mojave
JF-Expert Member
- Apr 30, 2016
- 5,568
- 6,424
Nimeshangaa maamuzi aliyotoa ni kama wanajichanganya,
Kwani hao viongozi wa mifuko ya jamii si yupo nao kila saa na hata usikute wazo alilitoa yeye,
Sipingi ila ninavyoona serikali inafanya mambo kwa kukurupuka na kutokufikiria
Kwani hawakuona sheria hii ni mbovu na itaumiza watu wakati wakitaka kuipitisha?
Yani lililofanyika leo ni kama siasa
sio kama siasa, ni siasa na propaganda za kinafiki!
Kwa mujibu wa utaratibu wa Public Administration in Tanzania kitu mpaka kimepitishwa tayari kimeshajadiliwa na Baraza la mawaziri ambao Mwenyekiti ni Rais na pia kimejadiliwa na Inter Ministerial Technical Committee (IMTC) ambapo Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Sasa jiulize kama alikua hajui hili suala, ameona reaction ya umma imekua kubwa anajisafisha wakati ndio aliwatuma hao wakurugenzi wa hiyo mifuko kufanya huo ujinga.
Halafu kuna watu wanasifia eti Raisi wa wanyonge katusaidia wakati Rais huyo huyo ndo amekwapua nyongeza ya mishahara na kupanda kwa madaraja kwa watumishi( hashindwi kukwapua mafao).
kilichomtuma kukusanya kodi yote ikae mifukoni mwake na kufanya matumizi anavyotaka ndo kinachomdanganya na kupelekea kua na kibri cha kukopa pesa za wastaafu na kununua wabunge na chaguzi za kipuuzi na kujisifia kununua ndege na kutengeneza madaraja bila utaratibu( bunge) na kupigiwa makofi na wapuuzi wachache!