Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Kuanzia Dream liner, Bombadia, mpaka zile VX na Helicopter anazotumia Magufuli zimetengenezwa na mabeberu na zikisumbia tu ni mabeberu hao hao wanaitwa kuzirekebisha. Sijui ni kwanini Magufuli hazilitii mashaka na badala yake anapotosha watanzania kuhusu Barakoa na Chanjo?

Farao ana matatizo makubwa kichwani.

Hizi siasa za kina Magufuli na wenzake zinafikirisha sana...

Unajua unapokuwa na hoja kama hii, yakupasa;

1. Kama unasimamia Sayansi, basi, uwe na very strong scientific proof itakayosaidia kujenga hoja ya kukataa scientific products za wengine bila kuleta chenga chenga na mauza mauza ya kisiasa...

2. Kama mtu anasimamia IMANI, vivyo hivyo ni lazima uwe na maandiko yanayo prove kwamba, that's a satanic plan to destroy and kill Africans and especially Tanzanians...

But very unfortunately, hakuna maelezo yoyote ya maana yanayotolewa na Magufuli na serikali yake yanayoweza kumshawishi kila mtanzania ingalau kwa uwingi wao wakaelewa...

Kinachofanyika ni poliwanavyoelekezwa na e manoeuvres ya serikali kujijitetea kila uchao kiasi cha kufikia mahali sasa imeanza kujichanganya yenyewe na kuleta big confuse miongoni mwa wananchi kiasi cha kushindwa kuelewa wafuate lipi na waacha lipi....!


Mara anawaambia wananchi wachukue hatua zote za kujikinga kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya...

Mara paaa anatazama mbele yake anawaona masister wa Kikatoliki wamevaa barakoa, anawasimanga na kuwaeleza kuwa mtakufa, barakoa hizo zina sumu...

Haa haa haaa. Magufuli bwana, ni shida kweli....
 
Umeulizwa swali badala ya kujibu unamwambia Kiranga amtafute Mzee Butiku amuulize?
Inaelekea hiyo story yako ni fiction.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
Ametaka ushahidi. Ushahidi utolewa kwa namna tofauti. Si lazima uwe ushahidi ulo andikwa. Au Atafute magazeti ya wakati huo. Mzalendo, Mfanyakazi na Gazetu la uhuru, ilikuwa mwaka 1984. Usirukie mambo usiyo yajua.
 
Hapa nilipo leo limepita tangazo korona imerudi.. korona imerudi wananchi mchukue tahadhari.. kila nyumba au duka lazima iwe na ndoo ya maji, marufuku mikusanyiko.. ukikiuka unakamatwa na mgambo. Naomba nisitaje eneo hilo ili kulinda ajira/vyeo vya hawa werevu
Wako sawa kabisa, kuanzia kesho matamko yanaanza upya
 
Kwa yeyote ambaye anataka kuelewa vizuri aende kusoma 𝗦𝘂𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝗣𝗶𝗹𝗶, 𝗜𝗯𝗮𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝟯𝟳(𝟮) ya 𝗝𝗠𝗧. Japokuwa hili HALIWEZI tekelezwa kutokana na MFUMO wa Utawala, bado ni muhimu kwa Kila mmoja wetu kupitia Sheria ili kuzijua HAKI zake.
 
Wakuu,

Nimemsikiliza Rais Magufuli akiwa anaongea leo kanisani. Nimeshtuka, Rais anaongea kama layman kabisa. Hii ni hatari kwa Usalama wa Taifa kwa mtu ambaye amepewa dhamana ya juu kabisa hapa nchini.

Rais ni Comforter-in-Chief hivyo kama mfariji mkuu wa Taifa ana mamlaka makubwa aliyobebeshwa na hili inaelekea Magufuli analisahau sana. Huwezi toka huko na kuanza kuwambia watanzania eti “Kufa tutakufa tu”.

Rais ni kama BABA katika familia, na kwa Taifa yeye anasimama kama kichwa cha familia. Huwezi kuwa baba bora ukawa unatishia watu wako (wanao, mkeo, ndugu n.k). Kama baba, unaweza kulaumiwa, unaweza kuliliwa, unaweza kupongezwa, unaweza kuumizwa na hatutarajii kuwa utaitangazia familia kuwa wakome kufanya hivyo! Utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yako.

Rais ni KIUNGO katika Taifa. Unapotokea mgawanyiko, ana wajibu wa kuhakikisha watanzania wanakuwa wamoja. Hili limekuwa likionekana kuwa tofauti kwa Rais wetu huyu.

Rais anapotoa kauli, ni kauli ya Taifa si yake. Mambo mengi anayoongea Magufuli watanzania walio wengi (wanaojielewa) watakubaliana nami kuwa si yale ambayo kimataifa tungependa kiongozi wetu ayaongee kwa niaba yetu!

Msikilize:



Sasa:

1) Magufuli leo kaongea UONGO mwingi kuhusu barakoa. Alichokiongea ni matusi kwa serikali yake mwenyewe!

- Kama barakoa zilizoingizwa nchini zina virusi au hazifai; kwanini watendaji wake wameziacha ziingizwe sokoni? Anataka kutuambia kuwa TBS na TFDA hawajui kazi yao? Kwanini watendaji wakuu wa taasisi hizi bado wapo kazini?

