Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Credit gani? Mwanzon walikuwa wanalipwa kwa asilimia ngap? Yaan utengeneze tatizo kwa makusudi,halafu unalitatua. Mwisho wa siku uonekane jasiri

kwa hiyo unasemaje wewe mwenzetu
 
upuuzi mtupu matatizo utengeneze wewe halafu ujifanye kutatua wewe... nitaendelea kukuona mjinga sana ukiomba tena nafasi 2020
 
Wengi hawajui kama jamaa kafinyanga hili zimwi mwenyewe na kaliimba usiku na mchana hadi likaanza kuwatisha watu hadi wameamua kumpigia magoti aliue mwenyewe na kafanya hivyo. Siasa ni sihasaa kweli kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha mbona kikokotoo kilipopita upinzani ndiyo walilalamika sasa maamuzi yamechukuliwa kwa wakati mnaanza kulialia, Upinzani Tanzania hakuna yamebaki majigambo tu

Hiyo inaitwa chukua maamuzi magumu kwa wakati.Hongera JPM kura yangu 2020 kwako
 
Pamoja na kwamba jana walijifanya kuongea na waandishi wa Habari,.....

Huu ndio sasa ujumbe kamili na maalum kwa wafanyakazi wote kwamba huyu ndiye jiwe imara lilokuwa nimeamua na kuhakikisha swala LA kikokotoo kuwa 25% linabaki na lazime lipite na litekelezwe full stop.

Our worst enemy is our own servant.. you can't believe this... Why praying for you???? And why not cursing and bewitching you???
Hebu rudia tena kusoma utumbo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hayo ndio mambo sasa.. wastaafu watakula kuku kwa mrija.
 
Regardless ya nani kutengeneza tatizo na nani kalitatua, bado tuna kitu cha kupongeza kwa maamuzi haya.

Pia naomba FAO LA KUJITOA liwe nalo limerudishwa.
 
UPDATES:



Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wametoa historia ya walikotoka hadi walikofika. Aidha, wamedokeza kuwa wapo waliozimia kwenye ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Rais Magufuli anawasikiliza na anataka kila mtu aongee na kutoa dukuduku ili aweze kuongea.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi (upande wa walimu) wanadai kikokotoo kimekuwa ni suala kubwa na Rais Magufuli kama mwalimu anatambua changamoto za walimu. Wanamwomba Rais aliangalie suala la kikokotoo kwa jinsi atakavyoweza kwakuwa wanajua anaweza na kwa wanavyomsaidia Mungu atamsaidia alitatue hili.

TUGHE: Tunakupongeza Mhe. Rais, lakini tunapenda ufahamu kuwa wastaafu wengi hawakuwa wameandaliwa na mabadiliko haya yametokea ghafla na kusababisha negative impact. Morali ya kazi imeshuka!

Waziri Mhagama
Hoja na kuunganisha mifuko ilikuwa ni hoja ya wafanyakazi.

Hapa tunazungumza tu kikokotoo, ili tupate kikokotoo lazima turudi kwenye contribution rate, tukitaka tuendelee na kikokotoo cha 50% contribution itabidi itoke kwenye 20% hadi 25%.

TUCTA: Tunafahamu kwa moyo wako na unavyowasaida wanyonge. Tunaamini utasaidia kutatua

Mwanzo Wastaafu walikuwa wanapata 50% kwa mkupuo na 50% kidogo kidogo kila mwaka

Tulipendekeza mkupuo uwe 40% na si 25%


CHAMA CHA WALIMU: Suala la kikokotoo ni shida, hakuna asiyejua shida za waalimu. Uzuri ni kwamba hata wewe Rais ni Mwalimu

Kwasasa hata mishahara ya mwisho wa mwezi haitoshi. Kwa namna unavyofanya mambo makubwa najua hata hili unaliweza


TUGHE: Wastaafu wengi hatukuwaandaa kisaikolojia. Mabadiliko haya ya kikokotoo cha mafao yametokea kwa ghafla sana.

Wafanyakazi wa umma waliowengi wanalalamika nakuomba mheshimiwa Rais uongee chochote ili Wafanyakazi warudi kwenye morali ya kazi

TUICO: Watu wa sekta binafsi kima chao cha chini ni 100,000. Ili kwenda vizuri kamati itakayoundwa ikachunguze hii mishahara

Pia kuna fao la kupoteza ajira hawalipwi na makampuni mengi yanaondoka bila ya kuwalipa


WAFANYAKAZI WA RELI: Tumepitia misukosuko sana ikiwemo mishahara kuwa kidogo na ulipwaji wake ni wa kusuasua sana

Tulitegemea mafao ya kustaafu yatusaidie kujenga nyumba ili hata tukifa tufe vizuri.

