Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Huu ni upumbavu, Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake.....kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu...........what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mkopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.

Hizo ni signs za depression na kukata tamaa! He’s dying slowly!
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”

Hapa kapiga mochwari
 
Rais Magufuli leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”-JPM
“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”-JPM

My take.
Kuna maslahi madogo hasa ya kimshahara katika utumishi wa serikalini, naomba serikali iongeze mishahara kwa watumishi ili kuepukana na changamoto hii. La sivyo serikali itaendelea kupoteza mapato kwa watu kukimbia utumishi wa umma serikalini.
Uonezi

Alikopa, analipa riba ya mkopo,
 
Ingekua sahihi kama angaelipa kwanza 100% ya mkopo wa Serikali aliokopa na riba yake ndio atoke
Mnatetea kila kitu wakuu..kwani kuna makubaliano kwamba ukikopeshwa mkopo wa masomo ufanye kazi na Serikali? Mbona tukisema ajira hakuna mnatuuliza lini serikali iliingia mkataba wa kutoa ajira kwa wasomi wote?
 
View attachment 1689777
wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”

Mchango gani tena zaidi ya kulipa Kodi ya mapato?
Serikali haina pesa, pesa ni zawalipa kodi cha msingi aliyekopeshwa alipe deni lake basi inatosha tofauti na hapo Rais nae ana sifa za hao mabeberu anaowaponda majukwaani kila siku.
 
Na serikali inahakikisha wanapata kazi hata nchi nyingine.
Cuba hawana shida kutoa madokta wao provided mwajiri anapeleka maombi kupitia serikali yao; mnaingia makubaliano unapewa hao wataalamu.
 
Ndio maana nikakwambia inategemea na nafasi, sasa mtu keshakuwa experienced Dr na hiyo experience kapewa na serikari jumlisha na elimu yake iligharamiwa na serikali halafu asepe tu.

It’s not hard to train a teacher or replacing one uitaji kumuwekea ‘restrictive covenant’ kwenye mkataba wake. But a doctor is another story it takes time and money to train one and they become more valuable with years of experience.

Halafu experienced Dr asepe tu kirahisi rahisi bila ya ridhaa ya mwajiri wake ilo kwakweli hapana atapike hela za serikali; kwanza sio kitendo cha kiungwana wala kizalendo.
Mbona wanasiasa wanakula hela za serikali za kila siku mnawaacha. Si jana kasamehewa alonunua gari la anasa na zahanati hazina ambulance.
 
Kule hawatibu watu ?

Wanadaiwa ?, Wamelipa hawajalipa ?, kuliko kufungia hospital / mtu anayetibu watu pia ni rahisi sana kwenye mkataba wa mkopo waseme kwa miaka kadhaa lazima ufanye kazi ya serikali sehemu yoyote utakayopelekwa (hapo mtu anakuwa anabanwa kwa mkataba) sio aina hii ya sheria / maamuzi kutoka kwenye kinywa cha mtu
Nafikiri hichi kitu kipo na wanafunzi wa Udaktari huwa hawapewi mikopo bali grants hawalipi. Ila kunakipengele cha kufanya kazi 5 yrs.
 
Cuba hawana shida kutoa madokta wao provided mwajiri anapeleka maombi kupitia serikali yao; mnaingia makubaliano unapewa hao wataalamu.
Sasa sio kosa la daktari. Kama serikali haina huo utaratibu ni tatizo la serikali.
 
Majengo, vifaa tiba inabidi yaende na maslahi kwa watoa huduma. Ni sawa na kupaka rangi gari ila kutoweka oili katika injini. Itafika mahala itakwama.
Mtu anapelekwa sehemu anacheleweshewa stahiki.
Watawala, watunga sera wakipewa nyazifa wanapewa stahiki ikiwa ni pamoja na mishahara mizuri, magari mazuri na makazi mazuri pamoja na ulinzi.
Sekta ya Afya inaitambua huduma za idara binafsi na inahudumia watanzania hao hao.

Kuna watu wengi wanahitaji ajira waajiriwe hao kwa mshahara wa mtu aliyeondoka.
Vitisho kwa watumishi vitasaidia kwa muda ila madhara yake kwa ujumla ni makubwa. Kuna vitu havihitaji hisia bali hekima.
Uzalendo si kunyenyekea tu hata kutumia ubongo na kutengeneza maslahi bora ni uzalendo. Si afya kwa taifa kuwa na watu woga wanaoshindwa kujieleza.
Nchi ya watanzania ni ya wote tupendane.
 
Huu ni upumbavu, Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake.....kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu...........what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mkopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.
On the positive side:
Alitakiwa kutambua kuwa wanapolalamika maslahi yao kuwa madogo wanamaanisha.
Wameona wanapuuzwa maeamua kwenda kwenye unafuu.
Halafu huwezi kuiwajibisha hospital binafsi kwa kumuajili mtu,mission ya hizo hospitali ni huduma bora ili biashara iwe viable.
Kama hawezi kufikiria badi aombe msaada wa fikra.
 
Ndio maana nikakwambia inategemea na nafasi, sasa mtu keshakuwa experienced Dr na hiyo experience kapewa na serikari jumlisha na elimu yake iligharamiwa na serikali halafu asepe tu.

It’s not hard to train a teacher or replacing one uitaji kumuwekea ‘restrictive covenant’ kwenye mkataba wake. But a doctor is another story it takes time and money to train one and they become more valuable with years of experience.

Halafu experienced Dr asepe tu kirahisi rahisi bila ya ridhaa ya mwajiri wake ilo kwakweli hapana atapike hela za serikali; kwanza sio kitendo cha kiungwana wala kizalendo.
Kwani mkuu kama ni hizo hela si bado anailipa serikali? Kwan amelikimbia deni? Na kama mnajua kumpata daktari tena ni kisanga, sasa kwanini hamyathamini maslahi yao? Kwann hamwathamini??? Alafu daktar alichokifanya amehamia kituo kingne tu ila jukumu atakalolifanya huko aliko n sawa na ambalo angelifanya akiwa serikalin!

Waswahili husema, huwezi kujua umhimu wa tako mpk upate majipu matakoni ndo utajua kumbe tako lina umhimu sana!
Alafu kwani wale walimu wanaofundisha st Francis girls wametoka Kenya?

Private institutions zishajua udhaifu wa serikali thus y wanatembea mle mle. Serikal ipandishe masilahi uone kama hawatatoka huko sekita binafs kuja serikalini.
Mnajifanya hamjui tatz et
 
Back
Top Bottom