Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Uchaguzi umekaribia tunapaka girisi kidogo
 
Nimekua nikishangaa ukimya wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi hasa TUCTA pale wanapokua wanasifiwa na Rais Magufuri kua ndo aina ya viongozi anawaowataka nikashangaa kweli yani wewe uombe kura kwa kua utaenda kutetea maslahi ya watumishi na ulipwe vizuri kisha uufyate ukae kimya hadi wabunge waupinzani na watumishi wapaze sauti zao alafu Leo bila aibu Rais anatengua 25% Viongozi wa TUCTA,Cat,Tughe wanashangilia hadi wengine wakitikisa makalio yao kwamba wametetea watumishi je ni kweli wamekua wakitetea watumishi? Kwanza kabisa viongozi wanaopaswa kua ktk trade unions ni aina ya viongozi wenye ushawishi,uharakati na wengi kutopendwa na waajiri....Madai ya watumishi ni Zaidi ya Fao hili la 25%.... Labda niwakumbushe TUCTA wenzao wakina MGAYA na wengine walikua hawafanyi mazungumzo na serikali kwa kujificha zaidi walikua wakiomba wakutane mezani na serikali ilipokaidi walianzisha migogoro hadi serikali ilitii na tuluona mabadiriko....Lakini kwa Miaka hii mitatu ya JPM tumeona TUCTA wakikaa kimya baada ya kusifiwa na JPM kua ni viongozi bora uku serikali ikiwa haitimizi na zaidi kudumaza waajiriwa wake...Baadhi ya Mambo ambayo TuCTA ya sasa haijaweza na serikali kuendelea kukandamiza ni kama:-
1.Serikali kushindwa kuongeza mishaara tokea 2015
2.Serikali kuvurunda kwenye Madaraja ya watumishi yani serikali inaweza ikaamua kupandisha baadhi wengine ikaacha mfano mpaka sasa bado serikali inapandisha wa 2012 na kimsingi ilipaswa kua imemaliza 2016 na sasa ingekua inapandisha walioajiriwa 2014 au walipandishwa madaraja 2014....Lakini watumishi wamezulumiwa haki yao ya madaraja kwa miaka hii ya JPM na mbaya zaidi amedhulumu haki za msingi za madeni yatikanayo na madaraja....Aya ndo mambo ambayo ni ya msingi haingii akili watumishi wanaanza kazi mwaka mmoja,kada moja lakini mishahara yao tofauti na hivyo kupelekea ata mafao yao kua tofauti...Viongozi wa watumishi lazima mjue kua hakuna mahali popote Duniani viongozi wa wafanyakazi wakapendwa na serikali ukiona hivyo basi jueni hamtetei maslahi ya watumishi zaidi mnatetea unyonyaji wa serikali....Miaka 3 bila nyongeza mpo kimya,Miaka 3 madaraja yamekwama mpo kimya then mnaenda Ikulu mnatingisha mawezele kua mmeshinda! Poor You!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Jamaa ana watu na taasisi fulani ambazo huwa anawatuma wafanye kituko fulani ili yeye mwishoni aje aonekane anawasikiliza wanyonge. Alianza Mwakyembe na kanuni ngumu za kuoa akaja yeye kubadilisha. Ni mchezo wa siasa wa kutuchezea tu huu. Maana kama ni uamuzi wa serikali huwa na mchakato mrefu kweli kweli. Iweje awe hajui haya mambo hadi tulalamike? Amesikia Lissu atagombea urais ikabidi ajiongeze. Bado la Katiba Mpya. Atanyooka tu.
 
Kwa mujibu wa ITV, wafanyakazi hao wameandamana chini ya uratibu was vyama vya wafanyakazi. Swali ni lini waliandaa mabango na kibali cha maandamano waliomba lini na hata RC alijulishwa saa ngapi?...inafanana na maigizo!
 
Jiji la Mwanza lilisimama baada ya maelfu ya wafanyakazi kuandamana hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwaondolea kikokotoo cha 25%.
Waandamanaji hao walipokelewa na RC Mongella na wamemuahidi Rais Magufuli ategemee ushindi wa kishindo.

Source ITV habari!
 
Yaaani unavoandika utadhani haupo Bongo hii ya bahati mbaya!!!!! Wahuni washajua huyu mshamba anataka nini, so wanampa bila ajiziiii
 
hayo ni mapandikizi sawa na yale yaliyokuwa yanaimba tuna imani.. na ... oya oya oya!
 
Hiyo sheria 13.7.018,hao ulio wataja ndio waliitia sahihi?acheni kuwapa lawama watu,mtu alitengeneza tatizo mwenyewe kisha asome upepo unavyovuma eti aje na soln aonekane shujaaa!!!???
 
Kumbe maandamano ya kumuunga mkono Rais ruksa??

Mbona wakitaka kuandamana wanaChadema wanapambana na kipigo cha mbwakoko cha Polisi??

Hivi hao Polisi wanajua kwamba wajibu wao ni kulinda maandamano yoyote ya wananchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi na wala siyo kuyazuia??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…