Tupo wote.. ukipata maelezo mazuri naomba unitag Mkuu.
Naomba nikueleweshe ili na wengine waelewe..ila maelezo yangu ni kutokana na jinsi nilivyoelewa...kama kuna ambae hajaelewa naamini hapa atanielewa...ila ikiwa nimetoa maelezo yasiyo sahihi, mwenye uelewa zaidi atafafanua ila mpaka hapa naamini nimeelewa na niko sahihi kwa asilimia 100%...Naomba usome kwa makini...
Iko hivi...zamani (kuanzia jana) jiji la Dar lilikuwa linaundwa na halmashauri/kulikuwa na mayors 6 (Temeke, Kinondoni, Ilala, Ubungo, Kigamboni walikuwa na mayors wao then DSM as a whole nayo ilikuwa na Mayor wake ambae ni mayor wa jiji zima..so jumla kulikuwa na mayors 6 ndani ya mkoa mmoja)...Kwahiyo, bajeti ya Mayor wa Halmashauri ya jiji la DSM ilikuwa inachangwa na zile halmashauri zingine 5..kiufupi zile halmashauri 5 zilikuwa na kazi ya kuchangia bajeti zao halafu tena zitoe kiasi kidogo ili kuchangia bajeti ya Halmashauri ya jiji zima..Hapo ilikuwa ni gharama mara mbili...
sasa, ili kupunguza gharama Rais ameamua kuiua halmashauri ya Jiji la dsm na badala yake halmashauri ya Ilala ndo itaplay role kama halmashauri ya Jiji...Maana yake, sasa zitabaki halmashauri 5 tofauti na 6 za mwanzo...Halmashauri za sasa zitakuwa ni TMK, KINONDONI, KIGAMBONI, UBUNGO na ILALA ambayo sasa itasimama kama halmashauri ya jiji zima...Maana yake hakutakuwa na ile hali ya mapato ya halmashauri moja kuchangia bajeti ya jiji...pesa inayokusanywa tmk itatumika tmk, the same as kino, ubungo na kigamboni halafu pesa au mapato yatakayokusanywa Ilala yatatumika kwa jiji zima maana Ilala sasa ndio halmashauri ya jiji...Hapo gharama mara mbili zitakuwa hazipo kama mwanzo.
KIUFUPI..mkoa wa DSM utabaki kuwepo na JIJI LA DSM litaendelea kuwepo ila tu kiutendaji, Ilala itakuwa inafanya majukumu ya mkoa mzima ndio maana imepandishwa hadhi kuwa Halmashauri ya Jiji...BINAFSI NIMEMUELEWA RAIS.
Ngoja nikupe mfano mwingine....
Assume, shule uliyosoma ilikuwa na form 1 hadi 4...sasa kila darasa lilikuwa linatoa kiongozi wake ambapo jumla viongozi watakuwa 4 (mmoja kila darasa) halafu pia anakuwepo na kiongozi wa shule nzima (huyu anachaguliwa mmojawapo miongoni mwa hao viongozi wa madarasa)..Jumla tunapata viongozi 5....sasa, ili kuiendesha shule mapato ya form one yalikuwa yanatumika kumlipa kiongozi wa form 1 na kiasi kingine kuchangia kumlipa kiongozi wa shule nzima maana kila darasa lazima lichangie kumlipa yule kiongozi...Matokeo yake sasa, kila darasa lilikuwa linaingia cost mara mbili...moja gharama za kumlipa kiongozi wake wa darasa na pili kuchangia gharama za kumlipa kiongozi wa shule na wakati huo huo, kiongozi wa shule anapatikana kwa kuchaguliwa mmojawapo kutoka kwa wale viongozi wa madarasa...Kikawaida huu ni mzigo mkubwa wa uendeshaji..
sasa ili kupunguza gharama, shule inaamua kuwa viongozi wa form 1, 2 na 3 watasimamia madarasa yao halafu kiongozi wa form 4 ndo anapewa hadhi ya kuwa kiongozi wa shule nzima..kwahiyo mapato ya form 4 yatatumika kuendeshea shule nzima (Hakuna tena michango kutoka madarasa mengine) halafu mapato ya yale madarasa mengine yatatumika kwenye madarasa yao tu..Hakuna kuchangia tena kwenda kwa uongozi wa shule nzima....Ila bado shule itaendelea kuitwa jina lile lile..Hadhi mpya ya Form 4 haina effect kwenye jina wala hadhi ya mkoa kwa ujumla..
Maana yake...JIJI LA DSM litaendelea kuwa hivyo..MKOA wa Dsm utaendelea kuwepo..Wilaya za Ilala, tmk,kino, ubungo na kigamboni zitaendelea kuwepo....ila katika utendaji na usimamizi wa bajeti na miradi ya mkoa mzima...Ilala au maamuzi ya Ilala ndio yatasimamia jiji zima...So, ilala ni monitor wa Jiji (dsm) ila bado jiji litajulikana kuwa JIJI LA DSM...
Mpaka hapa naamini walau utakuwa umeelewa japo kwa kiasi kidogo...!