Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Magufuli leo July 19,2020 amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya July 17,2020 ambapo amemteua aliyekuwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Mwita kuwa RC Njombe, Mwita ameteuliwa badala ya Jumanne Fhika ambaye atabaki Ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.
 
Rais Magufuli amemteua mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe badala ya Dr Jumanne Fikha anayerudi ofisi ya Rais.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Ni jambo jema!
 
Rais anabadilika kama kinyonga.
 
Kabla ya juzi mkuu wa mkoa wa Njombe alikuwa Ole Sendeka, juzi akawa Jumanne Fikha, leo Mwita Rubya!

Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais, kwa sasa aachane na haya mambo ya kutumbua na kuteuateua, afanye mambo mengine. Hayana faida yoyote kwa sisi wananchi, tumeshayachoka.
 
Mkoa hauwezi kukaa bila kiongozi!
 
Daah huyu mzee nimesoma na mwanaye, mzee smart sana
 
Kumbe ofisi ya rais kuna wafanyakaz kibao
 
Aendelee tu mpaka aangukie kwa kigogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…