Rais Magufuli alivyovuruga Uhusiano na Wadau wa Maendeleo

Maoni mazuri ni kuboresha tuu hatuna haja ya kugombana na wahisani muhimu ni kukaa meza moja na kujadiliana lakini tatizo la wahisani kwakuwa wao wanapesa basi wanataka kila wanalojiskia wao nyie mufanye tuuu.
 
Watu hawajalipwa pesa za kustaafu mwaka ushapita
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani anajua anachokifanya si bure, tulipofikia panasikitisha, tumerudishwa nyuma miaka zaidi 30.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa kweli tuna safari ndeeefu sana! Kama mawazo ya wananchi wetu wasomi ni haya haya ya kufikiri kwamba misaada kutoka kwa wafadhili itatuondolea umaskini na kutuletea maendeleo makubwa basi safari ya maendeleo bado hatujaianza. Tumepata misaada mingi ya kutupumbaza tu toka tupate uhuru. Mpaka tukaitwa eti “darling of donors” ambao ni upuuzi tu wa kutufunga kitambaa cheusi machoni. Misaada yote tuliyokwishapata bado hatukuwa na vituo vya afya vya kutosha, shule za kutosha, umeme wa kutosha, barabara za kutosha, maji ya kutosha, reli na ndege za kutosha, nk, nk. Misaada hii inapokuja utaambiwa dola milioni mia lakini 55% ya pesa hizo inarudi kwao kwa njia ya uani..Inayobaki 45% inalifanya Taifa liwe tegemezi..Misaada hii ni aina ya “ukoloni” fulani ambao ni wa kijanja sana na ndiyo maana hakuna msaada ambao hauna masharti magumu maana ipo kumsaidia zaidi mtoa msaada kuliko mpokeaji. Sasa, awamu ya tano ya Serikali ya Tanzania imeliona hilo na kwa kweli kwa miaka 3 tu ya uongozi wa nchi imefanikiwa kuleta huduma nyingi sana kwa wananchi kuliko kipindi kingine chochote kwa miaka 30 iliyopita.
 
Mkuu kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako kwa uelewa wako mkubwa katika namna ya uchangiaji wa hoja yako.

Kabla sija anza na section yako kubwa ya kukuthibitishia wewe kuwa watanzania hatuna budi kuwa wanyonge kila mara tunaposikia vitisho vya wazungu tuna ingia mteru na badala yake kutembea kifua mbele, nadhani kwanza ungefanya jitihada ya kutambua era za matukio ya maendeleo ya binadam badala ya kukazia mkazo kuwa wakati wa kutoa references zangu nizingatie kuwa North Africa was not Part of Africa.

Ndiyo maana nataka utambue kuwa ukisema maneno "North Africa was not a Part of Africa" ujue pia ni wakati gani au katika era ipi didn't North Africa belong to Africa. Ili uelewe haya yote vizuri inabidi usome vitabu vya zamani kutoka mataifa tofauti ya ulimwengu.

Lazima ukubali kitu kimoja kuwa sisi waafrika tulivamiwa na wazungu kinyume na matakwa yetu, hapo na maanisha mababu zetu. Kwa bahati moja au nyingine sisi wa East Afrika na hasa watanganyika hatukuathirika sana in terms of umwagaji wa damu kama mataifa mengine kama South Africa na mengineyo.

Wewe unajua kuwa sisi, I mean mimi na wewe, ni vizazi vilivyotokea kupata bahati mbaya au nzuri ya kuishi katika kipindi ambacho hatukuwa na jinsi nyingine ya kuishi zaidi ya kukubaliana na hali iliyo kuwepo, yaani ya kwenda shule na ku-participate kwenye madhehebu tofauti ya dini za watawala.

