Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Namkumbuka Kinana, alisema Kuna mawaziri wengine ni mizigo. Hata huyu waziri wa sasa ni mzigo kwa taifa.
 
Kabisa Mkuu wamechota trillions 8 hawataki kuzilipa na kwa unafiki wake hakuzisema hizo. Inawezakana kabisa kulipa wastaafu 75% ya mafao kwa mkupuo ikiwa tu Serikali italipa deni lake lote na kuacha kabisa kutumia pesa ambazo si zao.

Hakuna jipya hapo maana pesa zote za mifuko ya hifadhi ya jamii pesa zote ashazitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aache kujikuta mwokozi kana kwamba ye Yesu
 
Hahaha silaha ndo hizi hizi mpaka unaona anahangaika kujibu sasa hivi ujue 2020 atapata tabu sana
 
Itategemea kama Lissu atakubali maana 2020 ashatabiriwa!!
 
Naunga mkono maamuzi ya busara ya Mh Rais Magufuli. Hata hivyo naona kauli yake imechelewa kidogo. Binafsi nilitaraji kusikia msimamo huu mara tu baada ya malalamiko ya wafanyakazi kuanza kusikika. Hata hivyo, Waswahili wa Ulaya wanasema better late than never. Hongera Mh. Rais.
 
Wenzetu wa visiwani Znz kuanzia mwaka 1990 mpaka 2000 hawatasahau madhira ya serikali ya komandoo salmin amour. Komandoo alikuwa hana tofauti sana na matendo anayofanya Magufuri isipokuwa yeye alikuwa akimtuma Naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna kuharibu Sheria na kanuni kisha yeye (komandoo) atafute ufumbuzi ili kujiijenga kisiasa. Ikumbukwe huyu Shamhuna alithubutu (kwa kutumwa) kufanya siasa za fitna na ubabe hasa kuleta dhana ya uunguja na upemba kiasi kutaka kuikanyaga katiba ya Znz ili Komandoo aitawale milele kwa manufaa yao. Ndiye huyu bwana anachokifanya na bahati mbaya waTz tuna kaujinga fulani cha kutokuwa na kumbukumbu ya matendo ya Viongozi ili kujua dhamira yao. Sasa hivi hatukumbuki vita yake na TEC maana angefanikiwa pale utawala wa sheria tungeusikia kwa Nchi za wenzetu
 
Haijachelewa mkuu maana ulikuwa bado mswada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu sijui akili zenu mnawekaga wapi? Yeye ndiye aliyepitisha baada ya kuona hali mbaya akaamua kujifanya kama hajui kinachoendelea!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya hao wabunge wa CCM waliokua wanakubali hicho kikokotoo kipya itakuaje ni wazando au upinzani ndio wazalendo
 
Nasikia utekelezaji wa 25% ulianza Aug na kuna Mama alienda kuchukua 50M akajikuta anapewa 25M akazimia.Sasa baada ya Rais kubadili hiyo,Je! Yule Mama atapewa 25M yake iliyobaki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…