Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Mkoa hauwezi kukaa bila kiongozi!
Hivi mkuu wa mkoa akiumwa, akiwa likizo, akisafiri mbali, mkoa unaongozwa na nani?
Kwa muundo wa kiserikali, kila kitu kinaweza kuendelea hata kama mhusika rasmi akiwa hayupo. Hakuna haraka ya kihivyo sana.

Ilikuwa ni jambo rahisi tu, serikali kutoa mwongozo katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi nini kifanyike (mfano mtu akiamua kwenda kugombea, basi aliye nyuma yake anakaimu ofisi, then mengine yatafuata upepo ukipita).

Maana kwa hali ulivyo sasa Rais anahangaika kujaza nafasi zinazoachwa wazi haraka haraka mnoo bila weredi mpana, maana anaweza kuniteua kuchukua nafasi ya fulani ambaye amekwenda kugombea ubunge sehemu fulani kumbe mimi pia niko njiani keshokutwa kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CUF sehemu fulani.
 
Kabla ya juzi mkuu wa mkoa wa Njombe alikuwa Ole Sendeka, juzi akawa Jumanne Fikha, leo Mwita Rubya!

Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais, kwa sasa aachane na haya mambo ya kutumbua na kuteuateua, afanye mambo mengine. Hayana faida yoyote kwa sisi wananchi, tumeshayachoka.
Kwani ukiendelea na majukumu yako nA yeye akiendelea na majukumu yake kuna tatizo?
 
Namba 3 ndio jibu sahihi
Jumanne Fhika juzi tarehe 17/7 aliteuliwa na rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, leo tarehe 19/7 katenguliwa...

Nini sababu,
1. Amekataa?
2. Hafai?
3. Ukosefu wa umakini wakati wa kuteua? au,
4. Mteuzi kadanganywa.
 
Back
Top Bottom