Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Hapa ndipo nilipokuwa napataka! Kwa mtazamo na kauli hii ya Rais ni dhahiri kuwa mikopo ya elimu ya juu inapaswa kulipwa kupitia utumishi/ajira ya mnufaika serikali na si sekta binafsi. Yaani aliyesoma kwa mkopo wa serikali hapaswi kuajiriwa kwenye sekta binafsi.
 
What if alichukua mkopo?

We dont have any facts to ramble on about the case

Former employer, the President, may have had the background before he spoke
Background gani kila siku anaongea then anabadilisha maamuzi,Yule aliyenunua gari kinyume na utaratibu,Pm,Jafo na yeye mwenyewe walipiga kelele kibao,juzi kamrudisha kwa mbwembwe zote,Pm na Jafo wataficha wapi sura zao? Ni mengi anayasema Ila hasimamii sheria....
 
Hiyo hufanyika kwenye seriously private institutions, but kwenye ile form ya mkopo haina vipengele hivyo mkuu! Na hiyo serikal yetu hakuna vipengele kama hivyo. Mbona walimu weng sana wanahamia huku private schools na hakuna wa kulalamika🤫💥
Ndio maana nikakwambia inategemea na nafasi, sasa mtu keshakuwa experienced Dr na hiyo experience kapewa na serikari jumlisha na elimu yake iligharamiwa na serikali halafu asepe tu.

It’s not hard to train a teacher or replacing one uitaji kumuwekea ‘restrictive covenant’ kwenye mkataba wake. But a doctor is another story it takes time and money to train one and they become more valuable with years of experience.

Halafu experienced Dr asepe tu kirahisi rahisi bila ya ridhaa ya mwajiri wake ilo kwakweli hapana atapike hela za serikali; kwanza sio kitendo cha kiungwana wala kizalendo.
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Kwani hiyo mikopo wanapewa bure?
Si kuna sheria inayo wataka mulipa hiyo mikopo?
 
Kuna watu/ wafanyakazi wakienda masomoni, wanawekeana bond na mwajiri/ serikali tena kwa viapo mbele ya shahidi mwana sheria kuwa akimaliza masomo lazima arudi hapa kwenye kituo cha kazi afanye kazi miaka mitano ndipo ahame kutafuta marisho ya kijani ama aendelee pale. Na wanafanya hivi kwa sababu mfanyakazi wao huyo anakuwa analipwa mshahara akiwa kwenye likizo ya masomo. Sasa akimaliza masomo na akasema anatafuta marisho ya kijani mbuga nyingine, bond inamlazimisha kulipa gharama/ stahiki zote alizolipwa akiwa masomoni.

Tukirudi kwa ndugu yetu daktari. Je. Alikuwa na bond na serikali !?
Hapana
Na hakuna sheria ya kuwaadhibu hao watu.
 
Wafanye kama Cuba wanaingia nao mkataba mapema ni waajiriwa wa serikali wanapopokea mkopo wa masomo tu.

Ukienda kufanya kazi private hiyo hospitali inabidi iingie mkataba na serikali yao na kuwalipa asilimia kadhaa ya mshahara wako kila mwaka. Brazil na Venezuela wanaotegemea madaktari wa Cuba ndio wanavyofanyiwa.

Ikitokea daktari bingwa ndio kabisa yaani wakusomeshe, wakupe na experience mpaka uitwe bingwa mtu anaemtaka lazima alipe dau kubwa zaidi; that’s how Cuba manages to keep their highly skilled Drs wanaopokea mishahara midogo compared to the world.
Na serikali inahakikisha wanapata kazi hata nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom