MAONI YA WATU KADHAA HUKO NJE JUU YA MKUTANO WA MH RAIS JPM NA WAPINZANI IKULU YA MAGOGONI JANA 03/03/2020 NA HASA MKUTANO WAKE NA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD
Ni ishara nzuri kwa utengamano na ustawi wa siasa za Tanzania na kanda nzima ya Maziwa makuu ( Marry Marle ,wa sudani Kusini)
Kwa hapa nyumbani Ghana hilo lililotokea Ikulu ya Tanzania haliwezekani maana upinzani na serikali ni Paka na Panya .(Nana Brentor : Wa Ghana)
Huo ndio uzuri wa kuwa na serikali inayotokana na watu, Nadhani watanzania wataendelea kumkumbuka Nyerere Kwa miaka mingi. (Dotista Do: Wa Ivory coast)
Kwa kweli inapendeza sana kuona wapinzani wanakaa meza moja na Rais wa Nchi ,kilichonifurahisha zaidi ni mamlaka za Tanzania kuchukua Tahadhari ya Virusi mapema picha ya ukweli kuwa hakuna kisa chochote cha maambukizi nchini humo. (Theophilus: Wa Guinea)
Hilo haliwezi kutokea hapa Liberia ambako wapinzani wanamuita Rais George Weah Shetani wa pangoni. ( Ebenezer Gatel : Liberia)
Umefika wakati vijana wanaochipukia kwenye siasa waige mifano hii na wajiepushe na Siasa za matusi,Ujambazi na Mapanga . ( Nyungwe : Wa Nigeria)
Hii inatuma ujumbe kwa Kizazi Kipya ambao wanaamini Kwenye Mabavu na Vurumai kama mtaji wa Ustawi kisiasa. ( Idrisa Ezra : Algeria)
Ni hatua nzuri ikiwa itaambatana na Matendo . ( Faiza Nasri : Wa Misri)
Wakati nchi zilizoendelea wanajiandaa kwa vifaa na kutenga bajeti kukabiliana na Virusi vya Corona kwa Vitendo wenzetu Afrika wanajiandaa kwa Picha na propaganda Mitandaoni ( Smith ASJr : Beberu kutoka Uingereza
Nampenda sana Rais Magufuli natamani aje atuongoze hapa Zambia . ( Erikrius Rula : Wa Zambia)
Hayo ni baadhi ya Yale yasemwayo huko Duniani juu ya umahiri wa JPM na umoja wa Taifa letu
C&P
Sent using
Jamii Forums mobile app