Utanisamehe kwa sasa. Nitarudi kukujibu! Ni maswali mazuri sana. Kuwa na subira kidogo.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaambaa ambaa, badala ya kujibu maswali, ndiyo sifa ya Utanzania. Kumbuka kuna nchi ambazo hazikuwahi kutawaliwa kabisa na hao wazungu. Ziko dunia ya ngapi? Kisha ujue kwamba wazungu hao walitawala Tanzania kwa takribani miaka 70 tu, na tangu tulipojitawala tuna zaidi ya miaka 57. Nipe bado mifano miwili tu ya kitu ambacho tunajivunia baada ya miaka 57, tangu tulipoachana na kunyanyaswa na hao wazungu. Something made in Tanzania, something a prestige of the country. Kwa mfano, wajapani ni watengezaji wa mameli makubwa duniani, watengezaji wa magari bora, wataalam katika electronics,camera nzsuri Japani, pikipiki nzuri Japan, genereta nzuri Japan, n.k.

Kitu gani tunacho?
 

Atakuambia tuna Rais bora duniani!
 
Mkuu umeongea kwa upole ila kiuwoga sana na inaonesha jinsi gani unavyowatukuza hiyo mibeberu eti economic partner tunao takriban 50 years hamn lolote zaidi ya misaad uchwara unayoambatan na sera didimizi wallah magu anajua anachofanya hawa jamaa hawajawahi kuwa wema kwa waafrika zaidi ya maslai makubwa kwao fatilia sera zao kwa afrika ndio utajua kutwa kutoa takwimu za kutufanya tujione wanyonge eti Tz ni Moj ya nchi masikini duniani na kunamisomi humu na elimu zao za kikoloni hata hayoni haya kwa nini wa sitoe takwimu za Tz ni nchi yenye utajiri mkubwa sana ila ni masikini ndio utaona ujinga wa hawa jamaa means wanajua tutashutka kwa sasa amekuja mtu binafsi anaongea ukweli kbs kama utaweka itikadi za chama pembeni au hii kitu mlolishwa eti demokrasia na hata hamtaki kujifunza kuona libya na maeneo mengine afrika kisa mlikaririshwa kuwa hy ni demokrasia nzuri na watesi wenu wa mangaribi na kweli mkasahau kuwa umoja ndio nguvu aloo tutasugua sana ndio maana lijitu linaanzisha uzi likitushawishi tuendele kuwa wanyonge kupiga magoti tu badala ya kutamani kujikomboa kiuchumi hlf unawez kuta jamaa lina phd asee au degrii[emoji848]
 
Akili mgando kabisa hii.Kitu hujui n kuwa hakuna free lunch katika dunia ya leo na hiyo misaada iliyomingi Ina masharti magumu lukuki

Kwa mtazamo uliowazi n kuwa misaada hiyo n maney trap au mitego ya wafadhili kwa nchi maskini kufanyiwa ukoloni mambo leo

Magufuli n Rais pekee aliyethubutu kuweka maslahi ya nchi mbele kwakuhakikisha misaana inakuwa ni ileyenye mashart nafuu na Kuna kuwa na maslah kwq nchi

Usifurahi hata kidogo nchi kuwa top ten ya nchi zinazopata misaada sana Bali furahi pale nchi inapoweza kupunguza utegemezi


Piga kazi changia pato la nchi hamasisha na Alie karibu na wewe afanye kazi tulipe Kodi.Wengi was waliokata misaada n wale ambao masharti yao tumeyakataa na magumu kwa maslahi mapana ya nchi.

Sikuzote watoa misaada wanapenda nchi yetu iendelee kuwa tegemezi ili waendeleee kufaidi kwa mlango wa nyuma.Ukilitazama hili juu juu utamlaumu Magufuli lakini ukijaribu kutumia sehemu ya akili yako vzr kuelewa namna misaada na mikopo inavyotolewa na siasa zake nyuma ya kapeti utakubaliana na mm kuwa n Bora kumuunga Mkono Magufuli kwa jitihada anazofanya.

Rais akimaliza muda wake tutamkumbuka sana ingawa kwasasa kwasababu ya mihemko ya kisiasa baadhi wanamuona Kama ameshindwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…