Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Yani naingia ndan kwako nakuibia alafu nakurudishia tena mi mwenyewe alafu unanipa hongera sana duh acha wazungu waendelee milele Pierre liquid anasema wazungu watabaki juu kabs mawinguni milele


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Na ndiyo mwajiri namba moja aunaweza kuchukua maamuzi magumu.Nani alikudanya, subiri 2025 ikipendeza hadi 2030
 
Neno zuri. Hii kama vile ni promotion iliandaliwa kwa ajili ya kuja kuleta shida kisha itatuliwe but ukweli kaongea mazuri na amejiongezea credit kiasi kwa watumishi.
Watumishi waanze kulipwa zote kama wabunge tu. Ni jukumu la mifuko ijiimarishe haraka ktk kipindi hicho cha mpito ili mfumo mwingine uanze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye ndiyo anawatumia viongozi wa vyama kisiasa
 
Sijasikia wakiongelea fao la kujito je nalo linaendelea kama kabla?
 
Leo nimeamini kuwa umoja ni nguvu baada ya watumishi wa umma kusimama kwa nguvu zao zote kupinga wizi wa mchana kweupe uliokusudiwa kufanywa na serekali ya awamu ya 5 umemfanya jiwe atishike na kubadilika utafikri siyo yeye aliyeasisi wizi huo.

Na wenye kumpongeza wanampongeza wakati alipohalalisha wizi huo napo walimpongeza.
 
Jiwe katika ubora wake [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
2023 kikokotoo kitatupa wastaafu 70%.

Good riddace Dr Magufuli. Yaani yule shosti w SSRA alikuwa anaita madai ya wafanyakazi kelele, kelele...🤬🤬🤬🤬
yule sijui dr Irene Isaka kanibowa sana, anaita kelele.. nilitamani ningekuwa karibu achezee makofi kidogo
 
Wengi hawajui kama jamaa kafinyanga hili zimwi mwenyewe na kaliimba usiku na mchana hadi likaanza kuwatisha watu hadi wameamua kumpigia magoti aliue mwenyewe na kafanya hivyo. Siasa ni sihasaa kweli kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Credit gani? Mwanzon walikuwa wanalipwa kwa asilimia ngap? Yaan utengeneze tatizo kwa makusudi,halafu unalitatua. Mwisho wa siku uonekane jasiri

kwa hiyo unasemaje wewe mwenzetu
 
haya ni maujanja ya jamaa yetu hapo tayari ameshapata mtaji wa kula za wafanyakazi 2020, mwanasiasa mjanja ni yule ambaye anayecheza na hisia za watu anaowatawala hili amefaulu bado mengine sasa.
 
*Hongera JPM kwa zawadi hii ya mwaka mpya wa 2019*

Na Daniel Mjema

Si kawaida yangu kupongeza pasipostahili kupongeza au kukosoa pasipostahili kukosoa, ila leo kwa dhati ya moyo wangu, nakupongeza Rais wangu John Pombe Magufuli au JPM kwa hili la Kikokotoo, kwa kurejesha 50% kwa mifuko iliyokuwa ikitoa 50 na ile ya iliyokuwa ikitoa 25% ibaki hivyo hivyo na 25% katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023.

Nimekusikiliza hatua kwa hatua, na kusoma lugha ya mwili wako, hakika umejiweka kwenye nafasi ya mfanyakazi, na kuyabeba machungu na maumivu ya kiakili na kisaikolojia waliyopitia tangu kutangazwa kwa kanuni mpya ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Nasema asante Rais wangi.

Nimefurahi zaidi ulipowaeleza wabunge wetu ukweli mchungu kuwa kama sheria hii ya 25% ingepelekwa Bungeni kuwahusu wao, hakika wasingeipitisha. Rais umesimama katikati ya wafanyakazi wa taifa hili. Umezungumza kama Baba.

Ni jambo ambalo lilikuwa haliingii akilini, na wewe umesema halileti logic, kwamba nimetumikia nchi kwa uaminifu mkubwa, ninapostaafu unanipa 25% halafu unaniambia hizo zingine nitakupa kidogo kidogo hadi ufe. Sielewi wasomi wetu wanafikiri kwa ubongo gani.

Ninapostaafu, na pengine kwa uaminifu wangu sijaweza kujenga hata kakibanda, natakiwa nikalipe kodi, nisomeshe watoto, niachane na gari ya umma nipande daladala, sasa nilitaraji hiko nilichojikusanyia kingenisaidia kuweka hata kakibanda au kabiashara, unaniwekea masharti magumu, ambayo wakati najiunga na mifuko hukuniambia.

Ndio maana nasema asante sana Rais wangu JPM. Sasa tutakula mwaka mpya kwa raha mustarehe hadi lile jino la Krismas litaonekana. Asante Rais wangu, ile stress ya miezi kadhaa waliotupa hawa watu wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa inaondoka.

Lakini baba, usimame hivyo hivyo ili kipindi cha mpito kikimalizika 2023 wasije tena na hadithi za ujanja ujanja au za Alinacha au Abunuasi ambazo hazina maslahi kwa mfanyakazi anapostaafu. Wewe ni Rais wetu, kwa hili nasema asante sana ila mishahara sekta binafsi kwa baadhi ya sekta ni hairidhishi na ndio msingi wa mahesabu. Wakija hiyo 2023, waje pia na fomula ya mishahara na kikokotoa.

*Mungu akubariki*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale Mganga wa kienyeji anapomroga mtu kwa kutega dawa njia panda,kisha kuja kumtibu mwanakijiji huyo.Na kwa shukrani nyingi,mwanakijiji anampelekea mganga mbuzi ili ale.
Mtaishia kusema hayo hayo muda unawaishia JPM hana mpinzani, kama wapinzani wenyewe wanashindwa hata kutiii mahakama, hadi wanafuttiwa dhamana, kweli mapunguani totoro. JPM kapindua meza kama bwana yesu kwa waliofanya nyumba ya bwana pango la wanyang'anyi
 
Kwanini katatua hilo tatizo jamani, UFIPA watamponda wapi Raisi wetu Mpendwa MAGUFULI kwa majungu yasiyo na tija?

Sent using Jamii Forums mobile app
Alitengeneza tatizo akijua atalitatua yeye ili ionekane ni Rais wa watu na kutafuta sifa za kijinga

Hii ndio itakuwa habari ya ufipa
Nyingine

Alikuwa anajaribu, pasingekuwa hashtag zetu alitaka afanye hizi pesa za wastaafu kma zile za bukoba na 1.5 trion zetu.

Tutegemee hizi komenti sana wiki hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wote tutakaostaafu 2023 tunakupongeza mheshimiwa ila tunaomba aliye kuja na wazo la 25 percent afunguliwe mashtaka ya attempted muder maana wengi wetu pressure zimepanda !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…