raha sana! ukiwa umeajiriwa na serikali au shirika la umma wewe ni kama mtoto wa familia bora usipolizika unajiliza kisha baba anakuja kukubembeleza!
sasa njoo huku sekta binafsi ikiwa mshahara 300,000 ni hiyo tu na haitegemei kupanda na hakuna huduma zingine kama matibabu
changamoto ya maisha haya inakuja pale kazi inapokwisha uishi maisha binafsi kama haukujipanga na kwa bahati mbaya ulikuwa na kipato kidogo na nyongeza ulichelewa kuoa na kujenga familia hivyo mtoto wa kwanza yuko form two!
hivyo nawashauri tumieni fursa ya kuajiriwa kukopa na kuwekeza sio kununua vigari kila kukicha hatuoni wivu lakini ndo ukweli tulioko huku tunaona fursa mnazo sana kuzidi mnavyofikiria.
hivi kuna tabu gani ukakopa ukanunua bajaji ukatumia kama 7,000,000/- mpaka 8,000,000 kwa siku ukapata 20,000 ambazo kwa mwaka ukapata 7,200,000/- inayotosha kusimamisha nyumba ndogo ya kupangisha ya vyumba viwili mpaka linta? tutaendelea nina mteja kwanza