Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

"Mgogo" sifa zake zimembeba,ni bora tungemtumia positively iwe model kwa watoto wetu wa kike kuliko kumbeza.Kama kuna mapungufu yake yange jadiliwa ofisini ingekuwa na afya.
You are right. Hakuwa professional jana.. he doesnt care about professionalisma at all.
 
Kwakuwa umekiri mwenyewe una thinking capacity ndogo. Ni jambo jema sana wachache sana hukiri mapungufu yao.
 
Kudraw attention za wajinga, wafanye wawe masikini wafanye wawe wajinga ili uwatawale
My Man. Hii ni point ya siku.
Hichi ndicho anachokifanya. Problem is watu wengi ni so dumb to see the big picture. Wengi ni bora liende.
Na yeye ameshajua akili za wabongo wengi zikoje.
Ndio maana anatumia hiyo strategy.
 
Wakikupa nafasi ni kwamba your a bright.. and qualified enough.
Kama wangekuwa wana hila na sis.. basi wangechukua mkenya.. au rwanda au hata south africa.
Na kama ingekuwa ni nafasi regular basi nadhan wangeshajaza watu weusi wa kutosha?
Why mwele?
Because she is bright. Simple as that.
Hizo sababu za hila ambazo huna ushahidi nazo hazitosaidia.
 
Magufuli anapenda sana kile wazungu wanaita "Populist Politics", siku zote anapigana aonekane anawapigania wananchi.

Lkn kwa wajuzi kama sisi sio rahisi kuhadaiwa. Hao hao anaodai kuwa wanampiga vita na sera zake ndio haohao wanaomkopesha hadi sasa amewapiku marais wote waliomtangulia kwa kukopa....!!!

Yeye ashukuru Mungu, hao anaowananga bado wanamstahi lkn siku wakimchoka ndio atawajua vizuri kwani aelewe kuwa hakuna wanachokitaka Tanzania ambacho hakipo kwingineko. Anawahitaji zaidi ya wanavyomuhitaji.
 
Sasa ulitegemea mzungu kama anataka mtu wa kumtumia atamchukua kabwela?
Amachukua wasomi kama hao kina Mwele.
Kwa hiyo watanzania wote walioajiriwa nje wanatumika?
Per your definition.
Tuna ma profesa.. walimu na wataalam mbali mbali wako america na uingereza? Tuseme wanatumika? That bullshit.

Na madai yako kuwa alikuwa anatumika.. una ushahidi nayo? Kama una evidence weka hapa.
 
Sasa wewe unachopinga ni kipi?
Kwamba kwakuwa kuna watu wameajiriwa huko njee basi Mwele hawezi kutumika?
Huu utetezi wako kwa Mwele unasababishwa na nini hasa?

Mwele katangaza kuna Zika ambayi mpaka leo haijaoneokana. Rais kasema yule mtu alikuwa anatumika na rais ana vyombo vingi vya kumpa habari sasa unabisha hiyo zika ipo?
 

Mkuu Bana likasi.

Indoctrination ya kusingizia mabeberu kwa kila mkwamo wa nchi maskini haikutumia syllabus isipokuwa kwa masomo machache kama siasa(msingi na sekondari) na DS(vyuo).

Kwa kiasi kikubwa ilifundishwa nje ya taaluma kupitia matawi ya chama, JKT, na kozi za Kivukoni na nguvu yake ilianza kupotea miaka ya themanini na hatimaye kukoma kabisa miaka ya tisini mwishoni.

Hata hivyo, sidhani kama wengi wa wanaolaumu mabeberu leo ni matokeo ya hayo mafunzo. Kwa kiasi kikubwa hicho kizazi kishajipitia zake mkuu.

Nadhani tunachokiona leo ni mkakati maalum wa kutawala akili za wananchi unaotumia “bottom up ignorant sentiments and top down state propaganda”.

Matokeo yake ni hofu na wananchi kujiona wamezungukwa na maadui na hivyo kuungana nyuma ya mtu atakayeonekana kuwa ndio “mwokozi”.
 
Mimi na shed light. Na usiishie kuniambia rais ana vyombo vingi. Nataka concrete evidence right here. Sio blah blah.
Sipingi kuwa hawez kutumika? But mna ushahid kuwa anatumika?
For the record tu Alikuwa DG wa NIMR.
A leader for ground team iliyokuwa ina conduct research. In their last reasearch waka conclude kulikuwa viashiria vya huu ugonjwa lakin haukuwa hatarishi by then.

