Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Jumanne Fhika juzi tarehe 17/7 aliteuliwa na rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, leo tarehe 19/7 katenguliwa...

Nini sababu,
1. Amekataa?
2. Hafai?
3. Ukosefu wa umakini wakati wa kuteua? au,
4. Mteuzi kadanganywa.

Kuna mmoja aliteuliwa kwenye post kubwa sana tu, na akajua baada ya kupigiwa simu na mdogo wake kupewa hongera, akabaki anashangaa, hakuna consultation wala nini. Ndio awamu ya 5 hiyo
 
Rais John Magufuli amefanya mabadiliko katika uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambapo leo Julai 19, 2020 amemteua Mhandisi Marwa Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe kuchukua nafasi ya Jumanne Fhika aliyeteuliwa Julai 17 kushika wadhifa huo.

Fhika atabaki Ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.

Azam TV

Kwa mliosoma Political Science na Public Administration hiki Kitendo ni cha Kawaida na tukipongeze au labda kuna tatizo mahala na linatia shaka?
 
Wakati wa Kikwete kuna mkuu wa Wilaya aliteuliwa kuwa DC Wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga lakini kabla ya kuapishwa uteuzi wake ulifutwa
 
Pia Kuna mkurugenzi (DED- kasuru) awamu ya kwanza (2016 )ya uteuzi wa magufuri Hadi aliapishwa kabla hata hajaripoti kasuru/ ama siku kwanza kazini akatenguliwa.
 
Kabla ya juzi mkuu wa mkoa wa Njombe alikuwa Ole Sendeka, juzi akawa Jumanne Fikha, leo Mwita Rubya!

Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais, kwa sasa aachane na haya mambo ya kutumbua na kuteuateua, afanye mambo mengine. Hayana faida yoyote kwa sisi wananchi, tumeshayachoka.
Kwa hiyo nafasi ikiwa vacant afanyeje!? Aiache hivyohivyo!? Asiteue!??
 
Back
Top Bottom