Labda sasa Kariakoo ndani ya jiji jipya itakuwa kama Dubai biashara masaa 24 , mwanga wa kutosha usiku wote lazima biashara zilizokufa Kariakoo ambazo wafanyabiashara kutoka Zimbabwe, Congo, Malawi , Zambia , Comoro n.k warudi na wasiwaze kwenda China wala Dubai kufuata mzigo.
Na machinga wote watasombwa kubwagwa Kinondoni, Ubungo, Temeke na Kigamboni.
Jiji la Dar es Salaam "mpya" litaambaa na barabara ya Nyerere kuchukua ukanda wa Tazara Stesheni DSM, viwanda vote Ukanda wa "Pugu Road " hadi Airport ya Uwanja wa Kimataifa wa JNIA. Jiji hili jipya litaamba Kurasini mivinjeni mpaka bandari zote kavu na bandari yenyewe. Maeneo ya Mjini Kati Posta, Gerezani, Mnazi Mmoja , Upanga, Magomeni hadi Ukanda wa Morogoro road Ubungo Maji mpaka Stendi Mpya Mbezi Louis.
Bila kusahau maeneo ya Oysterbay , Masaki hadi Mawasiliano 2000 stendi yatakuwa ndani ya Jiji jipya la Dar es Salaam lenye miundo-mbinu ya flyover, madaraja , BRT mwendokasi, superfast internet, bila uchafu wa meza za wamachinga, bidhaa kupangwa barabarani sehemu za wenda-kwa-miguu.
Hii itasaidia Jiji jipya la Dar es Salaam kukusanya kodi kwa kusaidiana na TRA kwa ufanisi huku miundo-mbinu ikibaki wazi na safi kwa wenye shughuli zenye TIN Number TRA na Dar es Salaam jiji jipya kuwa ULAYA ndani ya Africa.
Hawa wamachinga "wametuchelewesha" sana Dar es Salaam yenye miundombinu na magorofa makubwa kuchangia kodi, kwani biashara zimekufa na wameharibu muonekano wa jiji kisa wamechangia Tshs. 20,000 kitambulusho cha mfanyabiashara mdogo wakati wanaharibu mazingira ya biashara kubwa, biashara za kimataifa na hata watu wanakimbiza ofisi zao toka mjini kati kuzipeleka maeneo ya Victoria, Makumbusho ili kuondokana na hawa "wakuja" machinga wasioelewa maana ya jiji.
Watendaji nao wa serikali madiwani, mameya, waDC , Mkuu wa Mkoa bila kusahau viongozi wa CCM ngazi zote Dar es Salaam nao wamekuwa waoga na kukosa ubunifu kulifanya jiji kuwa Dubai au Singapore ya Afrika huku serikali imewekeza matrilioni ya fedha kuinua hadhi ya mji wa Dar es Salaam uwe wa kisasa kufuatana na uwekezaji mkubwa wa Maendeleo ya Vitu uliowekwa jijini Dsm.