Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Heeeeeee bhanya bhabya ketaaaaaa🤪🤪🤪🤪🤪, ujinga na upuuzi mtupu. Kumpa mkopo ndo tiketi ya kumtesa na malipo madg ya mshaharaa?

Lisu alisema "TUNA RAISI WA AJABU, NARUDIA TENA, TUNA RAISI WA AJABU SIJAWAHI KUONA"

leo nimekubali, kweli TUNA RAISI WA AJABU SANAAAAAAAAAAAAA. full stop.
 
Sasa wangekuwa wanalipwa wangekimbia?
Inawezekana wanalipwa vizuri lakini mazingira yote ya kazi hayafai, ukitembelewa na DC , Waziri, Katibu mwenezi unaanza kuulizwa maswali kama mtoto na ukimkera kwa majibu hata kama upo sawa unawekwa ndani saa 48. Kuna watu walikuwa wanaondoka private sector na kwenda serikalini sio tu kwa kufuata malipo mazuri lakini kwa sababu mbali mbali kama :

1. Frusa za kujiendeleza kimasomo.
2. Usalama wa kazi (Job Security) na kuheshimiwa.
3. Manufaa kama bima ya afya, nyumba ya kuishi etc.
4. Muda rafiki wa kufanya kazi.

Je hivyo vitu navyo vimeboreshwa au ni mwendo wa bakora tu.
 
Hata kama alisomeshwa na serikali, bado ana uhuru wa kuchagua. By the way, huko private bado ana tibu Watanzania hao hao. Na analipa mkopo wake hakupewa bure.
Huyu baba sasa atafutiwe jina..
 
Lbd anatibu kuku, alafu et hana uzalendo. Hiv huyu mzee anaujua uzalendo kweli?? Kwani huyo daktari amekimbilia malawi kuwatibu wamalawi au ? Raisi mjinga kweli huyu. Anazeeka vibaya kweli. Nahis bora m7 anajua kuchanganua mambo💥
 
Hapo weka kama 40% makato maana yake take home ni almost laki saba.

Kodi ya nyumba, umeme, maji, fuel (kama ana gari), ada ya watoto, chakula cha familia, kufanya maendeleo etc.

Lazima mtu upagawe.
 
Rais Magufuli leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”-JPM

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”-JPM

My take:
Kuna maslahi madogo hasa ya kimshahara katika utumishi wa serikalini, naomba serikali iongeze mishahara kwa watumishi ili kuepukana na changamoto hii. La sivyo serikali itaendelea kupoteza mapato kwa watu kukimbia utumishi wa umma serikalini.
 
Daktari aliyeajiriwa mwaka Jana kwa ajira za kutafutia kura kabond lini na serikali?
 
Kuna mzee wangu mmoja hapa ni shabiki sana wa magufuli ila toka afungue kinywa chake na kuzungumzia corona. Huyu mzee nikimuuliza vipi umesikia hotuba ya magu anajibu kuwa jamaa kama vile majukumu yamenzidi ameanza kuwa mwehu sasa
 
Hili waimba mapambio watakutoa macho.
 
Ingekua sahihi kama angaelipa kwanza 100% ya mkopo wa Serikali aliokopa na riba yake ndio atoke
Hakuna kipengere kwenye mkataba wa mkopo kinachosema kuwa ukimaliza Basi ufanye kazi serikalimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…