Rais Magufuli ameamua nchi ifungue sura mpya ya kimaendeleo kuelekea 2025

Safari 2020

2020 kuna safari gani, hiyo ya kutegemea kufanya ukatili kwa uratibu wa vyombo dola? Hamuwezi ushindani na hamtakaa muweze, sana sana mnategemea madaraka ya rais yafanye hujuma ili mfanikiwe kutangazwa washindi. Hakuna mtu mwenye akili timamu atasimama kwenye mstari wa kura ashiriki huo ushenzi unaoitwa uchaguzi. Kama mlipanga kuua watu hizo mbinu elekezeni kwenye mambo mengine.
 

Mleta mada seriously unaamini kuwa REA ni mradi ulionza na JPM?.
Nenda kaangalie risiti zako za kununua Luku kuanzia 2014 kurudi nyuma utaona kuwa ulikuwa ukikatwa kodi kwa ajili ya REA, na vijiji vingi sana vimepatiwa umeme wa REA kabla ya 2015

Na seriously unaamini kuwa SGR ni maamuzi magumu ya JPM?

Ngoja nikueleze sasa kuhusu SGR, SGR ni mradi uliobuniwa, na serikali ya JK, na hata Memoraundum of understanding ya awali kabisa kati yetu na EXIM bank ya China ya mkopo nafuu wa miaka 20 ulishasainiwa na serikali ya JK. Huyu wa sasa alipoingia madarakani alifanya kubadiri mkataba tu, badala ya wachina akawapa Waturuki

Angalia hapa Chini JK anahangaikia SGR kabla hata JPM hajawahi kudhani kuwa anaweza kuwa rais

 
Ametoa hela yake hii right?Magufuli tajiri
 
Nadhani hata RAISI WETU MPENDWA AMEKWISHA SEMA WATANZANIA SIO WAJINGA. hivyo wanaonao yanafanyika na hawana Sababu ya kusoma andiko lako ili wajue.
 
Kama huwezi kujenga hoja bila kutukana huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri.
 
Duh naona umeathirika sana as policies za JPM vumilia sindano imeingia hadi kwenye mfupa huyo unaye muita mshamba ndo kakufanya wewe mtoto wa mjini kulialia na mambo mpaka 2025
2025 hafiki....kama sio Mungu,wananchi au "mabeberu"
 
Umesahau ujenzi wa Kiwanja kipya cha ndege Chato na uzinduzi wa hifadhi mpya ya wanyama Burigi
 
Yaani point zako no.1,3,4,5,8,910,11,12,14,15 zote ni ujenzi,ujenzi,ujenzi it’s boring.

Hivi hakuna mambo mengine ya kufanya kama vile kuboresha maslahi ya wafanyakazi,utatuzi wa changamoto ya wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu kila siku lkn hawana ajira,etc.

Huko kwny miradi mnaishia kusema tu ooh miradi ya ujenzi inaleta ajira kwa wananchi,ajira zipi hizo?labda za kua vibarua huko site.

I bet huko kwny ujenzi kuna ‘wazalendo’ wanapiga pesa nyingi sana kwny hio miradi ndio maana kila wakiamka wana create projects nyingi nyingi za ujenzi ili waendelee kupiga ‘mtonyo’.

‘Wazalendo’ bana.
 
Umetisha sana your real a GT
 
Kama huwezi kujenga hoja bila kutukana huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri.
Na wewe pia kama ni walewale wa kule chatle city....nawe ni 'mshamba tu' tatizo lenu mnamsapoti huyu mshamba kwa mambo ya kipuuzi kabisaaa eti kisa tu ni mtu wa huko kwenu....kweli nimeamini ushamba ni mzigo aiseee
 
Mkuu huyu mshamba atakuongoza wewe mjanja hadi 2025 upo hapo?Huyu mshamba anakufanya ujifiche kwenye ID fake humu, upo hapo?Kwa haya mawili tu Wewe na yeye nani MSHAMBA?
 
Nimeshindwa nijibu nini yeye ni msimamizi wa matumizi wa kodi zetu kwa kuna Rais yoyote duniani anaendesha nchi kwa pesa yake ya mfukoni???

