tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Ifahamike kwamba kada maarufu wa CCM, ambaye pia ni Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya, pamoja na kada mwenzake (Katibu mkuu wa TUCTA), Yahya Msigwa, walitetea sana kikotoo hiki na kusema kuwa wao ndio walipigana hadi kikawa 25%. Ushahidi huu unaashiria kuwa CCM walidhamiria kuwaumiza wastaafu kwa makusudi kwa kuwa wao ndio waliohusika kuifilisi mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kuchota zaidi ya Tsh trilion 8 kwa ajili ya kufanyia mambo yao ya kununua wapinzani.
Serikali yabanwa ilipe Sh8.4 tril mifuko ya hifadhi
Aidha, CCM kama chama wamechota Tsh 600,000,000,000 kutoka kwenye mifuko hiyo na kuiacha mifuko ikiwa hoi bin taabani. Kwa hiyo, CCM ndio waliohusika 101% kuleta kadhia hii.
Sasa inapotokea mtu ambaye ndiye anayesaini sheria hizi kandamizi akajitokeza hadharani kujifanya anawatetea wafanyakazi, sote tunapaswa kumshangaa sana. Na pia makada wa CCM (Nyamhokya na Msigwa) wapo kule TUCTA kwa ajili ya kukandamiza haki za wafanyakazi na kuitetea CCM kwa nguvu zao zote. Hebu msikie kada wa CCM (Nyamhokya) anavyotetea kikokotoo kipya cha 25% halafu leo hii anajifanya kuwa na uchungu na wafanyakazi:
Pensheni mpya yaibua gumzo