Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Rais Magufuli leo July 19,2020 amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya July 17,2020 ambapo amemteua aliyekuwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Mwita kuwa RC Njombe, Mwita ameteuliwa badala ya Jumanne Fhika ambaye atabaki Ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.
View attachment 1510811
Haya mavyeo ya kupeana kwa jinsi mtu anavyoamka siku hiyo,yanalitia Taifa hasara,
Unamteua mtu leo,baada ya saa 48,unatengua,kama si kukurupuka ni nini?
 
Wale Wataalamu wa Nyota... hivi huu ndo Mwezi Mchanga, au ni Upepo wa Kusi?! Hoyaa Mshana Jr, hivi huku kwenye mambo ya Mwezi Mchanga huna utalaamu nako?!

Kule Uswahilini kwetu nasikia kuna kitu kinaitwa kipaipai! Nasikia watalaamu wa kipaipai huwa wanafunga kikaratasi kwenye mti!! Sasa ngoja pepo la kusi lianze kupeperusha kikaratasi huku na huko constantly!!!

Ndo hapo unakuta jamaa mmekaa mnapiga nae stori, mara anainuka huyoo, mbele kidogo mara anasimama na kurudi alikotoka kabla hajabadili tena njia kueelekea upande mwingine... ni mwendo wa kufuata mwelekeo wa kikaratasi hadi Kusi lipite!!

Halafu hata sijui nilitaka kusema nini hasa hapo... cjui na mimi ndo Pepo la Kusi lenyewe!!!

Ila tuache masihara... Watanzania tuweke siasa pembeni tukisake hicho kikaratasi kwa udi na uvumba kabla hamjasikia Bashite kateuliwa kuwa RPC Kanda Maalumu ya Kinondoni!!
HAAAAHAAAAAHAAAA NIMECHEKA KAMA KIBOSILE WAKATI HATA CHAPA JAILII MFUKONI.😀😀😀😀😀😀📻
 
Really now!?... Hii ni Sawa na kusema wabunge wa CCM wamejazana kwenye kamati za kudumu za Bunge bila kutilia maanani wao ndio wengi Bungeni...FYI kanda Ile INA 1/3 ya population ya nchi hii. Na demokrasia mara nyingi unasema wengi wape.
Pia wamesoma sana . mfano mzuri saivi mkurya akaachana na ng'ombe amejizatiti katika kusomesha na biashara. Zamani ile kanda waliyosoma kwanza wakurya Ilikuwa ni cows in blood really in blood. Kuua kisa kuiba cows ni easy task at him.
Sasaivi kuna bilionea amepata Hela kama 6+ bilioni Machimbo ya buhemba. Baada ya laizer akapatikana huyu.
 
Huyo aliyekuwa ameteuliwa ikiwa alikuwa amechinja hadi ng'ombe ya kufurahia uteuzi vipi atalipwa hiyo hasara!!
 
Tumechoka na hizi post za uteuzi,

Mtaani kwako au kijijini kwenu hakuna mambo ya muhimu yanayoizunguka jamii yako ukatupostia?
 
Rais Magufuli amemteua mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe badala ya Dr Jumanne Fikha anayerudi ofisi ya Rais.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Ndio maana wanakimbilia ubunge, imagine Fikha alikua anajiandaa ukuu wa Mkoa mara karudi kuwa desk officer
 
Back
Top Bottom