo kazini au ameenda likizo kuwatembelea ndugu na jamaa? mbona kwenye list ya wabunge waliowahi kutokea Kagera hayupo? au ubunge gani unazungumzia.
Utakua wa juzi. Bukoba mjini amewahi kuwa mbunge anaitwa Mujuni Kataraia. Marekani kwa wanae. Yupo broke vibaya mno kwa sasa.
 
Reactions: Qwy
Hii nchi kuendelea itakua ngumu sana; asimilia kubwa ya wakurugenzi wanaotokana na wanasiasa mara nyingi kama siyo zote wanatumia muda mwingi kujipanga namna ya kupata jimbo uchaguzi ujao kwani wengi walikua ni washiriki kwenye mchakato wa uchaguzi uliopita.
Hii ni tofauti na watumishi walioteuliwa kua DED; sijajua nia hasahasa ya viongozi wanafanya teuzi ni wananchi kupata maendeleo au yeye kuendelea kubaki madarakani?
 
Utakua wa juzi. Bukoba mjini amewahi kuwa mbunge anaitwa Mujuni Kataraia. Marekani kwa wanae. Yupo broke vibaya mno kwa sasa.
Sorry! nilielewa kua Joan ndiye yupo Marekani na ndo aliwahi kua mbunge. Basi ungesema Joan ni mtoto wa Mbunge staafu wa Bukoba.
Asante nimekuelewa; vp Mh DED yeye anafanya mishe gani hapa mjini
 
Sorry! nilielewa kua Joan ndiye yupo Marekani na ndo aliwahi kua mbunge. Basi ungesema Joan ni mtoto wa Mbunge staafu wa Bukoba.
Asante nimekuelewa; vp Mh DED yeye anafanya mishe gani hapa mjini
Ah! Kweli imebidi nisome upya. Sikua nimeandika vema kweli hapo mwanzo kumuwia mtu ugumu kuelewa.
Joan alikua active na UVCCM sidhani aliwahi kufanya kazi sehemu. Ila ni humble sana na si mtoto kama wengi wanavyodhani.
Ila kwa hii nafasi hata mie natia shaka. Siwezi kusifia tu kisa nina nasaba naye. Namna hiyo tunaua nchi!
 
Waligombea viti maaluma na akina Halima Bulembo pamoja na mzazi mwenzangu mmoja hivi. Ila sijajua kwanini anachaguliwa mtu ambae hajawahi kua mtumishi wa umma/private kwa muda mrefu na mwenye kutolea maamuzi mambo magumu.

Fikiria watu wanavyopiga zile pesa za mikopo ya makundi mbalimbali zinazotolewa na manispaa au halmashauri kwa ajili ya kuinua wananchi ki mapato ndiyo uwapeleke watu kama hawa wakazisimamie.

Akiletewa vocha ya cheki ya 700bil na mhasibu ikiwa bado dk 10 benki ifungwe yeyeatasign tu bila kupitia vizuri.
Maendeleo bado sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