Yapo mambo unayoweza kuficha lakini sio ugonjwa, Zika ilikua inasambazwa sana na mbu, ikumbukwe ugonjwa unaoitesa nchi yetu miaka nenda rudi ni malaria kutokana na hali ya hewa na kimazingira inyasapoti mbu wengi kuzaliana. Ikiwa mbu ndo inasambaza zika unadhani rais angeficha idadi kubwa ya wagonjwa wa zika? Huku mtaani Buguruni tungeona wagonjwa wengi wasio wa kawaida.
Ugonjwa wa zika ulikua unasambaa sana duniani kipindi kile, kwa spidi ile kama ulikuepo nchini ni lazima tungeona dalili hata sie tusio wataalamu.
Kuhusu ugonjwa wa covid 19 na rais kuficha data pia ni hisia za watu tu. Kuna kipindi wagonjwa walifika mpaka 190, kama serikali ingekua na nia ya kuficha isingetangaza hata hyo idadi kubwa ya watu 190. Serikali iliamua kutotangaza updates za kila siku kwasababu iliwaongezea wananchi hofu kuliko uhalisia. Wakubwa huko nje wanaposema "maiti zitatapakaa mitaani" alafu serikali kila siku inatangaza idadi ya watu kuumwa, kisaikolojia unatengeneza nchi ya aina gani? Hata hao wanaotangaza wengine wameacha, mfano uganda na suala la muda tu kila nchi itaacha kutangaza na korona itakuepo kwa miaka kadhaa ijayo.
Wazungu hawakupi kazi kubwa na nzuri hivi hivi tu, ni watu wa masilahi muda wote ni hizi nchi zetu za dunia ya 3 ndo sehemu yao ya kufanyia mazoezi. Siamini rais anamchukia dr Mwele.