MLETA MADA UNASEMA
HOJA: 1. Ujenzi wa barabara Nchi Nzima kwa gharama Sh. Trilioni 5.3 ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo ya biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.....
JIBU: Acha kutamka tu, sema ni barabara zipi hizo zinazokusudiwa kujenga, Tunachojua ni Kwamba Barabara zilijengwa za kuunganisha Kila mkoa na almost kila wilaya wakati wa JK , Na huyu JPM ndiye aliyekuwa msiamazi mkuu wa ujenzi huu!. Siku nyingine badala ya KULETA FIGURE pekee ili kuibua hisia leta mifano halisi.
HOJA: 2. Ununuzi Ndege Mpya Sh. Trillioni 1.3 ili kuchochea sekta ya Utalii na Biashara ya ndani ya nchi yetu...
JIBU: Ni utafiti gani umeufanya kuwa Ununuzi wa ndegu Unaongeza utalii?, maana kudhani kuwa na ndege ndo kuinua utalii ni dhana potofu, kwa mfano takwimu ziko wapi kuonyesha kuwa ununzi wa ndege umechochea utalii?. Takwimu ziko wapi zinazoonyesha namna Ndege tulizonunua zimestimulate utalii?. Operation cost za kuendesha hizo ndege ukilinganisha pesa zinazoingiza ni kiasi gani?, lete takwimu ndugu, usiorodheshe vitu kama listi ya wachezaji wa pira oyesha impact ya kitu. Tunachojua ni kwamba biashara ya ndege ni baishara pasua kichwa, na Taarifa za PAC na ripoti za CAG zimeonyesha miongoni mwa mashirika yanayopata hasara mpaka sasa ni ATCL, hizo ndege zimetusaidia vipi?. Lakini pia hizo ndege zimenunuliwa bila pesa kuidhinishwa na bunge, ndege zimenunuliwa kwa utashi tu bila kufuata sheria, hatujui tumepigwa au la, inabidi kamati maalum ya bunge au CAG achunguze hili.
HOJA: 5. Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) Sh. Trillioni 7 baada ya kukaa na reli ya mkoloni tuliyorithi zaidi ya miaka 200 iliyopita....
JIBU: Mleta mada, seriously unaamini hatujawahihi kuwa na reli nyingine isipokuwa iliyoaachwa na mkoloni?. Reli ya TAZARA unaijua?
HOJA: 9.Ukarabati Viwanja vya Ndege Nchi Nzima Sh. Trilioni 1.8
JIBU: Ukarabati wa viwanja vya ndege nchi nzima ulifanywa kwa asilimia kubwa na serikali iliyopita ya JK, labda utuambie kuwa huyu anamaliziamalizia kazi na pia gharama kubwa hapo imetumika kwenye ujenzi wa Uwanja mpya wa Chato usio na faida yoyote ya maana kiuchumi kwa nchi
HOJA: 11. Miradi ya Usambazaji Umeme vijijini kupitia Rea Umeme unaendelea kuchomoza vijijini...
JIBU: Usitutanie kuhusu REA, Sema JPM anaendeleza REA, lakini REA ilikuwepo toka awamu iliyopita, watu wamekatwa kodi wakati wakinunua umeme wa LUKU kwa ajili ya REA kwa muda mrefu kabla JPM hajawa raisi, na kukuonyesha kuwa REA ipo toka awamu iliyopita mimi kwa mfano umeme wa REA ulifika kijijini kwetu toka mwaka 2013 wakati wa JK
HOJA: 13 Ununuzi wa vivuko vya Majini maeneo mbalimbali ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo ya biashara.....
JIBU: Hujaeleza kivuko gani?, Maana huyuhuyu JPM alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ujenzi alikuwa akisifu kila wakati kuwa JK kanunua vivuko vingi sana hapa nchini, Msidhani watanzania hatuna kumbukumbu vizuri na msitake kusafiria nyota za wenzenu , tengenezeni Legacy zenu lakini msiibe legacy za watu
HOJA : 14. Ujenzi wa madaraja mfano Mfugale, Ubungo interchange, Surrender bridge n.k
JIBU: Daraja La baharini la Surrender siyo necessity ya Mtanzania ni la show off zaidi kuliko haja na umuhimu wake, Daraja la Mfugale, pesa ilitafutwa na utawala uliopita na mikataba ilisainiwa na utawala uliopita. Hebu Linganisha Significance ya madaraja hayo na daraja kama la Mkapa lilojengwa na BWM, Malagarasi, Kilombero, Kigamboni yaliyojengwa na JK . Hayo ndiyo madaraja ya Legacy na kujivunia kwa mtu mwenye hadhi ya Raisi siyo daraja la Flyover ya Mfugale
HOJA: 15. Miradi ya Maji inayoendelea Kujengwa Maeneo Mbalimbali ya Nchi yetu ni mapinduzi kwenye sekta ya Maji.....
JIBU: Mkapa alileta maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga, Kikwete akatutengenezea mradi mpya kutoka Ruvu chini kupitia bunju kuja mpaka Dar, Visima kibao vilijengwa nchi nzima!. Upo wapi mradi wa scale ya ule wa BWM au JK katika serikali hii?
Baada ya kukujibu hoja zako nikueleze sasa mambo ya msingi sana ambayo yanatugusa wananchi serikali hii haijafanya
1. Haiheshimu katiba iliyoapa kuilinda, kuna uonevu uliokithiri nchini kwa watu na taasisi mbalimbali kama vile wanasiasa wa upinzani, waandishi wa habari, vyama vya siasa etc
2. Wakulima wameendelea kutendewa visivyo haki, wakulima wa korosho walichukuliwa korosho zao kinguvu, zao la mbaazi limevurugwa, Zao la kahawa limeveurugwa
3. Wafanyakazi hawapewi stahiki zao kwa mujibu wa sheria za kazi, nyongeza ya kila mwaka iliyopo kwa mujibu wa sheria haipo
4. Wastaafu wanahangaika, wanapigwa danadana nenda rudi, wengine wanakaa miaka kibao bila mafao
5. Hali ya usalama wa wananchi iko matatani, watu wanatekwa, wengine wanapotea katika hali ya kutatanisha, watu wanaogopa hawajui fate yao itakuwa nini
6. Biashara zinaporomoka, Juzi hapa wafanyabiashara wamekiri jinsi TRA ilivyokuwa ikiwanyanyasa, biashara nyingi zimefungwa, maisha yamezidi kuwa magumu
7. Kilimo kiko arijojo, bajeti ya kilimo imezidi kupungua mwaka after mwaka, Pesa zinazopelekwa kwenye kilimo wakati mwingine haifiki hata asilimia 30 ya bajeti iliyotengwa, katika hali kama hii utainuaje hali za watanzania wakati zaidi ya asilimia 70 ya watu wetu wantegemea kilimo?
8. Ajira zimeendelea kuwa bomu linalosubiri kupasuka, mwaka wa 4 huu serikali inasuasua kwenye ajira, hata sekta binafsi ambayo ingebidi iisaide serikali kuajiri inasuffer, Sekta binafsi imekuwa paralysed, sasa katika hali kama hii Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato au daraja la Surrender unawasaidia vipi vijana?. hata pesa ambazo inabidi zitengwe na Wakurugenzi kwa mujibu wa sheria hazitengwi, wewe mwenyewe unalifahamu hili vizuri
HITIMISHO:
Mleta mada umeleta habari za utendaji wa awamu hii lakini ambacho hujakisema ni kwamba miradi mingi inayofanyika kwenye awamu hii ni miradi iliyoanzishwa kutafutiwa fedha na serikali zilizopita, kwa hiyo awamu hii inamaliziamalizia na kuongezea hapa na pale palipopungua
Pili, Miradi mikubwa kama SGR inatoa pesa nje badala ya kuingiza pesa ndani, Chuma tunatoa nje, kabla ya kuanza ujenzi pale tungehakikisha tumewekeza Liganga na mchuchuma ili tutumie chuma chetu cha humuhumu nchini ili pesa nyingi zaidi ibaki ndani etc, Lakini pia miradi mingine siyo Miradi PRIMARY kwa uchumi ni miradi SECONDARY kiuchumi kwa mfano mradi wa uwanja wa ndege Chato au Daraja la kupitia "Baharini" la Surrender
Tatu miradi hii inafanyika wakati maisha na mahitaji ya watu hayaguswi ipasavyo, Mkulima kama vile wa korosho, kahawa,etc ameendelea kutopewa umuhimu wa maana, Ajira za wananchi ziko chini, Private sector imesuffer mno ndani ya miaka hii minne.
Hali ya Kidemokrasia na kuheshimu viapo vya uongozi kama vile NAAPA NITALINDA NA KUTETEA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOWEKWA KWA MUJIBU WA SHERIA, NA KWAMBA KATIKA KUTIMIZA MAJUKUMU YANGU SITAPENDELEA WALA KUONEA MTU.....haviheshimiwi ipasavyo viapo hivi
NAWASILISHA
Ni mimi:
Missile of the Nation (Komboro hatari la Ulinzi wa Taifa)