Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

Kambi rasmi ya upinzani hatujaiona...
Kilichotokea ni kukutana na CCM B na CCM C....

Alisema kamanda fulani..
Kama a=b, b=c, kwa hiyo a=c...r we together??

Everyday is Saturday..............😎
 
Aliokutana nao sio Wapinzani amekutana na viongozi wa Vyama Tanzu na CCM,uliona wapi Mwenyekiti wa Upinzani akapokelewa na Mkuu wa Mkoa Kada wa CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mkiitangazia dunia kukosekana demokrasia, kuuawa, kuteswa hawacwapinzani wenzenu wanaenda Ikulu ku chati na kufanya mzaha na mnayedai ni dikteta!

Seif ni kiongozi katika chama chako Zitto unayedai nchi inaendeshwa kibabe! Raisi anakutana na aliye chini yako anakuacha wewe kiongozi wake! Hupati ujumbe? Unanuka!

Hao mnaowapa porojo si wanawadharau wakiona hivi? Mlango uko wazi ila mnashindwa kuingia kwa kuwa mu wachafu mno!

Mbowe unadai umemwandikia Raisi barua kutaka mkutane na unadai pawe na maridhiano unajisikiaje ukiona ambao hawajaandika barua ndio wanaenda Ikulu? Wewe umebaki na libarua lako!
Huoni kuna kitu hujapatia?

Iweje raisi akupuuze wewe lakini asiwapuuze kina Mbatia? Hivi kwa unavyomdhihaki majukwaani kutwa kucha unategemea akuite Ikulu?

Kwanini wewe, Zitto na Lissu mnakosa staha? Au mnadhani kina Mbatia ni wajinga? Mbona hatuwasikii wakimtukana mkuu wa nchi kama ninyi?

Hakika raisi anapaswa kuwapuuuza! Hata barua yako asiijibu! Mmekosa weledi katika siasa.
 
Kila mpinzani ana chama na sera zake msitake kuwapangia watu wafuate sera na misimamo ya CHADEMA.

Mbowe alipoenda Mwanza sherehe za Uhuru Zitto aliponda mkamkashifu ingelikuwa yeye ndiye kaenda mngemponda pia.

Kila mmoja apambanae na hali yake maana wanasiasa wote wachumia tumbo tu
 
atuwezi kusema kuna mtu kapatia sana au kakosea sana mwisho wa siku mwamuzi wa haya yote ni akili za utambuzi za wapiga kura.

Upande wapili mizaha hii inafanywa ili kuwa vunja mioyo walio kwenye njia sahihi. Cha muhimu zidisheni mapambano zaidi yenye kuleta fikra huru zaid nje na kwa wananchi mizaha yao itayeyuka.

Wananchi tulio wengi leo hatuangalii mizaha tunaangalia maisha yetu ya kila siku na ni nani anayetuchorea ramani nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya Mabeberu inaanza kuonekana. Ndio maana walikuwa hawana namna lazima wamfukuze Membe maana wanaona kabisa jicho la mabeberu lipo wazi muda wote.

THE ZITTO EFFECT: Kwa ufahamu wangu Magufuli asngekutana na wapinzani kama Zitto asingeenda kwa MABEBERU aka WAHISANI (kama upendavyo).

Akili nyingi ilibidi itumike kwa Magu kati ya kumuweka ndani Zitto au kuanzisha mazungumzo naye. Sijui kama ni mawazo yake Rais au ni ushauri nasaha alioupata toka kwa wazee juu ya kukutana na wapinzani sina hakika lipi ni sahihi.

Kama alishauriwa kufanya hivyo, bado tatizo halijatatuliwa, lakini kama wazo hilo limetoka kwake yeye mwenyewe ni ushindi mkubwa sana kwa WATANZANIA/wananchi wote. Ikiwa siasa za kibabe za kuwasweka ndani wapinzani zitajitokeza, itakuwa wazi kuwa wazo hilo kashauriwa tu na wala halitoki moyoni mwake - Hii itakuwa hatari kwa TZ. Zingatia huu ni mwaka wa uchaguzi.

Tusubiri, muda ndio msema kweli.
 
Hivi ninyi wapi-mzani nani aliwadanganyeni kuwa tume huru itapatikana bila kuwa na mabadiliko ya katiba? Tume iliyopo inatambuliwa na katiba na tumekuwa nayo for about 60 years,I don't catch you well

Sent using Jamii Forums mobile app

Si katiba wala tume huru ni jibu kwa wakati wa sasa.

Kwani hata hiyo katiba iliyopo haifuati, unatarajia ukipata nyingine ndio itafuatwa? Hii iliyopo ingefuatwa, ingekuwa na matokeo chanya makubwa tu.

Kwa ushauri wangu: la kwanza ni kutafuta mbinu itayowafanya viongozi kuheshimu katiba, tukianza na hii iliopo.
 
Zitto karibu huku ushuhudie wanasiasa nguli wanaojua siasa. Wenzako matatizo ya nchi wanakaa chini na kuzungumza, wewe unaenda ugenini kuzungumza halafu unajiona mwamba wa siasa. Rudi darasani ukajifunze uzalendo.
Fungua macho uone
 
Chadema walienda sana ikulu kipindi cha JK ila haikuwa shida.
 
Walipaswa kusema baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…