- Tukubali kuwa tumeingiziwa barakoa zenye kuwa na virusi ambazo zitawaua watanzania: Kwanini Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, IGP na CDF bado wapo kazini? Taifa letu manake usalama wake upo hatarini. Kwa mantiki hiyo, maduka ya madawa yavamiwe mara moja na barakoa zote ziondolewe sokoni

2) Magufuli amekuwa Rais wa kwanza mimi kumuona akiwa anahubiri katika Ibada za Kanisa Katoliki. Huu ni utaratibu wa kawaida kwa wakatoliki? Halafu anawachamba viongozi wa kanisa kwa kuhimiza waumini kujilinda?

3) Rais ametangaza dawa kadhaa kama Bupiji, COVIDOL etc, anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Sayansi nyingine haifanyi kazi tena? Kuwa watanzania wasiziamini dawa nyingine zinazotolewa hospitali tena? Haya matangazo ya dawa za asili imekuwaje hadi wasaidizi wake wamwacha hadi ataje baadhi ya dawa moja kwa moja (kwa kutaja baadhi tu)? Ana maslahi nazo? Nasikia mtu aliwahi kuwa RC wa Dar ana mkono kwenye pharmacy chain flani, na kuna tetesi kuwa yupo kwa niaba ya ‘mzee’; hii haoni inazidi kujenga hisia zisizo sahihi?

Nitarejea


Amesema Siku ina masaa 48 kwahiyo wanaovaa barakoa wanaweza kubadili barakoa 12?
 
Hivi mnataka Magufuli aweke nchi rehani apate hela ya kuwafungia awalishe? Aya Corona ipo and so what, mbona hao mnaotaka watusaidie kuhusu hii Corona ndo wanakufa kuliko sisi? Acheni usenge fanyeni kazi tukuze uchumi tutakao kufa tufe watakao ishi watanufaika na tukichowaandalia.
 
Mzee anasema

Siku ina Masaa 48, Barako inabadilishwa kila baada ya Masaa 4, hivyo kwa Siku tunahitaji Barakoa 12.

Najiuliza
#1. Siku gani ina Masaa 48????

#2. Je Barakoa zinavaliwa wakati wa kulala?????????????
 
By all account mzee yupo Sahihi sana Acha tu azidi kuiweka Corona kando haina maana Kuwa Publicized mana ina impact mbaya sana watu wakisema wajifungue tu kubali tu nature ina take place wacha iwe survive of the fittest tutakao Kwenda wacha twende ili wengi wabaki salama
 
Nimeshangaa, he admitted hadi ndugu zake wamepigwa, watendaji wake wa karibu wamepigwa. Halafu yeye kama Rais anapokiri haya anataka tuchukulie “POA” tu?
Kwani nani hajapigwa?. Rais wa Amerika (Trump) alipigwa, Waziri mkuu wa Uingereza alitandikwa na kadhalika. Ni vita ya kibiolojia. Wa Uchina wamekazana kutaka kumpiga, wakashindwa. Wa Urusi wakashindwa.
 
We jamaa nimekupenda bure. Nilichojifunza kwa watanzania ni uhuru mwingi wa kupitiliza afu kila mtu anadhani yeye anajua kuliko wengine.mhe.rais ni kiongozi wetu na amesema wazi kwamba yeye anataarifa nyingi kuliko sisi wote.anavyombo vingi vya kumpa taarifa ata kutoka kwenye mataifa mengine. Wewe ni nani mpaka unamdaharau mhe rais .

Lakin pia nimepitia michango ya watu humu kuna mtu anasema ata bila aibu eti malikia wa Uingereza na marais wengine wamechanjwa hiyo chanjo ya pfizer na nyinginezo wakati taarifa zilionesha kwamba hao watu hawakuchanjwa walifanya udanganyifu wa kukusanya vyombo vya habari na kujifanya wanachanjwa wakati sindano zikioneshwa kwa siri kwamba zimefungwa kwenye ncha.

Lakini pia hizi chanjo zinamadhara kwa watu weusi wa marekani japo hawasemi wanaficha.kunawatu wamechanjwa a wamekufa.south africa wamekataa chanjo kwasababu wanasayansi wamevundua kwamba sio effective kwa kirusi kipya kilichoundergo mutation,mara kimeshakuwa covid 21 watanzania wanajifanya wao ni wanasayansi kuliko mhe rais ambaye walau ana phd ya sayansi.

Pia chanjo hizo za europe zimetengenezwa kwa genetic engenering madhara yake yanakuwa kwenye gene maana yake watu wasipokuwa makin waafrica wa miaka ijayo hawatakuwa waafrica wa leo. Madhara ya genetics ni ya vizazi na vizazi watu hawaweze kuelewa ilo.

China na urus wametengenez chanjo ila wakubwa wa dunia wako wanapigana vikumbo kutoidhinisha izo chanjo na wanataka ziundergo review process wakati zao hizo hazijapitia hizo process.Mkila mkashiba mnaanza madharau.

WATANZANIA WENZANGU tujitafakari wakati wa kutoa maoni.

Mataga bwana! 😂😂😂
 
Nimeshtuka, Rais anaongea kama layman kabisa. Hii ni hatari kwa Usalama wa Taifa kwa mtu ambaye amepewa dhamana ya juu

Rais ni Comforter-in-Chief hivyo kama mfariji mkuu wa Taifa ana mamlaka makubwa aliyobebesgwa . ....,,,,Huwezi toka huko na kuanza kuwambia watanzania eti “Kufa tutakufa tu”.
asipowa comfort inakuaje hatari kwa usalama wa salama, watalipua mabomu ???
 
Back
Top Bottom