If kumpinga. Mngekuja na research yenu ambayo inaipinga research yake. With concrete supportive evidence. Not politics.
 

Wakuu
Ubeberu na ukoloni mambo-leo upo si hapa Tz tu bali katika bara zima la Afrika. Hao watawala wetu wanaotuzuga na siasa zao wanatumikia mfumo huo wa ukoloni mambo-leo. Ni sawa na CEO hapa Afrika anayetumikia wamiliki wa multi national company yenye makao makuu nje. Ndio maana hao ma CEO walifuta somo la DS ili waweze kutuzuga na kutufanya tusahau ukweli huu. Hatulaumu wazungu kama mnavyopenda kusema. Tunalaani mfumo mzima ulio ndani na nje ya nchi - ni mfumo wa kimataifa.
 
Unahemkwa sana na wewe Wasukuma na Wagogo wanautani
mnaona watu wajinga kabisa utani wapi mtu yupo serious kila kukicha Dr Mwele Dr Mwele ....utani wa makabila tungejua ila hii mguu aliotoka nao sio huo
 
Yes lakini kumbuka watoa lawama wengi ni aged above 50 yrs Hawa walisoma chini ya 80 s back Hadi 70 s,ndipo wanazuoni wa ujamaa kina Walter Rodney, Patrick lumumba huyu kada wa ccm Kenya,maprif wengi wazee wa UD Huwa upewa airtime tbc live kuwananga mabeberu sababu syllabus za zamani ziliwafunga akili wasifikirie nje ya ujamaa.

Tofauti na vijana wa Sasa ambao ni exposured society kwa mchango Mkubwa sana wa maendeleo ya technology ambayo yamechangia pa kubwa kuuona ukweli ya kwamba matatizo yetu yametokana na sisi wenyewe na sio external factors Kama walivofundishwa waliosoma syllabus za zamani kupitia masomo Kama historia,siasa,nk.Vijana wengine wa Sasa hasa makada hizi chuki za kuwachukia wazungu wanazitoa kwa boss wao wakiamini fikra za mwenyekiti ni sahihi na lzm zidumishwe bila kureasoning.

Matatizo yetu yamesababishwa na sisi wenyewe na yanaweza tatuliwa na sisi wenyewe, kutawaliwa sio tiketi ya kisingizio cha umasikini. Bali wakomunist utumia nadharia ya kuwalaumu wengine kama njia ya kufichia udhaifu wao wa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi.
 
Pia wazungu wakitaka kukutumia hawamtumii mtu mjinga asie na akili! Wanachukua watu smart wasomi wenye fani zao kama Mwele.
Kuna watz wengi wasomi na wataalamu wazuri wamesomeshwa kwa Kodi zetu Ila wako nje wanafaidisha nchi zingine sababu tumeshindwa watumia sababu si waimba kwaya wazuri Kama cv ya teuzi.
 
Kuna watz wengi wasomi na wataalamu wazuri wamesomeshwa kwa Kodi zetu Ila wako nje wanafaidisha nchi zingine sababu tumeshindwa watumia sababu si waimba kwaya wazuri Kama cv ya teuzi.
Kwa sababu hiyo basi Mwele hawezi kutumika?
 
Ili azile vizuri inabidi atafute uraia wa nchi nyingine otherwise atapata tabu sana au familia yake inapata tabu sana
Ni binti wa Malechela amuombe tu Mungu mzee wake aendelee kuwa hai Hadi huyu mtu amalize mda wake ili asijepata tabu.
 
Kilichomumiza Magufuli ni huyo mama kupewa kazi WHO.

Alitaka akimfukuza ateseke
Hukumtaka, uliona hafai. Wenzio wakamwona anafaa, wewe kuendelea kupiga kelele, wenye akili watakushangaa.

Urais ni nafasi tu, haimaanishi una maamuzi yote dhidi ya binadamu wenzako. Huwezi kuzuia riziki ya watu wote, kwa vile tu wewe ni Rais.

Rais atosheke na adhabu aliyompa kwa kutumia madaraka yake. Asiende zaidi ya hapo. Hapo kawa tu Mkurugenzi wa taasisi ya UN. Siku ik8tokea huyo Mama akija kuwa Rais, si atachanganyikiwa kabisa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani International Org zinaajiri vilaza au waimba kwaya kule ni CV yako na una delivery nn kwenye organization.Kwann huo ukoloni mamboleo uwe kikwazo Africa na usiwe kikwazo Asia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…