Ile 50% ya awali kama haiwezekani basi tunakubali iwe 40%


TAMICO: Kwenye suala la kikokotoo kuna shida hasa kwenye fao la kujitoa ambalo mbadala wake ni fao la kukosa ajira

Sekta binafsi tunapata shida kwasababu kazi zetu si za muendelezo. Tunaomba iwepo tofauti kwa watu wa sekta ya migodi na ujenzi kwenye fao la kukosa ajira


SERIKALI ZA MITAA: Tunapenda mifuko iwe imara lakini kwa mishahara yetu hii midogo kwa kweli inaumiza

Rais kelele ni nyingi sana, na kwa kikokotoo hiki mfanyakazi akistaafu atashindwa hata kujenga


CHAMA CHA WAAJIRI: Sheria hii ya mifuko ya jamii, ililenga kuiweka mifuko hii kuwa katika hali ya usawa

Baada ya mifuko kuunganishwa uchangiaji umekuwa ukitofautiana kutoka mfanyakazi mmoja hadi mwingine.

Kila mfuko una tafsiri yake ya mchango wa mwanachama


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Nimeamua niwaite wote ili niwe referee na inawezekana nikawa refaree mbaya

Nisingeweza kuwaita Wafanyakazi wote na tatizo hili naona litafikia mwisho.

Rais Magufuli: Kwenye baraza la Mawaziri tulikubaliana kuinganisha mifuko ya jamii

Hatua hii ilitokana na maombi ya muda mrefu ya vyama vya Wafanyakazi kutaka mifuko iiunganishwe

Watu walijua inaelekea kufa na kweli ilikuwa inaelekea huko

Nimewasikiliza, hapa tunaweza kuongea ikafika jioni. Tunaweza kunaliza yakaletwa mengine na ndio maana nataka tu concentrate sehemu moja. Ndio maana nimeleta regulator ili watoe mawazo yaliyo academic.

Nilipokuwa mwalimu nilianza na mshahara wa 1045, ninapofanya kazi nikataka kustaafu nianze kupata usumbufu naomba sio vizuri ndio maana nimewaita hapa tuzungumze.

Mtakumbuka tarehe 20 Oktoba 2017 baraza la mawaziri tulipitisha kuunganisha mifuko ya kijamii iwe mmoja kwabajili ya watumishi wa umma na NSSF ifanyiwe marekebisho ili iwe kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta binafsi.

Sababu ya kuunganisha mifuko hii ni kwamba watu walijua inakwenda kufa na kweli ilikuwa inakwenda kufa.

Kabla ya mifuko kuunganishwa kila mfuko ulikuwa na wanachama wake. Jumla ya wanachama wote ilikuwa milioni 1.2.

Awamu ya tano mifuko ilikuwa hali mbaya na walikuwa wanapigana vita na kugombania wanachama.

Hii mifuko pengine ilikuwa inaendesha kiajabu ajabu. Miradi mingi ikawa inaanzishwa hasa ya majengo. Nenda Dege Eco Village, Kigamboni uangalie majengo yale sasa mwekezaji alikuwa anategemea return gani?

Tulipoingia madarakan tulikuwa deni kubwa la trilioni 1.2, ikabidi tutafuta pesa Serikalini tukaanza kulipa madeni haya na tumelipa yote mpaka March 2017.

Rais Magufuli: Sheria inawataka wapewe kidogokidogo si bora unipe zote nikafe vizuri

Mtu anafanyakazi yake kwa muda wote, halafu anamaliza unamwambia apewe asilimia 25, haiingii akilini. utanipa kidogokidogo? hata Waziri akimaliza Ubunge wake ukimwambia utampa 25% kisha nyingine kidogo kidogo hawezi kukubali

Kuna challanges ambazo hatuwezi kuzikwepa kwenye mifuko hii na ninyi wenyewe mmesema kuwa matatizo yapo

Ni lazima kuzitatua changamoto hizi, mmesema watu wanapenda #Kikokotoo kitoe angalau 50% ya mafao kama ilivyokuwa hapo awali

Wakati wa kuunganisha mifuko wastaafu walikuwa wanadai bilioni 700 na zaidi ya bilioni 500 zimelipwa.

Hii fomula iliyotumiwa na PSPF na NSSF haipo duniani.

