Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Ifahamike kwamba kada maarufu wa CCM, ambaye pia ni Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya, pamoja na kada mwenzake (Katibu mkuu wa TUCTA), Yahya Msigwa, walitetea sana kikotoo hiki na kusema kuwa wao ndio walipigana hadi kikawa 25%. Ushahidi huu unaashiria kuwa CCM walidhamiria kuwaumiza wastaafu kwa makusudi kwa kuwa wao ndio waliohusika kuifilisi mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kuchota zaidi ya Tsh trilion 8 kwa ajili ya kufanyia mambo yao ya kununua wapinzani.

Serikali yabanwa ilipe Sh8.4 tril mifuko ya hifadhi

Aidha, CCM kama chama wamechota Tsh 600,000,000,000 kutoka kwenye mifuko hiyo na kuiacha mifuko ikiwa hoi bin taabani. Kwa hiyo, CCM ndio waliohusika 101% kuleta kadhia hii.

Sasa inapotokea mtu ambaye ndiye anayesaini sheria hizi kandamizi akajitokeza hadharani kujifanya anawatetea wafanyakazi, sote tunapaswa kumshangaa sana. Na pia makada wa CCM (Nyamhokya na Msigwa) wapo kule TUCTA kwa ajili ya kukandamiza haki za wafanyakazi na kuitetea CCM kwa nguvu zao zote. Hebu msikie kada wa CCM (Nyamhokya) anavyotetea kikokotoo kipya cha 25% halafu leo hii anajifanya kuwa na uchungu na wafanyakazi:

Pensheni mpya yaibua gumzo
 
Hongera sana John Mnyika hoja zako makini wakati wa uzinduzi wa Barabara ya njia Sita hakika umemlazimu Rais Magufuli kuzifanyia kazi haraka.

Tunatarajia hata fidia za waliovunjiwa nyumba zitafanyiwa kazi muda utakaporuhusu.

Hakika John Mnyika ni Simba wa vita,ulitema madini ya ukweli na sasa inawalazimu waliotia pamba masikio kusikia vilio vya wanyonge.
 
Raisi ameahirisha tatizo, hajatatua tatizo!
Ametangaza kwamba uamuzi wake ni uamuzi wa kipindi cha mpito, akasema ameamua kikokotowo cha zamani kiendelee kutumika katika kipindi hiki cha mpito. Sasa hilo tatizo limekuwa solved kivipi?, Hapo alitakiwa atangaze mara moja kuirudisha sheria ya hifandhi za jamii bungeni ifanyiwe marekebisho kuingiza kikokotowo kilichofair siyo kuahirisha tatizo mpaka 2023. Sasa ikifika 2023 what next? hajasema chochote!. Wakati mwingine mkilambishwa pipi msiridhike kiurahisirahisi!
 
Yaani namsubiria kwa hamu kule twitter na yeye kama anajua tuna hamu naye kauchuna tu.
Ile ni saa mbovu.... basi tu haijafikishwa kwa fundi...... na baada ya ile ajali.... sijui....
 
umekaa kujiuliza kuwa kwanini John Mnyika alitoa hoja tano na ni tatu ndizo zilizojibiwa pale pale na mbili hazikujibiwa?

ni kwa sababu hizo mbili hazikujibiwa kwa sababu ndizo hoja za msingi na rais Magufuli hakuzijibu kwa sababu alikuwa bado anazishughulikia na leo hoja moja imepata ufumbuzi

usitegemee rais kuvunja sheria kwa kusema kwamba maamuzi ya mahakama ya kuwabomelea wale watu sio sahahi. sahau hicho kutokea
 
Mheshimiwa kaonyesha kwamba anaweza kufanya vizuri akikubali kushauriwa na kusikiliza watu.
Anaweza kuwa Rais bora endapo atajitahidi kuepuka matatizo mwanzoni badala ya kuyaacha, kuwa sehem ya tatizo kisha kuja kulaumu wengine kana kwamba hakujua na kuleta suluhu wakati madhara yameshatokea.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mjalie Rais wetu hekima na busara.
 
Naunga mkono hoja.
P
usihofu wewe na mwenzio mtoa mada mtapewa nafasi ya hawa waliyoshindwa kazi,kaeni mkao wa kula muda woowte kuanzia sasa
1546010253800.png

1546010310879.png
 
Mkuu Maharo, kiukweli wewe ni ma... kabisa kama jinalako lilivyo, hii kitu kilikuwa mubashara kabisa na rais kalizungumza vizuri sana na kulipangua, halafu wewe unauliza?.

Next time kama hujasikia mubashara, ingia kwenye thread ya kilichojiri, ndipo upandishe bandiko.
P.
Paschal , mi siyo maharo , Ni mahoro ..!!
 
Eti hongera Mnyika.
Hivi unafikiri hiyo kauli ya mnyika pekee ndio imemfanya Raisi afanye hivyo.
Yaani upinzani kama mko hivi basi msahau 2020. Tena huyo Mnyika harudi Bungeni.
Hongera sana John Mnyika hoja zako makini wakati wa uzinduzi wa Barabara ya njia Sita hakika umemlazimu Rais Magufuli kuzifanyia kazi haraka.

Tunatarajia hata fidia za waliovunjiwa nyumba zitafanyiwa kazi muda utakaporuhusu.

Hakika John Mnyika ni Simba wa vita,ulitema madini ya ukweli na sasa inawalazimu waliotia pamba masikio kusikia vilio vya wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana wakati naleta thread ya kuahirisha uchaguzi wa 2020, Kuna wanajukwaa walisema ni ndoto ya mchana. Kama ilikuwa ndoto, leo imeanza kutimia.

Nauona uchaguzi 2020 ukiahirishwa baada ya vifaa vya NEC kuchomwa moto na watu wasiojulikana - JamiiForums

Leo hii, kabla ya masaa 24 kuisha, mheshimiwa katangaza kufuta sheria ya kikokotoo kipya na kuendelea kutumika kikokotoo cha awali hadi 2023 ikiwa ni katika kipindi cha mpito.
— Kwanini 2023?
—Sheria hiyo alisaini nani?
—Raisi ana mamlaka ya kutengua sheria aliyosaini mwenyewe?

Bunge laukana Muswada wa Mafao wa 25% kwa 75%. Ladai waulizwe Serikali ndio walioleta kanuni - JamiiForums
Screenshot_20181228-104247.png


Tegemea pia kipindi cha mpito October 2020 hadi hapo 2023 wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika.

This is a strategic planning.
 
Back
Top Bottom