Rais Magufuli alifanya mambo yasiyofaa na Rais Samia anarekebisha mabaya yaliyofanywa

Rais Magufuli alifanya mambo yasiyofaa na Rais Samia anarekebisha mabaya yaliyofanywa

Bila kuficha wala kuogopa, kwamba Rais Magufuli alifanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na uongozi bora na alikuwa akitupeleka kwenye hali mbaya sana kama taifa la Tanzania. Alikuwa na kauli za kinafiki na hata kuamuru taasisi za serikali kubambikia watu kesi. Kuna mengi sana ambayo yote yakiwekwa wazi hakuna atakaetaka jina la Magufuli lionekane popote nchini, labda hayo mengine tuyaache kwa sasa.

Lakini sasa kazi kubwa anayofanya Rais Samia ni kuturudisha kwenye mstari sahihi wa uongozi kwa maslahi ya Watanzania wote. Rais Samia anastahili pongezi toka kwa kila Mtanzania mwenye akili timamu, sio lawama na shutuma. Wito wangu kwa Raisi Samia ni kuwaondoa au angalau kuwabadilisha kazi viongozi wa taasisi wote waliomtumikia Magufuli katika kutekeleza mambo maovu dhidi ya serikali na wananchi - iwe kwa kuwadhuru watu au kuhujumu mali na fedha za taifa. Nenda mbali zaidi ya Takukuru - angalia pia katika taasisi zote za serikali, za kijeshi na kiraia kutia ndani wakuu wa mikoa na wilaya. Watu hawa wamekosa imani toka kwa wananchi na hawafai tena katika nafasi zao, hawana legitimacy ya kuendelea kushika nafasi walizotumiwa vibaya. Wanaweza kuwa walitumika na si kosa lao la moja kwa moja, lakini kanuni za uongozi zinalazimu waondoke au waondolewe.

Ni vizuri watu wakaelewa haya ili kumwelewa Rais Samia. Haisaidii lolote kuficha ficha mambo. Tuko pamoja nawe Rais Samia, kwa maslahi ya Watanzania na Afrika kwa ujumla. Hongera sana mama, ziba masikio usisikie kelele za vyura wanaodhani watamzuia ng'ombe kunywa maji wakizidisha kelele.


View attachment 2196325
Hv hamnaga mambo mengine ya kufanya ama mnalipwa!!!?
ukilala ukiamka Magufuli!!??
kwendeni zenu bana tumewachoka
 
Hv hamnaga mambo mengine ya kufanya ama mnalipwa!!!?
ukilala ukiamka Magufuli!!??
kwendeni zenu bana tumewachoka
Na kwa nini na wewe ukilala ukiamka unatafuta watu wamesema nini kibaya juu ya JPM? Ulikuwa mchepuko wake? Kwenda zako tumekuchoka!
 
Magufuli alikuwa laghai, mbaguzi, kiburi, alikuwa sadist
Sema Tanzania ina wapumbavu wengi wanamuona shujaa
 
Hivi najiuliza mbona watu wanatumia nguvu kubwa sana kumsema JPM kuliko kujenga nchi. Au ndio njia ya kututoa kwenye focus
 
Jengeni nchi acheni ujinga Tunahitaji mfumuko wa bei ushuke, ufisadi ukome. sio story za mtu aliekufa hapa
 
Naona unaelewa sana mtu anaemiminiwa anakuwaje kutokana na personal experience yako. Sasa sio mimi. Uko wewe na wenzio kama wewe.
Shika ukuta tu blaza huna namna kila siku mauufuli mauufuli mata.........yenu kumbaf
 
Mbona nguvu nyingi sana inatumika ili kujitangaza? Mazuri huwa wanakuja tu si lazima kumsema marehemu ambaye hawezi kujitetea, acha kupambana na marehemu!
 
Hivi najiuliza mbona watu wanatumia nguvu kubwa sana kumsema JPM kuliko kujenga nchi. Au ndio njia ya kututoa kwenye focus
Yaani badala ya kufanya mazuri tuyaone wanazurula tu wapewe ajira huko huko
 
Mie nafanya kazi nje ya nchi. Kwa hiyo uko wrong on all counts
Kwaakili mbovu kama hizo za kulialia pasipo naushahidi wowote sijui unafanya kazi nje ya nchi gani,labda upo ziwa nyasa upande wa malawi unavua dagaa.
 
Kwaakili mbovu kama hizo za kulialia pasipo naushahidi wowote sijui unafanya kazi nje ya nchi gani,labda upo ziwa nyasa upande wa malawi unavua dagaa.
Tatizo lako ni nini hasa, thread hii inatokana na video clip iliyowekwa, ambayo serikali ya sasa ndio inakupa uozo uliofanywa na Magufuli ambao imebidi iurekebishe. Sasa wewe unanishambulia mimi kwa kisa gani hasa maruhuni mkubwa wewe!
 
Binafsi siwezi kumpenda muuaji asilani hata afanye mazuri mengi kiasi gani. Hitler aliinua sana uchumi wa Germany, na bila WWII hakuna nchi duniani ingeikaribia Germany kwa uchumi imara. Na hata Hitler aliwapenda watu wake na kuanzisha gari ya VW kwa ajili ya kila Mjerumani, lakini ni watu punguani tu ambao wanampenda Hitler
Hakuna utawala usioua mwangosi alikufa nani alikuwa mtawala, rais wa madaktari aling'olewa kucha na meno nani alikuwa mtawala hata leo watu wanakufa na wataendelea kufa,hayo matusi mnayo mtukana magu Kama mwajiri wenu ni watawala hata Mimi hata Mimi natakiwa kufa.
 
Kuna kiongozi mmoja wa Magufuli kwenye kipindi cha kampeni za ule uchaguzi/uchafuzi aliwahi kusema kwamba hata msipochagua ccm ila itashinda tu. Kiongozi wake sijui tumfanyaje?
 
Kuna wakati kunakuwa na tofauti. Kumbuka CCM ni chama ambacho ndani yao wanafiki huenda ni 3% ambao ni viongozi. The rest ni wanachama watu wa kawaida tu kama mimi na wewe. Wakati wa JPM, yeye ndio alikuwa CCM, na the rest makanyaboya tu yakiogopa hata kumjibu au kutoa pendekezo
Pamoja na kwamba ameshaondoka duniani amewaachia wafuasi wale kindakindaki kazi ngumu ya kutetea jina lake na yote aliyoyafanya kwa ajili ya Tanzania.

Ni kazi ngumu na wanaifanya kwa upendo wa hali ya juu, wanapambana na walio hai wenzao, ni vita ya maneno zaidi ingawa mara moja moja inaweza ikaenda mbali na kuleta mitafaruku.
 
Hakuna utawala usioua mwangosi alikufa nani alikuwa mtawala, rais wa madaktari aling'olewa kucha na meno nani alikuwa mtawala hata leo watu wanakufa na wataendelea kufa,hayo matusi mnayo mtukana magu Kama mwajiri wenu ni watawala hata Mimi hata Mimi natakiwa kufa.
Mwangosi alikufa lakini sio kwa amri ya Kikwete. Kuna tofauti hapo.
 
Back
Top Bottom