Hayo matusi sio utamaduni wetu watanzania badirika ndugu yangu jenga hoja
Na wewe pia mshamba tu, ni wale wale tu nyie
 
Swali dogo tu kwenye viwanja vya ndege kuwa ye anamalizia malizia tu.Uwanja wa ndege Dar terminal 3 umeanza mwaka gani?Hadi unazinduliwa juzi ni miaka 4 toka utawala wa JPM uanze, Je ni kweli hicho kiwanja JPM kamalizia malizia tu kwa maana ya kazi kubwa ilifanywa na JK?
 

Suala la miradi huwa tunaangalia haswa ni nani aliyeplan kisha akatafuta fedha. anayeplan na kutafuta fedha ni kama ARCHITECT wa NYUMBA yaani , Anayesiamamia ujenzi mpaka ikaisha ni msimamizi tu wa kuwasiamamia mafundi, kuwakaripia hapa na pale wafanye kazi vizuri etc, Sasa huwezi kumlinganisha Architect na msimamia ujenzi aliyepewa ramani na fedha za kuimplement ramani hiyo mpaka jengo likamilike
 
Shida mnashindwa kujua Yote unayoyaona saizi yanatoka kwenye BAJETI YA AWAMU YA TANO. Ukisoma Ilani ya CCM 2015/20 iko wazi kabisa. Kuna miradi inatakiwa kumaliziwa, Kuendelezwa na kuanzishwa.

Sasa wewe ukisema REA kafanya JK sijui kama unataka kusema Jk alipotoka madarakan aliacha hela za kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme hata kama ni hadi 2050.JK kaacha Ujenzi wa Kinyerezi 1 na Jpm kaja kaendeleza kinyerezi 2,wewe ukija na hoja za kinyerezi ni mradi wa JK na JPM hana alichofanya sijui kama unakua na logic. JK kaacha mipango ya SGR,hajaacha hata sent na ilikua iwe mchina lkn JPM kampa mturuki, Reli inajengwa unakuja kusema ni kazi ya Jk na JPM hakuna anachotaka. Hivi huyo Jk toka alipoondoka 2015,haya yote yanayofanyika yeye ndio director?

Mradi wa Bagamoyo ulianzishwa na JK lkn JPM kaja kaupiga chini,kwanini hatuoni kuwa ktk miradi iliyoasisiwa na JK,JPM ananguvu nayo?Nilifuatilia uzinduzi wa hospital ya mloganzila Jk aliacha hatua ndogo sana pamoja na pesa ya mradi, lkn JPM kama Ilani ilivyosema kuwa anatakiwa akamilishe huo mradi tunaona fungu la kukamilisha hiyo hospital lilitoka kwenye bajeti yake.Leo unakuja unasema Jpm hospital ya mloganzila haimuhusu, ni Jk. Uko serious au unafanya SIASA UCHWARA?

Unajua mradi wa REA ulikua ukwame baada ya msaada wa 900B kupigwa chini 2016?Lkn je umekwama?Leo unaendelea kama kawaida, unasema mradi ni wa JK na JPM hana lolote. Are u serious?Miradi mingapi huwa inaishia kwenye makaratasi?Miradi mingapi huwa inakwama na mingine kwenda mwendo wa konokono?Kwamba mlitaka JPM aje apige chini terminal 3,apige chini mloganzila, barabara ambazo hazijaisha aachane nazo naye aanze zake, SGR apige chini au REA apige chini?Nini maana ya mipango ya serikali Kama kila kiongoz ili aonekane kafanya kazi lzm aje na mipango mipya?
 
Hoja namba 2 ndege wakati mmezikimbizia ofisi ya raisi na hamruhusu hata CAG akague we bwege sana,Ajira karibu awamu 4 zimelala mtaani we unajipendekeza ati upate cheo.
 
Mkuu huyu mshamba atakuongoza wewe mjanja hadi 2025 upo hapo?Huyu mshamba anakufanya ujifiche kwenye ID fake humu, upo hapo?Kwa haya mawili tu Wewe na yeye nani MSHAMBA?

Mkuu fake ID zilianza enzi za awamu ya tano!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…