Walioiweka ni makatibu wakuu wa wakati ule, sio wakati wangu

Rais Magufuli: Niombe kwenye mifuko waboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa

Kama tulikuwa na wanafunzi hewa, watumishi hewa, pembejeo hewa hatuwezi kukosa wastaafu hewa

Rais Magufuli: Hifadhi za Jamii zipunguze matumizi ya hovyo, zikiwa fedha za Wastaafu zinatakiwa kulipwa kwa mkupuo hata wa 60% haitawezekana kwasababu hakutakuwa na hizo fedha

Yawezekana tatizo halianzi kwenye kikokotoo bali hata uendeshwaji wa mashirika haya

Nafahamu shirika moja linalotumia bilioni 1.3 kuchapisha kaenda na matangazo. Wanachama hamuwezi kujua kama fedha zenu zinatumika hovyo

Limeajiri walinzi na kuwalipa bilioni 2 kwa mwaka, kama wangeajiri SUMA JKT wangelipa bilioni 1

Nitoe wito kwa watendaji wakuu, tupunguze gharama za uendeshaji wa mifuko. Sasa imebaki mifuko 2 hakuna sababu za kushindana

Wafanyakazi wa Serikali ambao ni wanachama wa NSSF wahamishiwe PSSSF na wale wa sekta binafsi vivyo hivyo

Mashirika yaanze kuangalia namna ya kuongeza wanachama sioni sababu ya NSSF kuwa na wanachama laki nne nchi nzima wakati sekta binafsi inakuwa kila siku

Wale wafanyakazi wa migodi na ujenzi kuna sababu gani ya wao kusubiri hadi miaka 60 wakati kazi zao ni za kipindi kifupi.

Tuongeze option za wanachama. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima lazima mstaafu awe respected

Mwalimu aliyefundisha kwa uaminifu miaka 40 hadi chaki zimemharibia macho na aliowafundisha wamekuwa na mishahara mikubwa na wengine ndio wakurugenzi wa NSSF

Ukitaka kuchukua mafao yake unamwambia nitakupa kidogo ili ukaishi, aliyekwambia nani ataishi?

Nimeamua tuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kikokotoo kilichokuwa kinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha miaka yote ya mpito

Kipindi cha mpito ni hadi mwaka 2023 ambapo wanachama wa mfuko 58,000 ndio watastaafu kipindi hicho.

Wanachama watakaokuwa wanastaafu wataendelea na kikokotoo cha 50%

Rais Magufuli: Mimi nitaichungulia hiyo mifuko na nina uhakika Waziri na Katibu Mkuu wa wizara zinazohusika wafuatilie mifuko isitumike hovyo

Katika kipindi hicho watawalipa watu mafao vizuri na kwasababu hali itakuwa imeimarika tutafanya mazungumzo ya mfumo bora

Niakubaliana kuwa si kweli lengo langu mifuko, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Si kweli kwamba lengo langu mifuko ife, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae pamoja mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Viongozi wa wafanyakazi muache kutumiwa na wanasiasa, watakaotumiwa na wanasiasa wataondoka

Mafao yakiwa bora hata wizi na ufisadi utapungua, kwasababu kila mmoja atakuwa anajua kuwa akistaafu atapata fungu lake

Hongera Bulaya, marehemu bilago na jmyika kelele zenu zimewaogopesha hawa wezi, ndo umuhimu w demokrasia
 
Tembeeni kifua mbere tena mkiwa mmevua mashati.. tupo kweny “rait traki”..[emoji1]
 
Mwaka 2012 Sister Irene +(Dau) wa SSRA alikazania sana jambo hili kama leo alivyoshupalia lakini wenzie macho yao yote yalikuwa kwenye mwaka 2015 na mwisho wa siku ikaahirishwa na watu wakalamba, leo hoja ikiwa ni ileile, Irene yule yule wa SSRA, Waziri huyo huyo na wenzie ni hao hao wanaosubiria 2020 kwa dukuduku lao moyoni... na leo ngoma imeahirishwa tena hadi 2023, Angalizo ni kuwa Irene anaweza kustaafu akaacha mambo yakiwa hivyo hivyo kwani interest zake ni tofauti na za wenzie
Na kuna kila dalili Irene akatumbuliwa anytime!
 
Toka lini wapinzani wanaongoza Tughe, tucta,cwt, pspf,nssf n.k maana hawa ndo waalialikwa ikulu kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye akili wanaelewa kinachoendelea ...kwa hili/sasa Hongera JPM.!Politics is defined as ..Who get what ,when,where and How
 
WALE UVCCM WALIOKUWA WANAPONGEZA SHERIA HII KANDAMIZI NA KUWAZODOA WOTE WALIOIPINGA NAPENDA KUWAPA POLE. ILA MNARUHUSIWA PIA LEO KUPONGEZA
Nchi imepata rais sahihi asiyeangalia chama chake kina msimamo gani, yeye ni problem solver wa wananchi bila kujali vyama wala dini
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]



HII SERIKALI INAONA WATU NI MATAIRA SANAAA... HAYA BABA TUMEKUSIKIA WEWE NDO MKOMBOZI WA WAFANYAKAZI!

UNATENGENEZA TATIZO ALAFU UNALITATUA HII NDO TZ YA VIWANDA..!!
ujingaaa ujingaaa tuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom